Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Kama mishahara ingekuwa inapandishwa leo hii dalili zingeanza kuonekana siku Mpango alipoiweka hadharani hotuba ya bajeti.

Hakufanya hivyo kwa hiyo ilitegemewa kabisa kuwa ongezeko la mshahara lisingeweza kutangazwa.

Alichokifanya Rais ni kuwajenga kisaikolojia wafanyakazi kwa kuwaambia kuwa mwakani litakuwepo ongezeko la mshahara.

Ukishakuwa mwanasiasa ni lazima ujue namna ya kutumia kinywa chako vizuri ili maneno yako yawe ni makali lakini yasiyomuumiza mtu kwa muda ule anapokusikiliza. Rais amejifunza namna ya kuitumia vyema hii silaha kutoka kwa Mzee Jakaya Kikwete.
 
Halafu ifike point tuache kuwasema swma viongozi vibaya nao ni binadamu...nyie ndo mnafanya viongozi wanabadilika na kuanza kutufanyia maovu kuweni na shukran na jema pia.

#chawa_wa_samia_suluhu_hassan
 
Hotuba ya My. Rais siyo public document. Ni siri. Na Rais wetu Samia ni mtu mzuri sana kuhakikisha hakuna siri Inatoka. Pili kwa muda wake mfupi na changamoto zilizopo si rahisi kupandisha mshahara. Kwanza ngoja apandishe vyeo/madarasa maana madarasa mapya pia nayo ni ongezeko la mshahara. Hivyo pia fungu la kuwapandishia mshahara litengwe. Inaonekana halikutengwa maana budget huwa inaandaliwa mapema.
Kwa msingi hiyo tumpe muda. Mwakani akikausha tena ndipo lawana kalikali zimuandame.
Kwa leo yapo machache amefanya ambayo itakuwa ni ahueni kidogo kwa mtumishi wa umma.
 
Kama wangejua kuwa mishahara haipandwishi wasingejitokeza wafanya kazi wangebaki makwao.

Hata hivyo nimefurahi wacha hiyo hela ya nyongeza ikaajiri vijana wanasota mitaani.
 
Kuna kitu hapa nimekichunguza nikahisi, naona Rais na serikali yake kwa namna fulani kama wanataka kuzima tetesi zizazozagaa kwenye mitandao halafu baadae huwa kweli, ni kama wanajaribu kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao (siri).

Sasa nahisi wameona wasome upepo kwenye mitandao wakiona watu wanaaminishwa jambo fulani (baada ya taarifa kuvuja) wao waje tofauti ili kuwapunguzia wenye ushawishi mitandaoni (twitter in particular) waonekane waropokaji na wazandiki.

Japo inawezekana kweli mpango ulikuwa ni kuongeza mishahara ndio maana mpaka kina Mhagama walikuwa wanajua hilo, inawezekana mchezo umebadilishwa ghafla hata hao kina Mhagama hawakuwa na habari.
Mkuu nimekuelewa sana[emoji120],
 
soon very soon

mliyempa majina ya ajabu ajabu mtamkumbuka sana
Akumbukwe kwa lipi ndugu?
Utekaji?
Kupoteza watu?
Kuleta wasiojulikana?
Kuongeza mishahara Mara dufu?
Au kwa lipi ndugu?
Kwa kujenga mabarabara?madaraja?
Raisi yupi aliepita hakujenga?
Au wewe nitajie rais yupi hakuongeza mishahara?maana marais wote waliopita walishaongeza.Kasoro Samia tu.
 
Mapema Sana wakati anaapisha wateule wake wa Mwanzo Rais Samia alisema kuna tatizo kubwa la Coordinations serikalini...

Leo nimeona hili tatizo kati yake Rais na waziri wake Jennista Mhagama...
Na lack of coordination Kwa ujumla kutoka IKulu kwenda chini Kwa watu Wengine ..

Kama Samia alikuwa anajua haiwezekani kupandisha mishahara leo alipaswa kuwaweka wasaidizi wake mapema ili waweze 'kuwaandaa watu kisaikolojia'mapema...
Ajabu leo wafanyakazi wameaminishwa kuna 'tamko'linakuja na hata waziri Jenista Mhagama alishadadia kabisa kuwa Leo kuna 'tamko'..

Hotuba za vyama vya wafanyakazi naamini IKulu ilizipata mapema na hata arrangements za leo walishirikiana kati ya serikali na Viongozi wa wafanyakazi..
Serikali ingeweza kabisa kuwaeleza mapema kuwa mishahara mwaka huu ni ngumu lakini mwakani itawezekana..

Hii ingepunguza 'expectation kubwa 'iliyokuwepo leo..na hali ya 'dissapointment' baada ya hotuba...

Nimejiuliza je Jesnista Mhagama alikuwa hajui Rais hatapandisha mishahara leo?
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi?..

Serikali ina vyombo vyake vya Ku leak taarifa kusudi..ili kupima upepo au kuwaandaa watu kisaikolojia...Leo mbona
Imekuwa tofauti?
Kama vile aliekuwa anajua kuwa mishahara haipandi Leo ni Samia peke yake...wakati kila mtu akiwemo waziri Jenista Mhagama walikuwa wana expect mishahara kupanda leo .tatizo lilikuwa wapi??

Samia ameanza kuwa 'anaogopwa'?

Kuna ukuta Kati yake na wasaidizi wake?

Kingine ilikuwaje Rais aseme hata yeye anakatwa kodi wakati haipo hivyo?
Mawaziri ,wabunge ,Ma Dc ma RC wameanza kukatwa kodi??..

Mbona kama Rais kaanza kuwa 'mkiwa'mapema? Kama wanaotakiwa kumsaidia hawamsaidii why asiwafukuze haraka?..
Fuatilia vema matamko ya Jenista Mhagama hata kabla ya hii mei mosi iliyopita jana... anzia bungeni wakati hususan bunge lililopita kisha matamko yake mengine utapata majibu wizara hiyo kwanini ina ombwe... labda yupo pale kwa kazi maalum... ajira zinazidi kudidimia wawekezaji wakizidi kuchanja mbuga mpaka imebidi apunguziwe huo mzigo kwa kuteuliwa ndugu Mwambe...
 
Kuna kizazi cha watanzania kitakuja na maamuzi ya kumpa hayati heshima ya utakatifu, i mean st. Magufuli. Itakuwa miaka kadhaa mbele na si kizazi hiki cha mafisadi na wala rushwa
kiongozi was malaika 😀😀😀😀😀
 
Ulitegemea huyu angeweza kumfunika Magu?! Magu is next to Nyerere. Hata kwa Nyerere anachopungukiwa ni ile brilliance ya Nyerere. Otherwise he is far ahead of them all.
huo mzoga wenu hakuna wa kumfikia kwa kuua watu na kuua demokrasia. Matatizo yote tunayoyapata Leo yameletwa na yeye. Mbona kabla yake mambo ya maslahi ya wafanyakazi yalikuwa yanakwenda vizuri tu.
 
huo mzoga wenu hakuna wa kumfikia kwa kuua watu na kuua demokrasia. Matatizo yote tunayoyapata Leo yameletwa na yeye. Mbona kabla yake mambo ya maslahi ya wafanyakazi yalikuwa yanakwenda vizuri tu.
NWOR
 
Back
Top Bottom