Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Wewe ndio umechanganya mambo hapa.Mkuu inawezekana una point.. lakini ungeona structure ya huo mtihani ungeelewa andiko la jamaa.. mtihani ni wakisiasa sana..
Maana mtihani una maswali 150 unayafanya kwa masaa 3. Maswali yote ni multiple choice na ni theory tu.
Kijana wa mwaka wa 3 ana mtihani ulio realistic zaidi ya mtihani wa post au pre intern..
Hii mitihani ingekua ya maana kama ingekua theory na practical kama mtihani mingine ya medical school. Lakini huu wa maswali 150 tana theory ni kupotezeana muda na pesa tu.
Pia hela ya registration kupata leseni baada ya kufaulu hio mtihani ni kubwa sana.. imagine mtu huna kazi utoe 300k kwa ajili ya registration na kupata leseni.
Mleta mada ameleta bandiko la kiujumla la kupinga uwepo wa pre& post intern exams kwa sababu eti wahitimu wa udaktari tayari walichafanya mitihani mingi sana na kufaulu wakiwa bado chuoni. Na sisi tumempinga kwa kusema wazi kuwa; kwa mhitimu yoyote wa Udaktari hapaswi kuogopa mtihani na anapaswa mara kwa mara kupimwa upeo wake kwa mitihani kwa lengo la kumkumbusha wajibu wake na kujiridhisha upeo wake kabla ya kutibu watu.
Kuhusu ubora wa hiyo mitihani, hilo sijui, na wala sio hoja ya hapa. Yote kwa yote, kwa kuwa mitihani hiyo inaandaliwa na baraza la madaktari (MCT), chombo chenye jukumu la kusimamia utendaji wa madaktari kila siku basi presumptive tunaweza kusema ni mitihani yenye viwango na kukidhi taaluma ya udaktari hapa Tanzania.