Mkuu, swala la kuongeza mishahara sio jepesi kama watu wanavyofikiri lina impact kubwa sana kwenye uchumi na sio kila nchi huwa inaongeza mishahara mara kwa mara.
Tatizo la jamii yetu sio kila mtu ni mwajiriwa na anafahamu ongezeko la mshahara ni kiasi gani, mfanyabiashara ambaye hajawahi ajiriwa akisikia tu tangazo kuwa mshahara umeongezeka basi naye atapandisha bei ya bidhaa na huduma, hajui kwamba mshahara umeongezeka kiasi gani, mradi kasikia tu umeongezeka naye atapandisha bei.
Sasa hii inamadhara kwani kipato hicho hakijaongezeka kwa watu wote bali kwa watu wachache tu, hii itaathiri mno wale ambao hawana ajira ambao ni wengi,
Ongezeko la mishahara pia inamaana kwamba tupunguze kufanya baadhi ya mambo tuliyokua tunayafanya ili fedha ziende huko
Kupanga ni kuchagua, tuamue kulipana mahela tu tusifanye lolote au tubebane hivyo hivyo kwa manufaa ya wote.
Rais ataamua.