Mechi ya Taifa Stars na Uganda yasimama kwa muda kutokana na taa za uwanjani kupungua mwanga. Taa ziliwaka ikaendelea

Mechi ya Taifa Stars na Uganda yasimama kwa muda kutokana na taa za uwanjani kupungua mwanga. Taa ziliwaka ikaendelea

Ni kama wewe heading umeandika HURKA badala ya HULKA na utataka tukuchukulie poa tu,au unaweza hata kusema "si umeelewa lakini"

😀😀
 
Mchezo wa Tanzania vs Uganda umesimama sababu ikiwa ni baadhi ya Taa kuzima[emoji3064].

Kumbuka apo tuna Onyo kutoka CAF la kurekebisha pitch ya kuchezea ,Nani wa kulaumiwa..?

Ina maana uwanja hauku kaguliwa siku moja kabla..?

Je Mara ya mwisho kubadilisha Taa ilikua lini ..?

[emoji3064]HII AIBU KWA KWELI TENA MBELE YA WAZIRI MKUU...
IMG-20230328-WA0059.jpg
 
Tulizungumza hili jambo tukaonekana wabaya, huyu kipara ni maharage ndani ya wizara.Ukiacha Uganda ambapo nchi nzima inatazama mpira,Dunia nzima inashangaa! Hii ni aibu kubwa sana! Ilipaswa wawajibike kwa kujiuzulu ila huenda wote ni walamba asali hakuna atakayewajibika!
Nchi inaendeshwa na wapiga porojo tu maneno mengi vitendo sufuri
 
Tukienda tu kwa kubembelezana kama ilivyo kwa Waziri wa Nishati! Iko siku tutapata bonge la Aibu zaidi ya hili la umeme kuwa mdogo kwenye uwanja wa Mkapa mechi ya kimataifa ya Tanzania na Uganda!

Halafu sijui ni kwa nini huwa inakuwa hivi!

Kila mtu aliyewahi kulalamikiwa sana na wananchi kwenye tawala hizi, mtu huyo huja kuwa sababu ya serikali kufeli vibaya na kuwa ya hovyo hovyo tu

Nchi nzima kwani imekosa watu makini hadi iwe yuleyule tu aliyefeli hata kabla ya kuanza?

Hivi majuzi kwenye ziara ya Rais kabisa kule Arusha! Umeme ulikatika mbele yake na bado mh Januar Makamba bado aliendelea kuwa waziri

Mfano

Makonda!
Januari watu hawakupendi mama anakubeba kwa mbeleko kwa sababu ya connection ya jk inayofika hadi kwa makamba mzee. Waswahili uongozi hamuwezi mumeweka mbele ubinafsi. Laana ya kumsaliti magufuli haitawaacha milele.
 
Kuna watu kwa kweli hawajipendi walienda kuchezea switch makusudi wameshakamatwa tayari jeshi la
Polisi wanafanya kazi Yao.
Kwamba hii ndio jinsi ya kudanganya umma? Ili iwe nini, kumsafisha mama?

Taa za kumulika pitch, kwanini ziwe na switch nying tofauti tofauti?
 
Wazee kuchomoa Waya,,,wameleta Mazoea yao,,,leo Wakaenda Kuzima Swichii,,###Wameyakanyaga
 
Hamjaelewa

Hizo ni mbinu za kimchezo ili kupiga MILION 10 Mama!

Hiyo ni kete muhimu Sana ya kumtema marope ikitumika vema!
 
Ni aibu iliyoje kwa taifa kutokana na aibu ya taa za uwanja kutoa mwanga hafifu na baadhi kuzima kabisa.

Changamoto za uwanja zimekuwa nyingi mno na sijui ni kwa nini hali inazidi kuwa mbaya.

Kama mwenda zake angekuwepo,leo shoo ambayo angetoa, sijui kama kuna mzembe angeendelea kuwa madarakani leo.

Tumerudi nyuma sana na wahusika hawashtuki.
 
Walamba Ramba Ramba......usirudi na mechi hiairishwe kabisa.

Tukiwaambia jamaa alikuwa anapiga kazi muelewe sasa.
 
Kesho tutasikia Rais amewapongeza kwa kurudisha umeme haraka na mchezo kuendelea.

Nilivyo ona Gerson Msigwa kajiingiza sana kwenye mambo haya ya zawadi za "mama" za kununua magoli nikasema kuna balaa linakuja la aibu ingawa sikudhania itakuwa aibu hii, jamaa ni gundu full muziki.

Simba na Yanga wamkatae huyo
 
Back
Top Bottom