Medical Council of Tanganyika (MCT) lengo lenu ni lipi kwa vijana wetu? Njooni mueleze

Huu mfumo wa kureniew Kwa CPD sijui binafsi siuafiki basi tu. namfikiria jamaa yangu yupo rukwa huko anaendesha bajaji ana miaka miwili saiv kazi hana anakusanya vipi hizo points??? baadhi ya vitu ni vya ajabu sana.

Nawajua wataalamu kibao wa lab ngazi ya degree waliopo mtaani ...hawa hizo CPD watazifanyia wapi pindi walitaka kureniew hizo leseni? Yaani sina kazi ,na hakuna dalili ya kuajiriwa ..halafu hiyo hela kidogo nayopata Kwa kupambana mtaani nikahudhurie training kisa kureniew leseni ....aah wap

ingekua better mfumo huo WA kureniew uanze kumkaba mtu akishaingia kwenye system ....japo shida nyingine huwez mtoa mtu kwenye ajira kisa hajareniew leseni na wataalamu wengi huwa hawareniew humo makazini.
 
Mkuu hao shida yao ni kupata mapato tu.
Ujinga mtupu, tz kila mtu anatafuta pa kupigia ,leo ninao uwezo angalau kumsadia kijana je ni vijana wangapi ni yatima na nyuma ana wadogo zake anawasaidia Hata KWa lile bum ,alafu anaanza angaika na ujinga wa namna hii ,wizi mtupu
 
WEWE una akili pungufu how nizungumzie law school wakati utendaji wake sijui ,nazungumzia nilipobobea ,ACHA kujikuta Bwana, nazungumzia ninapopajua vizuri, na WEWE Kama mada ukifika unapopajua vizuri nitakaa kimiya,
Sasa law school na medicine wapi na wapi japo ipo sehem vyaweza kutana ,kaa Kimia mkuu
 
We umewajuaje ,mbona kiroho nakuona Hata WEWE ulikua kilaza Sana, Acheni mazalau, Mimi nimepitia huko ,Kipindi hicho Amo ndo walikua mabosi wetu wa kutufundisha KAZI , utaniambia nini, WEWE limbukeni ,wafikili ulipo ndani ya medicine wajua KILA kitu ,changia KWa adabu
 
Yani nyumba MOJA KILA mtu na kipande chake ,why afya tuwe na vikundi vingi Kama sio wizi ni nini, binafsi mgonjwa mpaka anatoka hospital huduma yake imechanginwa na watu kibao KWa nini lisiwepo shirikisho moja ,KWANZA WIZARA YA AFYA ,NIWAOMBEN ,TCU NIWAOMBEN MCT ,na vyama vingine vya afya visitake wapandeni vichwani, tz wizi ,ukiritimba, ujinga ujinga tu
 
Jamii forum Kuna watu ,huwa Wanamazalau Sana , nakujiona wao Ndo kila kitu, wanakosea Sana jf ina watu majembe ,na waviwango vya juu Sana na hawanaga makuu ,simple but sure, nawapena wanajf wote mungu akawazidishie wote na imekua KWa leo na KWa Mara ya kwanza
 
Wanapigq hela tuu yaan ni kupiga pesa tuu hakuna kingine!!!
 
Dhumuni kuu ni ukusanyaji pesa. Hata ERB waliambiwa hakuna ruzuku wajibebe!!
 
Umeandika vizuri sana...huyu jamaa wa MCT ana uwezo mdogo sana......
 
Waige kwetu Pharmacy Council, hatubembelezi. Utafauli kwa uwezo. Hawa MCT hata wakipigiwa kelele na Wanasiasa wanafyata.
MCT ilitakiwa iwe na mbinu imara kushinda Pharmacy Council, ila ndio imekuwa kinyume chake. Na tena wanavyolia hivi hii mikakati inaweza kulegezwa
 
MCT ilitakiwa iwe na mbinu imara kushinda Pharmacy Council, ila ndio imekuwa kinyume chake. Na tena wanavyolia hivi hii mikakati inaweza kulegezwa
Sio kulegezewa waje na majibu, haya mavyama yamekaa kiupigaji KWa mlango wa nyuma, hivi huwa yanawakilisha mahesabu yao kwanza KWa CAG ,au ni upigaji tu , leo Ma Dr , wengi wanapiga mzigo sio wa kawaida je wote wanapitia mfumo huu, wa kinyonyaji na wakipuuzi Kama huu ,Kuna arafu kubwa ya kifisadi kwenye mavyama uchwara Kama hivi
 
Laiti MD wangekuwa wana Sup mitihani hiyo kama wale wa Pharmacy Council(Pharmaceutical personnel), hoja ya upigaji na ukusanyaji wa mapato ingekaa vyema sana, maana ungeona wanavyolipishwa kila wanapofanya mtihani.

MD kwenye hii mitihani wanafaulu wote(sijasikia habari za kusup).

Kule Pharmacy Council ufaulu huwa ni chini ya 50% kwa kada zote(Pharmacist, Pharm Tech, Pharm Assistant), halafu kuna masomo 3 ya kufanyia mtihani. Kila somo linalipiwa. Watu husup hadi mara 4 na kila sup wanailipia. Huoni hapa ndipo wanapokusanya mapato? Unaweza kulinganisha na MD wanaofaulu wote, tena somo(mtihani) moja(mmoja)?

Pharmacy Council, pepa zinapigwa mara 3 ndani ya mwaka 1, MCT wanapigisha pepa kwa awamu ngapi kwa mwaka?

Si unaona Pharmacy Council wanavyokusanya mapato?

Suala la mitihani libakie palepale na kuboreshwa zaidi, hapa tuungane kuhoji upigaji kama dalili zipo, ingawa upigaji lazima uwepo.

Wenzetu(mataifa mengine) wamepiga hatua kwa sababu mifumo yao ya kuzalisha wanataalum ipo madhubuti, sisi huku wakitaka kuimarisha mifumo tunaona ni nongwa, sijui ni lini tutafika walipofika wenzetu.
 
Kweli hii ni ajabu, inamaana vjana wetu sikuhizi hawasimamiwi vizuri?!!

Enzi zetu Kama unasua sua usingeweza toboa.

My take,

Basi TCU wameshindwa kusimamia vyuo na huenda mifumo ya rushwa inatukwamisha.

Na ni imani yangu kua hiyo mitihani haisaidii chochote Kama mtoto hakusimamiwa vema na mwalimu wake hasa kwenye basic science.

Ushauri,

Nguvu ielekezwe kwenye kuwapa motisha wakufunzi wawasimamie vema watoto wetu, huko ndo pakutatulia tatizo, haya ni masomo ya science ambayo misingi yake hujengwa kwa matofali ya Theories,principles na concepts.

Mengine hayo sioni faida hata.
Labda hiyo ya uniformity na matakwa ya nchi nyingine.
 
Kwani Kada zingine mbona hawapigi kelele..??? Mitihani yenyewe wote wanaofanya wanambiwa wamefaulu...
Wengine wana post intern sio pre-intern..

Hii pre-intern ni kuleta ukiritimba mwingine umezaliwa..Though ni vizuri kujiridhisha kama watu wana skills kiasi kuhusu fani hiyo kabla ya mafunzo kwa vitendo.
 
Wengine wana post intern sio pre-intern..

Hii pre-intern ni kuleta ukiritimba usiokuwa na kichwa wala miguu..h
Kwa kumaanisha nini??? Pre intern kwa MD inakuwaje????
 
Wanafanya mtihani wa MCT kabla ya kwenda intern,usipofaulu unasugua benchi kwanza..
Eeehe kumekuchaaa... Mbona majanga kwani hii imepitishwa????[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…