Mechi gani ya Watani wa jadi (Simba na Yanga) unaikumbuka zaidi?

Duuh mzee heshima yako! Wenzetu mlifaidi kuona vipaji halisi kipindi hichoi! Siku hizi msisimko wa pambano la watani wa jadi umepungua sana! Mzee tukumbushe na ile simba aliyotia mpira kwapani!

hahahahahaha ile game nilikuwepo uwanjani uwanja wa taifa sasa uwanja wa Uhuru...Yanga ilikuwa na kikosi kikali sana...Akina Sanifu Lazaro na wengineo..Simba nayo ilikuwa na vijana wazuri lakini kiukweli Simba walikuwa underdog kwa Yanga...Simba katika game ile kipindi cha kwanza walicheza rafu za ajabu na za kushangaza lakini hakuna kadi nyekundu iliyotolewa kwa mshangao wa wengi...Refa alikuwa ni Hafidh kutoka Zanzibar sasa ni marehemu ...wakati anafariki alikuwa ni Mbunge....Kipindi hicho cha kwanza mpira ulikuwa unachezwa kwenye lango la Simba lakini matokeo bado yalibaki 0-0 na hakuna kadi iliyotolewa kwa Simba pamoja na rafu za ajabu...Kepteni wa Simba alikuwa nadhani ni Method Mogella akicheza namba nane...msimu uliofuatia Method alihamia Yanga ambako alikuwa anacheza namba 4 au 5...sasa katika game ile Simba wakagoma kuingia uwanjani kipindi cha pili...Ilifahamika baadaye kuwa Simba walikuwa wanafanya rafu makusudi ili wapewe kadi nyekundu na iwe ndiyo sababu ya wao kususia mechi kwa kisingizio cha kuonewa...Ilifahamika baadaye kuwa refa aligundua janja hiyo ya Simba na ndiyo maana akawa hawapi kadi....Na habari ambazo hazijathibitishwa zinasemma kuwa ndani ya uwanja Hafidhi aliwaambia wachezaji wa Simba kuwa hatawapa kadi nyekundu ila watafungwa tu kihalali...Kiukweli Simba walizidiwa mno game ile na wangerudi tu uwanjani wangepigwa nyingi...hawakuingia uwanjani kipindi ha pili kukwepa aibu ya kufungwa.....
 
Hii match nilikuwepo Uwanjani nikiwa bado Kijana mdogo kabisa.
 
4-3 2010 hilary echesa anapiga mashine moja toka katikati ya uwanja dk za majeruhi
 
Hivi kwanini yanga wakifungwa na Simba wanadai hujuma lakini wao wakishinda wameshinda kihalali hata Kama goli limefungwa kwa mkono
 
Usipotoshe,Yanga ilizidiwa kiuwezo.
Kama Yanga walikula mlungula je mechi ya Jana walikula nini
 
Mechi ya 3-3 haiwezi kusahaulika kwa muda mrefu. Haikuwa mechi yenye msisimko sana nje ya uwanja lakini uwanjani ilikuwa ni burudani mwanzo mwisho. Hakuna dkk ya mchezo ambayo haikuwa na maana.

Yanga iliperform kwa kiwango cha juu sana katika kipindi cha kwanza huku Simba ikionekana kuzidiwa kila eneo. Kipindi cha pili ilionekana kinyume chake. Vijana wadogo wa Simba wakiongozwa na Said Ndemla na William Lucian, walitandaza kabumbu la karne na kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo vijana walizidi kuwa watamu. Ni mechi ambayo kila timu ilicheza kwa kiwango cha fainali ya Ligi ya mabingwa Africa lakini katika dkk 45 tu kila moja.
 
Nakumbuka hii mechi kwenye kibandaumiza mashabiki wa simba tulikuwq wqtatu tu lakin was Jangwan walikuwa kama wote
 
Mechi hii akina Azim Dewji na wenzie walinunua.
 
Kwa umri wangu, ile mechi ya goli 3 - 3
Picha linaanza Ngasa anaahidi kama hataifunga Simba, atachoma moto nyumba yake Mwanza. Daah!! Kweli kijana akatufunga Simba, huku nikikerwa na Shangilia ya Hamis Diego Kiiza ile kama anatetema aiseeee....Kipindi cha kwanza tumeloa 3 nunge, napigiwa simu na watu wa Yanga, wakiongozwa na Kaka yangu mnazi mkubwa wa kwasukwasu akijinasibu leo tunawalipa zile 5. Kipindi cha Pili anaingia Ndemla na William Lucian, huku kocha Kibaden akionekana hana wasiwasi kabisa.... Yule beki mrundi anachomoa bao la 3 aisee nilishangalia sana. NAIPENDA SIMBA.....(kama isingekua ubora wa Kakolanya 2018 Yanga ilikua afe 5 tena, bahati ilikua upande wao)
 
Mwaka 1947 hii mechi ni kama naiona hivi.game ilikuwa tight kinyama. Wanaume walikuwa wanatunduana uwanjani kunawaka moto.ile mechi ilikuwa inashuhudiwa na maelfu ya watanzania uwanjani. Simba walikuja kushinda kwa mbinde bao 3-0 kama sikosei.
 
Simba ilishinda 5-0; nilikuwa Taifa kushuhudia hii kipande ya historia.
 
4-3 2010 hilary echesa anapiga mashine moja toka katikati ya uwanja dk za majeruhi
Hiyo mech ilikuwa mzuri sana. Tegete alitia 2 kama sikosei. Kwa simba uhuru suleiman alikuwa kwenye kiwango bora sana.japo timu yangu ya yanga ilifungwa lakin ilicheza vena sana
 
 
Yanga unijitetea tu
Mechi nyingi simba anakuwa na nafasi ya kupata matokeo chanya kuliko Yanga.
 
Ile Volley ilikuwa hatari sana.
Japo kwangu mimi game nzuri ni ile tuliyosawazisha goli tatu tukiwa na kikosi dhaifu kuwa wao.
4-3 2010 hilary echesa anapiga mashine moja toka katikati ya uwanja dk za majeruhi
 
Yanga unijitetea tu
Mechi nyingi simba anakuwa na nafasi ya kupata matokeo chanya kuliko Yanga.

Wewe inaelekea ni shabiki wa Simba wa kizazi cha kuanzia miaka ya 2000....inawezekana ulizaliwa miaka ya 2000...waulize wanaojua historia ya timu hizi mbili ni ipi kati ya Simba na Yanga imemfunga mwenzie mara nyingi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…