Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Masikini Hapendi Watoto
Code:
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mwakani Tarehe Kama Mtafurahi Ninyi 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Maneno Matamu Sitayasema Mimi Kwenye Serikali Yangu. Mimi Ni Makavu Tu
JPM

20210501_204107.jpg
 
Kazi ya Urais ni ngumu Sana.

Mama anatakiwa ajipange.

Naona mama ameanza kutafuta huruma kwa watu.


Tusiruhusu mama adeke, kipindi Cha majonzi kimeisha sasa achape Kazi bila woga Wala kinyonge.

Wananchi tunamtegemea.

Ila kitendo cha leo kinaonesha nchi na serikali imeanza kuwa dhaifu Sana na mda so mrefu atashindwa kuongoza.

Mama chukua hatua mapema kabla kivuli cha Magufuli hakijawaisha wanaokuzunguka na kuacha kabisa kufanya kazi.
Angalia fujo za barabarani ndipo utajua kuwa yajayo yatamfanya JPM kuwa rais bora
 
Huenda ilikuwa ipande, lakini "raisi wa jamuhuri ya twita" akaharibu mambo!
 
Kuwa na akili basi, bajeti ilishatengenezwa kukiwa hakuna fungu la nyongeza, sasa unataka yeye adange aongeze mshahara?


We ndo huna huna akili
Wapi umeona nalalamikia mshahara?
Mimi nazungumzia watu kupewa expectations ingine na kupewa tamko lingine....

Soma vizuri uelewe..
 
Kupandishwa mshahara ni kuongezeka kwa take home pay ambayo inaweza kuongezwa kwa kupunguziwa kodi. Je wafanyakazi hawajapunguziwa kodi Ingawa kidogo?

Hata wakaopandishwa vyeo wataongezewa mishahara..Kwa ujumla speech ilikuwa nzuri hasa aliporekebisha wategemezi hadi umri wa miaka 21..

Mimi nachoshangaa why yeye na waziri wake Mhagama kama walikuwa hawana coordination
 
Sijamwelewa mtoa mada, Ina maana hotuba ya rais ifahamike kwa waandamizi wake wote? Sasa kama wafanyakazi wangefahamu mapema hakuna nyongeza ya mishahara umuhimu wa hotuba ya rais ingekuwa Nini?

CEO huwa anaongea public kitu ambacho kila msaidizi wake anakijua
 
Kwa uelewa wangu hotuba ya Rais inapaswa kutoa majibu ya hotuba nyingine zote kwa halfa husika kutokana na key issues ndio maana anapewa za wengine kabla azione ajue wanataka nini.

Sasa kusema kwamba hakuna coordination sio sawa, maana hao wengine wameomba nyongeza akawajibu kuwa siwezi mpaka wakati mwingine.

Kwa mantiki hiyo sioni sababu ya wasaidizi wake kuwa na majibu ya maombi yao kabla ya tukio.
 
Hata wakaopandishwa vyeo wataongezewa mishahara..Kwa ujumla speech ilikuwa nzuri hasa aliporekebisha wategemezi hadi umri wa miaka 21..

Mimi nachoshangaa why yeye na waziri wake Mhagama kama walikuwa hawana coordination

Mimi nadhani Waziri Mhagama ndio hakuelewa kuwa kupunguzwa kwa kodi ni njia mojawapo ya kuongeza mshahara. Alitakiwa alifafanue hilo kwa Viongozi wa wafanya kazi mapema kwani wao wamezoea kuambiwa mshahara umeongezeka kwa kiwango fulani!! Jenista ndio kalikoroga hapo, upeo wa mawaziri wetu na watendaji wengi ni mndogo hivyo kuelewa concept ya coordination itachukua muda!! Wamezoea kila mtu na MUHOGO wake!
 
Back
Top Bottom