Kutoka jijini Mwanza tunawaletea taarifa za moja kwa moja, maadhimisho ya sherehe ya siku ya wafanyakazi duniani,ambayo kitaifa yanafanyika hapa.
Mgeni rasmi anatarajiwa kua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan, ambapo atapokea maandamano ya wafanyakazi mbalimbali Tanzania.
View attachment 1769649
Hali ya hewa ni tulivu kabisa,uwanja umepambwa vyema,barabara za jiji zimesafishwa safi huku zikichagizwa na mabango yenye ujumbe wa hapa na pale.
Wananchi wameanza kumiminika viwanjani hapa.
Karibuni.....
============
Updates.
Tayari uwanjabwa ccm kirumba umeanza kufurika huku ukipendezeshwa na sare mbalimbali za tishirts na kofia za vyama vya wafanyakazi wa sekta binafsi,serikali kuu,mashirika ya umma,serikal za mitaa,na chama cha walimu,nyuso za wafanyakazi zinaonyesha tabasamu lililojaa matumaini tofauti na mei mosi za miaka 5 iliyopita.
Viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya wafanyakazi wameanza kuwasili uwanjani.
Namuona Makamu wa Rais,Dr.Mpango,Waziri Mkuu Majaliwa,Katibu Mkuu Kiongozi,Spika wa bunge na makamu wake.
View attachment 1769738
===========
Updates
Tayari msafara wa Rais Mama Samia umewasili uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa shughuli za Mei Mosi kuanza rasmi,shangwe na nderemo zinashamiri uwanjani hapa wananchi wakimshangilia Rais wetu.
View attachment 1769780
======
Maandamano yanaanza baada ya Rais Samia kuwasili jukwaani,takribani vyama 17 vya wafanyakazi vitashiriki maandamano haya.
View attachment 1769848
=========
Updates