Frateri Mtanzania aliyekuwa ametekwa nchini Nigeria, Merikiori Mahinini pamoja na mwenzake raia wa Mali, Padre Paul Sanogo wameachiwa huru usiku wa kuamkia leo Alhamis Agosti 24, 2023, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dk Benson Bana amethibitisha.
Mtanzania huyo ambaye pia ni frateri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers) mzaliwa wa Parokia ya Kabanga, Jimbo la Kigoma, alitekwa nyara na watu wasiojulikana Agosti 4 mwaka huu katika jimbo la Minna huko Nigeria akiwa na mwenzake raia wa Burkina Faso.
Pia, soma:
- Mtanzania, Melchior Dominic Mahinini anayesomea ukasisi nchini Nigeria atekwa na waasi