Jiwe ndio kiboko ya kila mpuuzi nchi hii.
Enzi hizo mwanaume akiongea kauli ni moja tu na mnaufyata.
Sasa hivi mnaleta unafki wa kupiga kelele mngeongea mbele ya kidume tuone kama mnayaweza.
Mafisadi na vibaraka walikimbia nchi.
Wafanyakazi wazembe na wezi waliichukia serikali maana waliishi kwa halali yao ya mshahara na posho wanayostahili.
Kile kidume ni noma ndio maana wabaya wake bado wanateswa na jinamizi lake wakilala jiwe wakiamka jiwe.
Wananchi wa kawaida wanalia sana kupoteza lile dume la mbegu sababu alisimama nao pamoja na unyonge wao. Aliwapa uhuru wa kweli mwenye biashara alifanya na hakusumbuliwa, aliwapelekea umeme, zahanati, maji na barabara nzuri alihakikisha kinachopatikana kinaenda kuwafaidisha watanzania walio wengi haswa maskini pangu pakavu na ndio maana watampenda daima.
Maofisini huko alipanyoosha at least mwananchi mnyonge alisikilizwa na mtumishi wa serikali tena bila connection wala kutoa rushwa tofauti na tawala zingine.
RIP Chuma aka Jiwe.