Wakuu bila shaka mmejionea kilichotokea jana/leo kwanza niipongeze timu yangu ya Simba kwa mpira wa jana, Simba imepiga mpira mkubwa mno tena kwenye ardhi ya Mwarabu saa saba za usiku.
Note: Tunaposema Mwarabu ndio kama hawa Raja, Wydad, Al ahly, CR Belouzdad, Js Kabylie etc.
Sio Waarabu wa mchongo akina Club Africain, Us Monastir na wengine, tunaongelea giants of Africa. Binafsi matokeo ya jana ni sare ya bao 1-1 hayo mengine mtajua wenyewe na babu yenu, haiwezekani anatuchoma mara ya pili mtawalia.
Niongeze kwa kusema kwamba mechi ya jana imenipa confidence sana kama shabiki katika kuielekea robo fainali ya CAF champions league. Kwa pira tulilopiga jana ni dhahiri tunao uwezo wa ku-battle na magiant wengine waliopo kwenye hatua hii ya robo, na tumeonyesha dhahiri kwamba Horoya hakupigwa 7 kwa bahati mbaya, na pia tumeonyesha dhahiri kuwa hatupo nafasi ya nane kwa ubora Afrika kwa bahati mbaya.
Hivi wachambuzi mnaosema kila siku Simba mbovu huwa mnaangalia Simba ipi, mbona maneno yenu hayaakisi uhalisia? Anyways Simba tuna kitu na mwaka huu kwenye CAF Champion's League tutafikia malengo yetu ambayo ni Nusu Fainali au zaidi inshallah.
NB: Timu yako kama haishiriki CAF Super League basi uzi wangu achana nao.
Nguvu moja [emoji881]