KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Pole sana mkuu, lakini maumivu ni yetu sote.
Hebu ngoja nikusononeshe na mifano mingi zaidi ya hiyo uliyoitaja hapo.
Tanzania kuna jua karibu kila siku, mwaka mzima. Kuna sehemu zina upepo wa kutosha sana kuzalisha umeme. Sasa hivi tunao viongozi wanao kesha wakitafuta namna ya kuwaleta wawekezaji hapa, waje watumie jua letu, upepo wetu wazalishe umeme ili watuuzie kwa bei mbaya, na wala viongozi wetu hawaoni uchungu wowote hapo.
Tunayo ardhi nzuri kabisa ya kutuwezesha kuzalisha mazao ya kutupatia mafuta ya kula ya kutosha kwa matumizi yetu na hata kuwauzia wengine nchi za nje. Wananchi wetu, wakulima wanakosa msaada wa serikali yao ili wazalishe mazao haya kwa wingi, lakini viongozi wetu wanajuwa jambo moja tu, la WAWEKEZAJI toka nje!
Huku ni kuwa na kilema cha akili, sijui kilema hiki kitarekebishwa vipi tuanze kujuwa namna ya kutumia raslimali zetu kutunufaisha sisi wenyewe.