joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 19,513
- 41,719
Kwa picha nilizo ziona kutoka Dodoma Chamwino, kama kawaida yetu mwendo wa hekima na busara,maswala ya kanuni yamewekwa kando. Kesho litajirudia lile lile, kama la Fei likaja kujirudia kwa Dube. Tuna safari ndefu na mpira wetu,kweli soka letu kivyetu vyetu.Sizani kama tunalisaidia soka letu, leo Msemaji wa Mtibwa anakwambia wameshinda ubingwa wa Championship wamepewa kombe, ila hela zao hawajapewa vipi hawa nao?Dabi ya Kariakoo ya June 15 imesogezwa mbele Kwa mara nyingine tena
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeusogeza mbele mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya klabu ya Yanga na klabu ya Simba ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 15, 2025 kuanzia saa 11:00 jioni.
Mchezo huo sasa utafanyika Juni 25, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.
Bodi inazitakia maandalizi mema klabu za Yanga na Simba kuelekea mchezo huo.
View attachment 3367072
Ninavyojua mpira wetu na imani zetu tarehe 24 hamna,walio lalamika kufungiwa huwanja hawata peleka timu kufanya mazoezi kabla ya mechi.