Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Ulitegemea huyu angeweza kumfunika Magu?! Magu is next to Nyerere. Hata kwa Nyerere anachopungukiwa ni ile brilliance ya Nyerere. Otherwise he is far ahead of them all.
Ulikuwepo katika utawala wa Nyerere? Kama ni bora sana kwanini walitaka kumpindua?
 
Matamko yalikua ya kutosha na wafanyakazi wamerishika nayo.
Makato ya kodi yatakua 8%
Umri wa wategemezi umeongezwa mpaka mika 21
Mishahara itapanda mwakani (angalau tumaini lipo)
Retention fee ya HESLB (6%) imeondolewa
Na la muhimu zaidi masikini hampendi mwana.
 
Subiri kidogo tu tutaelewana! JPM alikuwa ni hero kubali Katapa huo ndiyo ukweli unaowauma
Hero kwako, rais mvunja katiba kiasi kile kumsifia yataka moyo.Kwangu ni kukosa uzalendo kwa taifa
 
Pia mama kapandisha vyeo wafanyakazi 85000-91000
 
Kuna kizazi cha watanzania kitakuja na maamuzi ya kumpa hayati heshima ya utakatifu, i mean st. Magufuli. Itakuwa miaka kadhaa mbele na si kizazi hiki cha mafisadi na wala rushwa
Haahaa, endelea kuota.Mama kwangu ni hero na shujaaa.Mwendazake alikuwa mtawala na sio kiongozi..
 
Soon mtakiri wenyewe ni swala la muda tu
...kwangu never ever, japo yapo Mambo mazuri alifanya Kama mwanadamu, kile kitendo Cha kuvunja katiba na kiapo chake kilifuta Nia yake yote njema aliyokuwa nayo.Kiongozi yeyote mvunja katiba hafai kamwe.Ni usaliti mkubwa Sana kwa watu wake
 
Sir Magufuli the hero, ndiye alikuwa rais mwenye maono, mwelekeo sahihi na misimamo. Kwake ilikuwa rangi either ni nyeusi au nyeupe. Hakukuwa na mapichapicha kama haya.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
...haahaa, kwangu alikuwa rais mbabe na mvunja katiba ya nchi yake...
 
Kama Samia alikuwa anajua haiwezekani kupandisha mishahara leo alipaswa kuwaweka wasaidizi wake mapema ili waweze 'kuwaandaa watu kisaikolojia'mapema...
Binafsi nilishajua kwamba hilo suala halipo! Sio kwamba mimi ni Insider bali huwa siishi kwa mazoea!!!

Unajua zamani wafanyakazi walizoeshwa kutangaziwa nyongeza Siku ya Mei Mosi! Mwamba Che Ben, akaona hii kitu ya kuwa-tune wafanyakazi kwamba kila Mei Mosi wanatangaziwa kupanda mshahara ni jambo lisilo na afya!!

Akaachana na huo upuuzi!!

Sikumbuki JK kuwahi kutangaza kupanda kwa mshahara wakati wa Sherehe za Mei Mosi... labda nimepitiwa!! Sana sana watu walikuwa wanashtukia tu kuna elf 9500 imeongezeka!!!

Mwenda zake angekuwa ni mtu wa kupandisha mishahara, labda huyu ndo angeturudisha zama za Mwinyi kwa sababu Mwamba alikuwa anapenda sana kucheza na jukwaa!!

Anyway, hawa watu wa serikalini siku hizi wananitia uvivu sana kuwafuatilia kwa sababu, kwa kawaida huwa SIPENDI WATU WAONGO!

Sasa kama Jenister aliwaaminisha watu kwamba kutakuwa na ongezeko la mshahara basi atakuwa ni mpuuzi kweli kweli!!! Yeye amehudumu kwenye serikali iliyopita! Aliona lini na wapi serikali aliyokuwa anahudumu ikitangaza kupanda mshahara kwenye Sherehe za Mei Mosi!!!
 
Ieleweke tu kwamba hoja ya mtoa mada sio mishahara kupanda hapana.

Mtoa mada hoja yake ni kwamba iweje viongozi wa serikali wanapishana kauli?.
Watendaji wa chini walipo simama kauli zao zilionyesha moja kwa moja kwamba ile kiu ya siku nyingi ya wafanya kazi ya kutaka ongezeko la mishahara leo inakwenda kutimia. Kitu kilichopelekea asilimia kubwa ya wafanya kazi kuwa na matarajio makubwa kwa Rais kwamba leo ataongeza mishahara. Ndio maana Rais Alivyo Simama Imemlazimu Atafute Maneno mazuri ama azunguke Sana Wakati Anafikisha Taarifa Ya kutokuwepo kwa nyongeza ya mishahara maana watendaji wake walishamuweka kwenye mtego kati yake na wafanya kazi.
Baada ya Rais kutoa kauli ya kutopandisha mishara wafanya kazi wengi walionyesha kunyong'onyea ghafla maana ni kitu ambacho hawakutegemea kutokana na kauli za Viongozi wa chini Walio tangulia kusimama kabla ya Rais.

HII NDIO POINT YA MTOA MADA.
 
Lakini Wafanyakazi hata kama tunanjaa ya muda mrefu ya kuongezewa mishahara tuwe na subira. Mama ameingia juzi, corona imepiga uchumi tumwache mama ajipange. Kifupi tumpe muda.
 
Sasa page ikipungua kutoka 9 Hadi 8 net pay inaongezeka? Au tatizo hesabu
 
Hii mitego inategwa kweli kweli.
Waziri Jenista kaleta uchonganishi mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…