TANZIA Medi wa Ngara Oil afariki Dunia

Jikite kwenye jukwaa la mapenzi
Mnapenda sana hizi taarifa za misiba sijui mnafurahia ama? So boring

Mnaumiza ndugu jamaa na marafiki kwa ushabiki wenu wa kijinga.

Acheni kufurahia vifo vya wenzenu
 
Ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji.Tuko njia moja mkuu.La msingi ni kujiandaa kwani hatujui siku wala saa.
 
Apumzike kwa amani.

Ila kwa vifo hivi Mh. Rais kwa kujua au kutojua kwako unatukwaza sana mheshimiwa.

Kwanini unatufanyia hivi kweri?

Hadi afe nani? Au hadi tufe wangapi?
Kwani Mh Raisi unaemlalamikia ndiyo aliyeumba kifo!?
 
Inakera kinyama, mtu akisikia msiba tu anawahi JF kuanzisha uzi
Si bora huku huko whats up watu wana default msg wanabadili jina tu wameshatuma mtu hata hajapoa wameshatuma. Juzi nilipewa habari ya msiba nikasema saa ngapi amefariki naambiwa sasa hivi, nikasema siwapigii wahusika kuwapa pole mpaka niwasikie wenyewe wametangaza maana msiba kawaida wenye msiba wanatakiwa waseme, wewe unapiga simu poleni kumbe mtu yuko ICU haya mambo nashauri hata kama umesikia lakini subiri wenye msiba wathibitishe.
 
Jf imekuwa ya MATANGAZO YA VIFO.
ipo siku mtu atafiwa na KUKU wake ataleta tanzia humu.tumechoka
Kwani ndugu zao wamewatuma mje mtangaze msiba wao?
Wewe unajuwaje kama wanaoleta hizi taarifa hapa ni ndugu zao wafiwa? Halafu kama hutaki kusoma siuache kwani umelazimishwa we vipi?
 
Jazia Nyama kwenye Uzi wako, alizaliwa wapi, je Mtaji wa kuuza mafuta aliupataje,je baada kifo chake Nani atakua Mrithi wa biashara zake nakadhalika! Sasa wwe unatuambia tu mtu kafa Basi umemaliza!!
 
Waarabu na waarabu koko watakufa sana,tatizo wanapenda sana kukusanyika na hapo ndo wanaambukizana. To be honest nimeona wagonjwa wengi ni wanaume waarabu na waarabu koko.
 
Mnapenda sana hizi taarifa za misiba sijui mnafurahia ama? So boring

Mnaumiza ndugu jamaa na marafiki kwa ushabiki wenu wa kijinga.

Acheni kufurahia vifo vya wenzenu
Unadhani kuficha taarifa kunapunguza ukweli wa vifo? Ushabiki ni upi ambao mleta taarifa ameutonesha? Dhamira ya unafiki na Kiburiii vinawachoma. Just a matter of time, Truth is there to stay!!
 
Wapi nimekutukana nyokolist. Unajiumbua kwa ID nyingi nyingi
Mimi nimeingiaje tena huko?
Nilipoandika "Tafadhali tusitukanane" niliandika kwa kukusudia matusi yanayoingia jukwaani humu.

Sisi wa Ngara au wenye uhusiano na Ngara tunahusika na taarifa hizi.
Marehemu alikuwa ni sehemu yetu.
Tunamshukuru sana mtoa taarifa.

Naamini hakuna anayelazimishwa kusoma asilolitaka.
 
Tatizo mnalazimisha kila kifo kiwe cha corona,mnaumiza ndugu,jamaa na marafiki.
Ni sehemu gani ameonesha sababu ya Corona?
Mnajishuku, ingawa mpo karibu na ukweli!!!
 
Kwahiyo unasubiri Rais akuambie unawe mikono, uvae barakoa, n.k?
Basi sawa
 
Wapi alisema hakuna ugonjwa?

Halafu akisema upo au haupo ndio inaondoa ukweli na uhalisia wa huo ugonjwa? Huko kwenye matangazo daily ndio ugonjwa umeisha kwa matangazo ya Rais?

Chuki ZINGINE zihamishie shambani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…