FATHER OF HISTORY
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 915
- 638
Fuatilia kinachojiri kwenye Maadhimisho ya siku ya Mei Mosi Kitaifa, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, leo Mei 1, 2024
Maadhimisho haya yamehudhuriwa na Makamu wa Rais, Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Tulia Ackson, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
KATIBU MKUU TUCTA, HERI MKUNDAAkizungumza kwenye Sherehe hizo, Katibu Mkuu TUCTA Heri Mkunda amesema maboresho ya mishahara iliyofanyika bado haijakidhi mahitaji ya wafanyakazi, hivyo vinapaswa kuboresha kwani gharama za maisha zimepanda sana.
View attachment 2978185
Amesema wanatambua uwepo wa nyongeza ya 23.3% ya kima cha chini cha mshahara iliyofanyika, lakini inafaa ongezeko hili lizingatie pia wafanyakazi wengine.
Aidha, wafanyakazi wanaolipwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri wanalalamika kutokulipwa maslahi yao kwa wakati kwani uwezo wa halmashauri unatofautiana. TUCTA inapendekeza wafanyakazi wote wa halmashauri kulipwa kutoka Serikali kuu ili kuondoa ubaguzi.
Kuhusu kikokotoo, wafanyakazi hawaridhishwi na namna kinavyofanyika na kimeleta malalamiko mingi. TUCTA inashauri kanuni za ukokotoaji mafao ziboreshwe ili kuleta manufaa kwa wafanyakazi.
Mambo mengine aliyozungumza ni kuongezewa likio ya miezi 3 kwa wanawake waliojifungua watoto njiti pamoja na kupitishwa kwa kitita kipya cha bima ya NHIF bila kushirikisha wafanyakazi kupitia vyama vyao hivyo kuzua taharuki. TUCTA inapendekeza wafanyakazi washirikishwe kwenye maboresho haya ya kitita.
Kikokotoo ni haramu, Wizi na uonevu, Nimestaafu Nina miaka 60, Halafu makadirio ya kuishi ni miaka 72, Halafu mtu anakwambia utapewa kidogo kidogo, hivi hiyo ni akili kweli? Hiyo Hela nitumie nikiwa kaburini? Imebaki miaka 12, Sasa kidogo kidogo hiyo sijui iweje? Huu ni unyonyaji, uonevu, ukiukwaji wa haki ONDOA KIKOKOTOO