Mechi ya Barcelona na Juventus leo Juni 5, 2015

Mechi ya Barcelona na Juventus leo Juni 5, 2015

Kama ni kanuni, kanuni inasema matokeo ya mpira ni dakika 90! Kanuni haisemi barca achezapo lazima ashinde. Ndiyo maana wakali wa darajani walimkalisha barca akiwa kwao. Na msimu huo ndoo ya UEFA ilienda darajani!

hahahaha jua ndo lile linazama, masaa yanayoyoma kuashiria hivi punde barca anaenda kukamilisha ratiba, anaenda kujitwalia mwanamwali.
 
messi atapiga goli mbili takatifu huku neymer akiweka kimiani goli moja lililojaa ufundi wa kutosha na kuisisimua jumuiya ya wapenda soka duniani. Goli la Neymer litatokana na pasi bora kabisa kutoka kwa fundi wa mpira duniani yaani messi. Goli la kwanza ambalo litafungwa na Messi katika dakika ya kumi na sita litatokana na pasi nzuri kutoka kwa suarez ambaye atafanya maajabu mengi sana uwanjani ambayo ni nadra kuyashuhudia katika kizazi, hakika itakuwa gumzo kubwa duniani. Dakika tatu kabla ya kipindi cha kwanza kuisha fundi Iniesta atapiga pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja na pasi hiyo itamfikia Messi ambapo atafanya manyanga pale na kiwatoka mabeki takriban watatu na kutupia wavun goli moja la ukweli sana. kwa upande wa juve watacheza jihad na kubahatika kupata goli moja ambalo halitaeleweka limefungwaje maana itakuwa ni butua butua tu hamna ubunifu, ufundi wala umaridadi wowote, hiyo ni katika dakika ya themanini na mbili ya mchezo. Hivi ndivyo itakavyokuwa.

Hongera kwa ndoto nzuri ya mchana! Lakini usiku utakiota kibibi kizee kwa ndoto halisi!!
 
Kule Juve kuna Pogba,Vidal na Tevez mtanange hautabiliki huu
 
hahahaha jua ndo lile linazama, masaa yanayoyoma kuashiria hivi punde barca anaenda kukamilisha ratiba, anaenda kujitwalia mwanamwali.

hakika mkuu leo tunakamilisha ratiba
 
Hongera kwa ndoto nzuri ya mchana! Lakini usiku utakiota kibibi kizee kwa ndoto halisi!!
ha ha ha ha ha ha ha ha mkuu nakusikitikia kwa
kupambana na barca uwanjani mmeishindwa vijiweni mtaiweza??
 
Nimeota mchana huu.. juve 4 barca 3... sasa nyie bisheni

Madokta wanashauri mtu ale kiasi kabla ya kulala. Ukishiba sana utasababisha upate maruweruwe kama uliyoyapata wewe. mkuu zingatia maelezo ya madaktari kwa ajili ya afya yako
 
Kwa niaba ya jumuiya hii kubwa ya jf nimezungumza na wataalamu mbali mbali, tazama wanauchumi, wanafizikia, wachambuzi wa soka, wanasaikolojia na wanazuoni wengine kibao na wote wameonyesha imani yao kubwa kwa club ya wananchi duniani, barcelona. "kimahesabu kwa kweli barcelona ameishachukua kikombe na hakuna wa kuzuia hilo" alizungumza kiufundi mtaalamu fulani wa hesabu. Nyinyi mnaobisha hili humu ndani mnataka nini?

Hahahahahaha unaleta habari za ukawa humu tayari naona. Ila nashukuru umekuwa na maono kama yangu..... #teambarca ooooooooiiy
 
hahahaha hawa watu hadi nawaonea hiruma, hivi kwanini wanajitesa kwa kushabikia timu ambayo kwa namna yoyote ile haiwezi kushinda? Hivi kweli kabisa mtu unaishabikia juve na kuiacha barca?

Haya! Naona wewe unakisikiaga tu kibibi kizee cha Turin!! Chonde Chonde! Barca nini Bwana? Unataka kutuambia kuwa hujawahi kushuhudia barca akichezea kichapo tena kwao! Jiandae kisaikologia! Juventus 3-0 barca!
 
Hongera kwa ndoto nzuri ya mchana! Lakini usiku utakiota kibibi kizee kwa ndoto halisi!!

mkuu natumia mahesabu kuchambua haya mambo, naongozwa na principles, kumbuka namba hazidanganyi mkuu.... barca anachukua kombe
 
Haya! Naona wewe unakisikiaga tu kibibi kizee cha Turin!! Chonde Chonde! Barca nini Bwana? Unataka kutuambia kuwa hujawahi kushuhudia barca akichezea kichapo tena kwao! Jiandae kisaikologia! Juventus 3-0 barca!

Mkuu chuki zako dhidi ya Barca zitakusababishia vidonda vya tumbo
 
Haya! Naona wewe unakisikiaga tu kibibi kizee cha Turin!! Chonde Chonde! Barca nini Bwana? Unataka kutuambia kuwa hujawahi kushuhudia barca akichezea kichapo tena kwao! Jiandae kisaikologia! Juventus 3-0 barca!

mkuu sijakataa kwa huyo bi kizee anaweza akafunga goli au hata magoli lakini abadani asirani kombe hatolichukua, ile ni mali ya inayopaswa kwenda catalunya
 
Juve leo bao chache atakazopigwa hazipungui tano, tunatarajia bao ishirini na kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom