Mechi gani ya Watani wa jadi (Simba na Yanga) unaikumbuka zaidi?

Mechi gani ya Watani wa jadi (Simba na Yanga) unaikumbuka zaidi?

Wewe inaelekea ni shabiki wa Simba wa kizazi cha kuanzia miaka ya 2000....inawezekana ulizaliwa miaka ya 2000...waulize wanaojua historia ya timu hizi mbili ni ipi kati ya Simba na Yanga imemfunga mwenzie mara nyingi...
Hivi rekodi ipo vizuri Hadi kwenye makombe ya mapinduzi,kagame,Tusker challenge,Taifa cup? Mtani jembe,ngao ya hisani n.k n.k....kwa ligi yanga imezidi kufunga Simba ila Sina hakika kwa mashindano yote Kama yanga kamzidi Simba....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia inaonyesha mechi kali ni ile ya 1987 marehemu Sahau Kambi akiwabeba mikia wasishuke daraja na Fred Felix Minziro akimshushia kipigo cha mbwa mwizi Kambi
Daaah ilikuaje hii Mkuu
 
Ile mechi ya 4-1 iliuzwa...Wale wafanyabiashara wa kiasia waliokuwa wamejazana Yanga kwa madai ya kuifadhili walikula njama kwa lengo la Yanga ifungwe ili George mpondela ''Castro' aliyekuwa madarakani kama Katibu Mkuu ang'oke madarakani...'Castro' alikuwa hataki Yanga ijiegemeze kwa wafayabiashara hao wa kiasia...Hii ni sawa na mechi ya 5-0 ambapo mfanyabiashara mmoja wakiwemo baadhi ya vizee vya Yanga walikula njama Yanga ifungwe nyingi ili mwenyekiti Nchunga ang'oke madarakani na alifanya hivyo baada ya kichapo hicho ...Mechi ya kihistoria ya Yanga na Simba ni ile ya mwaka 1974 pale Nyamagana Mwanza ambapo Simba alilala 2-1. Wafungaji Yanga ni Gibson Sembuli na Sunday Manara na Simba ni Adam Sabu. Mechi hii ilichezwa dakika 120 ...Sunday alifunga goli la 2 kwenye dakika za nyongeza ...Yaani kwenye dakika 15 za mwanzo za nyongeza. Sembuli alisawazisha dakika ya 87...Adam Sabu alifunga goli la Simba kipindi ha kwanza kati ya dakika 16 na 20....Hiyo ndiyo ilikuwa game ya ukweli...Simba walilalamika kwa goli la Sembuli wakidai kuwa alifunga wakati dakika 90 zimemalizika ...waliwasilisha malalamiko hadi CAF lakini haikusaidia kitu...ukweli goli lile lilifungwa ndani ya dakika 90....Mechi hii ilikuwa na hisia kali sana miongoni mwa mashabiki wa timu zote mbili..Yanga ilikuwa ikiigaraza Simmba kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 1968 hadi mwaka 1972. Na mwaka 1973 Simba ilijikomboa kwa kuifunga yanga goli 1-0 goli lililofungwa na Willy Mwaijibe kama sijakosea..kumbukumbu zinanitupa kidogo inawezekana ni Haidari Abeid...........Mwaka 1974 timu zote mbili zikajiandaa vilivyo..Kabla ya michuano ya ubingwa kuanza Simba ikaenda Poland kwa mazoezi Yanga nayo ikaenda Romania ...Ikawa ni vita...Yanga anataka kuifunga Simba akidai kuwa simmba ilibahatisha tu mwaka 1973...Simba nayo ikaona kuwa ni lazima iendeleze kichapo kwa Yanga...Siku ya mechi pale Nyamagana nchi ikasimama...masikio ya mamilioni ya mashabiki wa pande zote mbili yakaelekezwa Mwanza...Kulikuwa hakuna TV watu wanasikiliza kupitia RTD na viredio vvya dudu proof...betri za redio kabla ya mechi zikawa zinaanikwa ili kuongeza nguvu ..Baada ya game wapenzi kadhaa wa Simba waliripotiwa kujinyonga na kufa kukwepa muendelezo wa masimango mitaani..kwa mfano kule Tabora mnazi mmoja wa Simba aliamua kujitumbukiza kwenye pipa la pombe aina ya kangara iliyokuwa jikoni....Baadhi yetu tulikuwa wanafunzi sekondari na wakati wa mechi hiyo tulikuwa likizo...sasa shule zilipofunguliwa baadhi ya wanafunzi manazi wa Simba walichelewa kuja shuleni kukwepa kejeli za manazi wa Yanga...Mchezo ule ulitungiwa kitabu na goli la kusawazisha la Sembuli likawa kwenye mchoro kitabuni kuelezea namna lilivyofungwa...Kama sijakosea mwandishi wa kitabu kile aliitwa Hadji Konde.....Nakummbuka Sembuli alifunga goli lile kwa pasi ya Kichwa ya Kitwana Manara ....Aisee ilikuwa raha sana...Kwangu mimi haitatokea mechi kama ile iliyojaa hisia kali..Katika mechi ile ya Nyamagana mchezaji nyota wa Simba, Saad Alli...alizirai uwanjani dakika za mwanzo kabisa na kukimbizwa hospitali ya mkoa wakati ule nadhani ni Sekou Toure pale Mwanza....ilikuwa ni katika dakika za mwanzo kabisa za mchezo...Mengi yalisemwa kuhusu kuzirai kwa Saad Alli wengi wakihusisha na imani za ushirikina... .
Mkuu umeiva aisee
 
Ile game I think it was 1994, naikumbuka sana kwa sababu 1993 yote Yanga walitutesa kupitia Kizota na Lunyamila.

Sasa siku ile George Masatu ndo alianza kufunga, Kimanda akarudisha. Tukaja kumaliza na goli 4, nakumbuka tulizunguka mji mzima tunashangilia.

Nilirudi home saa 6 usiku, mama akagoma kunifungulia, dingi anauliza nilikuwa wapi nikamwambia. Akasema ingia ndani, bila zengwe.
Mkuu yaani miaka hiyo kijana wako nlikuwa bado chalii
 
Wakuu tujadili hii gemu kesho ndo kinanuka tena. Nani mwanakulipata mwanakulipewa kesho?
 
Mm nakumbuka mechi ya simba na yanga mwaka 1985..
Front line ya simba ilikuwa zamoyoni mogela,..,zuberi magoha..Sunday juma.
Huku beki za yanga kuna Athuman juma chama Jogoo..rasheed IDD chama,,ahmedi amasha..Yusuf bana.
Nakumbuka mogela alirukiwa miguu miwili ya kichwa na athumani chama,,
Watu tulidhani hatorudi uwanjani,, Mogela alirudi kavaa usongo kwa bendeji kichwa kizima..
Uwanja mzima shabiki wa mnyama tulilipuka kwa furaha..
Hizo ndy zilikuwa mechi za ushindani kipindi hicho.
 
Tarehe 16 kinawaka tena.

Safari hii wanakutana wote wakiwa vizuri.

Unampa nani ushindi?
 
Zikiwa zimebaki siku chache mapacha wa Kariakoo (Simba na Yanga) watakutana uwanjani tar 16/4 jumapili kukabana makoo.

Ukiwa Kama shabiki kindakindaki wa timu Kati ya hizo mbili Simba/ Yanga.

Njoo utueleze hapa ni Derby gani ambayo ilikuumiza roho/kukufurahisha?

Ukitaja na mchezaji aliyefunga/kukufunga na siku yako kuwa mbaya/nzuri itapendeza zaidi.

Screenshot_20230412-100838.jpg

 
Zikiwa zimebaki siku chache mapacha wa kariakoo (Simba na yanga) watakutana uwanjani tar 16/4 jumapili kukabana makoo.

Ukiwa Kama shabiki kindakindaki wa timu Kati ya hizo mbili simba/ yanga.

Njoo utueleze hapa ni Derby gani ambayo ilikuumiza roho/kukufurahisha?

Ukitaja na mchezaji aliyefunga/kukufunga na siku yako kuwa mbaya/nzuri itapendeza zaidi.View attachment 2585127
Lile goli la Morrison kwa Manula tukiwa na timu ya kuunga unga.
 
Back
Top Bottom