Sina mengi ,kwanza niwasalimu, wanajf popote mlipo, KILA mmoja KWa imani yake.
Pili niende kwenye mada moja kwa moja
Tanzania tunavyama vingi Kama sio utitiri vinanvyo simamia taaluma flani flani ,nk, ila leo nimejikite KWa Hawa MEDICAL COUNCIL OF TANGANYIKA(MCT)
Binafsi Kama baba na mlezi ambae nimepitia Iyo taaluma na kusonga mbele, ningependa ( MCT) mnipe majibu ,
Taaluma manayosimamia najua mnaijua vizuri,ndo maana mpo apo,mnajua pamoja na intern inachukua miaka sita shule kumalizika ,inayojumlisha mafunzo ya vitendo na theory ilo Sina shaka kabisa kwamba hamjui
Enzi zetu hatukua na post intern exam, japo ni hivi karibuni mlianzisha ,binafsi Sina shida na Hili ,WENDA lego lenu nikumpima uyu Dr nini amejifunza zaidi, japo sion logic yoyote ,kwani alipo kule si ana waangalizi wake kwenye hospital aliyopo, Sasa unampa mtiani umemfundisha nini badala ya mtiani kupewa pale Hospital alipofanyia intern,
NAOMBA JIBUN ILI PIA
Hamjatosheka Sasa nasikia mmekuja na kitu kinaitwa pre intern Exam , kwamba vijana wamemaliza masomo ya miaka mitano, walim wao ,vyuo vimejiridhisha kwamba wako vizuri na wamefaulu nyie ndo ,mwajifanya kutoamini vyuo vyao, walim wao ,kwamba mnatoa mtiani wa kuwapima tena Ili waende intern, ebo nyie vipi ,kuzalisha ukiritimba mpaka kwenye maisha ya watu,
Nyie mlioko hapo na kugawana posho mlifanyiwa hivi?
1.Sasa toeni majibu Iyo pre intern exam KWa awa vijana impact yake ni ipi, ?
2.Alafu naomba mtueleze KWa uwazi majukum yunu yawe wazi msije kua mnaingilia mpaka KAZI za TCU, maana nimeona kijana wangu KILA kukicha anaomba pesa ,nikiuliza ya nini naenda kuverify vyet vya form 4, 6, Ili nitume maombi MCT Ili kufanya mtiani
Swali
KWa Iyo nyie mmejigeuza TCU iliyomdahili uyu mwanafunzi kwenye chuo chake, akapata na mkopo bord, asilimia 100, leo wewe unataka vyeti vya nyuma Ili iweje?
2. Awa vijana mnaowachelewesha KWa ukiritimba tu ,badala waende intern wamalize wapate pa kujiegesha, Ili nakuanza angalau rejesha pesa walizokopa ,Ili iwasaidie vijana wengine ,je mnaona mnawatendea haki watanzania ,na Kama sivyo KWa nini muendelee kalia viti hivyo
Mwisho naomba MCT mlete maji live , vinginevyo nitajua Kuna kitu nyuma ya pazia ambacho mnapitia mlango wa nyuma kukifanikisha KWa malengo YENU