Uchaguzi 2020 Mechi kali nne za Uchaguzi Mkuu wa Wabunge ni majimbo ya Arusha Mjini, Kawe, Mbeya Mjini na Tarime Vijijini

Vijana wengi mpo kwenye social Media kwa ajili ya porojo, Mmegeuza hii mitandao kana vijiwe vya porojo.

Kwa uhalisia kabisa ukiondoa ushabiki wa vyama sisi kama Watanzania tunatakiwa kufanya tasmini. Halima Mdee mbunge wa Chadema Jimbo la Kawe ni nani kati yenu humu anaishi jimbo la Kawe anambie Halima Mdee 2015/2020 hii amemuona Halima jimboni anafanya hata mkutano na wananchi au anafanya siasa jimboni kwake au ameongelea hata jambo moja linalowahusu watu wa Kawe.

Mimi nipo Bunju kama mbunge wa Bunju ndio Halima asahau kura za watu wa Bunju kuna kero Bunju mbaka basi lakini hatuna mwakilishi bungeni.
 
Sasa Askofu Gwajima umeingia rasmi ktk siasa za Tanzania.

Umechaguliwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la kawe. Unajua kuwa uchaguzi mkuu unaambatana na figisufigisu ikiwemo wizi wa Kura.
Kwa wadhifa wako wa Uaskofu Sitegemei kuwa utajihusisha na mchezo mchafu wa kukubali kupewa ubunge wa kutangazwa pasipokuwa na kura za kutosha, yaani kutotenda haki.

Itabidi uonyeshe njia ya kushinda kwa haki au kukubali kushindwa kwa haki.
 
Ongeza Vunjo na Rombo
 


Ujumbe huu umetolewa baada ya kujiridhisha kwamba Mrisho Gambo mbali na kuchaguliwa baada ya "KULIPIA UKUMBI" haungwi mkono na wanaCCM wachache waliopo Arusha, itambulike kwamba watu wa Arusha wanazo kadi za CCM kwa sababu maalum bali ukweli hawajawahi kuwa wana CCM.

Kura zote ni kwa Mh Lema
 
Yule siyo askofu yule ni mwizi kama walivyo majizi wengine! askofu wakweli ubunge kwake wa kazi gani wakati kondoo wa bwana wana msubiri.
 
Mechi za kibabe. Hapo mtoto hatumwi sokoni. Heche na Waitara wanawezana. Namsikitikia Sugu. Watu wa Mbeya kwa Polisi ni wepesi. Halima kwa Gwajima atafute kazi ya kufanya. Lema na Gambo hapo ni moto. Muda ni mwalimu, yangu macho.
Naona umesahau msaada uliombwa jkt mafinga na itende na haikuwezekana kutuliza fujo

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
UCHAGUZI DERBY:

Gambo vs Lema
Mdee vs Gwajima
Dr Tulia vs Sugu
Waitara vs Heche
Kimei vs Mbatia
 
Hii Vita naisubiri Sana yaani.

Best friend wangu na Mwana familia mwenzetu wa IHUNGO BOYS HIGH SCHOOL 2O12 ambae alikua Diwani wa chadema kata ya butimba mwanza Alie maliza muda wake Ndugu JOHN JUSTIN PAMBALU VS STANSLAUS MABULA. Naiona njia nyeupe mapema nyamagana ikirudi upinzani.

Labda watu wapande juu mbinguni wakazibe.

Siasa za nyamagana hazirudishi MTU bungeni MIAKA 10
 
Kama kawaida wabongo washakuwa kina Sheikh Yahya.

Jitokezeni mkapige Kura siyo mnakaa nyumbani mnasubiri matokeo.

Na nyie NEC msichezee sanduku la kura tunawaonya mapema.
 
Ukweli mchungu

Gambo in, Lema out

Mdee in, Gwajima out

Sugu in, Tukia out(itatokea fujo ambayo haijawah kutokea nchi hii)

Heche in, Waitara out
 
Haya majimbo yote ni chadema, umesahau moshi mjini, hai, tunduma ,iringa mjini,kibamba na mengine mengi
 
Kwa kawe Sina shaka na ushindi kwa Mdee, ccm kinachowasumbua Jimbo la kawe ubungo kibamba wakaazi wake %kubwa Wana elimu na kipato Cha haja, mtu aliyeelimika kudanganyika ni ngumu Sana....
 
Sina uhakika kama Sugu na Halima watarudi
Halima atarudi kupitia viti maalum ambavyo tayari alishagombea na kupitishwa na chama chake. Alishajua kurudi kupitia ubunge wa majimbo kwake haitawezekana. Sugu, Lema, Heche na Msigwa ndiyo basi! Inatia huruma.
 
Hata Bill Clinton aliekua rais wa Amerika alipatikana na issue kama ya Gwajima ,hakuna jipya chini ya jua
Kwaiyo Bill Clinton alikuwa ni pastor kabla ya kuchaguliwa kuwa wa marekani!!!?[emoji15][emoji22]
 
Halima atarudi kupitia viti maalum ambavyo tayari alishagombea na kupitishwa na chama chake. Alishajua kurudi kupitia ubunge wa majimbo kwake haitawezekana. Sugu, Lema, Heche na Msigwa ndiyo basi! Inatia huruma.
Unafikiri watu wa Kawe ni kama watu wa Kondoa au Kongwa Dodoma huko???? Utapata majibu October
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…