Mei Mosi: Dkt. Mpango asema Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake

Mei Mosi: Dkt. Mpango asema Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake

Watumishi acheni mbwembwe.!! 😁
Screenshot_20240501-103742~2.png
 
Wekeni na mabango yaliyopo huko
 
Mpiga mwingi kaingia mitini ujue hakuna kitu hapo hadi mwenyewe anaona aibu kusimama mbele za watu.

Wese mkoa kwa sasa ni 3500/lita na hakuna hata mpango wakayaondoa hayo makodi.
 
Mpiga mwingi kaingia mitini ujue hakuna kitu hapo hadi mwenyewe anaona aibu kusimama mbele za watu.

Wese mkoa kwa sasa ni 3500/lita na hakuna hata mpango wakayaondoa hayo makodi.
😀😂
 
Huyu Askofu anachekesha sana, etu tupate mvua za kawaida inamaa hajui kwamba mvua ndio inapotea.
 
Nimechoka kuhudhuria haya maadhimisho yenye kupambwa kwa lugha nzuri na ahadi zisizotekelezeka.. Basi hata hili la kutuandalia tustaafu vizuri kikokotoo sio rafiki kabisa ni cha kuhujumu maslahi ya mfanyakazi
 
Mtoto wangu wa darasa la Saba nimemwambia usiende shuleni Leo,baadhi ya wilaya za Tanzania zimewaambia walimu waendelee kufundisha siku Yao ya wafanyakazi
Hahahaha walimu nao kuchukulia kazi yao kama wito ndiyo maana maslahi yao hucheleweshwa, watabaki vivyo hivyo
 
Najaribu kuwaza kama hii siku inaadhimishwa ipasavyo kitatua changamoto za wananchi wanaoitumikia hii nchi maana watoa mada naona wamejisahau wanawasilisha vitu ambavyo havihusiani
#makondaspeech
 
CHATANDA AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI SHEREHE YA MEI MOSI

📍 Arusha
📅 30/4/2024

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) Amewasili Jijini Arusha Usiku wa Aprili, 30, 2024 kuhudhuria maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yanayotarajia kufanyika Jumatano ya Mei Mosi, 2024 kwenye Viwanja vya Michezo vya Sheikh Amri Abeid.

CHATANDA amepokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdine Babu Pamoja na Viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha na Viongozi wa Chama Wilaya na Serikali.

Mgeni Rasmi wa Sherehe ya Mei Mosi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

IMG-20240501-WA0027.jpg
 
SALAMU ZA MEI MOSI

Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) anawatakia wafanyakazi wote Heri Ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Nyongeza ya Mshahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha.
 

Attachments

  • IMG-20240501-WA0015.jpg
    IMG-20240501-WA0015.jpg
    142.4 KB · Views: 4
  • IMG-20240501-WA0012.jpg
    IMG-20240501-WA0012.jpg
    72.9 KB · Views: 4
Hakuna anayeweza kuzuwia mvua, Mungu ndiye muweza, huyu katibu wa TUCTA kachemka, eti anasema alipata maelekezo toka kwa waziri mkuu wakawaone wazee jadi ili wazue mvua isinyeshe Arusha leo! Ni ajabu msomi wa hadhi ile anaamini ushikina na ulozi karne hii. Kutokunyesha kwa mvua leo ni kutokana na msimu na majira yake na wala mvua haijatii wazee hao ikaacha kunyesha. Huyu msomi ni jamii ya wasomi wapuuzi
 
Back
Top Bottom