Laiti MD wangekuwa wana Sup mitihani hiyo kama wale wa Pharmacy Council(Pharmaceutical personnel), hoja ya upigaji na ukusanyaji wa mapato ingekaa vyema sana, maana ungeona wanavyolipishwa kila wanapofanya mtihani.
MD kwenye hii mitihani wanafaulu wote(sijasikia habari za kusup).
Kule Pharmacy Council ufaulu huwa ni chini ya 50% kwa kada zote(Pharmacist, Pharm Tech, Pharm Assistant), halafu kuna masomo 3 ya kufanyia mtihani. Kila somo linalipiwa. Watu husup hadi mara 4 na kila sup wanailipia. Huoni hapa ndipo wanapokusanya mapato? Unaweza kulinganisha na MD wanaofaulu wote, tena somo(mtihani) moja(mmoja)?
Pharmacy Council, pepa zinapigwa mara 3 ndani ya mwaka 1, MCT wanapigisha pepa kwa awamu ngapi kwa mwaka?
Si unaona Pharmacy Council wanavyokusanya mapato?
Suala la mitihani libakie palepale na kuboreshwa zaidi, hapa tuungane kuhoji upigaji kama dalili zipo, ingawa upigaji lazima uwepo.
Wenzetu(mataifa mengine) wamepiga hatua kwa sababu mifumo yao ya kuzalisha wanataalum ipo madhubuti, sisi huku wakitaka kuimarisha mifumo tunaona ni nongwa, sijui ni lini tutafika walipofika wenzetu.