Mechi ya Azam FC Vs Kitayosce imemalizwa kabla ya muda baada ya Kitayosce kubakiza wachezaji pungufu uwanjani

Mechi ya Azam FC Vs Kitayosce imemalizwa kabla ya muda baada ya Kitayosce kubakiza wachezaji pungufu uwanjani

Unawezaje kuchezesha timu ina wachezaji pungufu ( wanane ) uwanjani halafu baadae uje utoe kiatu cha mfungaji bora?

Hizi mambo mbona ni uhuni mwingi sana?
Hivi kulikuwa hakuna njia nyingine hili lisitokee?

Nimesikitishwa sana na huu uhuni wa leo
Kwani kanuni zinasemaje?
 
Yeye yuko kazini anatimiza wajibu.wanaotakiwa waone aibu ni viongozi wa hiyo timu kufanya mambo kibabaishaji.Walikua wapi siku zote kuweka mambo yao vizuri.
Ila hako kambinu ka kuumia kamewasaidia sana kitayse!!

La si hivyo wangepigwa hata hamsini[emoji1787][emoji1787]
 
Timu haijakamilisha taratibu za usajili na kwa hivyo wachezaji walioruhusiwa ni wanane tu.

Kipa kwa sasa ameumia mchezo umesimama.Wamebaki 7 uwanjani na hakuna sub hata mmoja
wachezaji nane uwanjani mechi inapigwa kama kawaida ila wasipungue chini ya wachezaji saba..
 
Fesal hajatoka bure!

Goli tatu sio haba[emoji1787][emoji1787]
 
Sasa wanacheza je nane uwanjani?? Kwani wachezaji wengine wa akiba wako wapi
Nafikiri kufungiwa na FIFA Usajili na pia hawakuwa wamesajili wachezaji wengine rasmi kulingana na TFF ao wachezaji 8 tu ndio wamesajiliwa na wana stahili kucheza ligi na ndio hao walioanza. Kisheria na toka tukicheza michangani, hakuna mechi itakayochezwa au iendelee ikiwa timu moja ina wachezaji chini ya 7. Kipa na jamaa kujiangusha na kusingizia kuumia walikuwa sahihi kabisa na game imeisha sasa huku Azam ikipewa point 3 na goli 2 za mezani.
 
Hii timu ilisafiri kwa mafungu (Batches) Nini? Iweje timu inaingia uwanjani haijatimia?!!
 
Live from chamaz,mpira umesitishwa,kutokana na sheria ambayo hairuhusu mchezo kuendelea iwapo,wachezaji watapungua saba...ingawa fei toto kapewa mpira wake..sasa sjui imekuaje???[emoji1787][emoji1787][emoji1787]poor poor poor kwa TFF
 
Back
Top Bottom