Hicho kituo kiko wapi na kinafikiwa vipi?Mkulima wa Tanzania sasa hivi ana kituo cha kisasa cha huduma kwa mtej (,Customer care).
Bashe kwa mara ya kwanza Tanzania, anaifanya Wizara ya kilimo kuwa ni watoa huduma wa kisasa kwa wakulima. Jionee:
Mengine tutaendelea kuwaletea.
Hongera Bashe, Hongera Rais Samia.
Nyie ndo wale Pinga Pinga wa bawacha?Kituo cha huduma kwa wateja kinamsaidia nini mkulima anaetegemea mvua na mbolea isiyo na bei ya kueleweka?
Kituo cha huduma kwa wateja kina msaada gani kama mkulima analima kisha anapangiwa bei ya kuuza ama anazuiliwa asiuze mazao yake nje ya nchi?
Ama mkulima anakua anapiga simu anauliza kama shamba lake limejaa magugu, je ayapalilie ama anachome anapewa majibu wa desk officer farmers wa ofisi?
Mkuu inaudhi sana. Mijitu inavimbiwa tu Chipsi na Dona mjini hawajui hata Kilimo chake. Yaweza kuwa mimi siyo Farmer lakini Mkulima wa kati, hizi ngonjera za akina Bashe labda ni kwa ajili ya Big Farmers siyo Peasants waliojaa kila kona ya Tanzania.Wakulima tuliopo kwenye kilimo tumenyamaza tu maana yaliyopo hayatufurahishi, ila nyie wadananda mnajifanya yamkulima mnayajuwa.
Mtu hujawahi hata kulima, hujuwi chochote kuhusu kulima ila na wew unazungumzia kilimo. Customer care itanisaidia nin kama nalima mazao ya biashara na bei inakuwa iko chini, sanaa sanaa tu kila mwaka.
Kitu gani kinapendeza? Nchi ina wajinga sanaInapendeza na ahsante kwa taarifa...
Huu uzi siyo wa kuchangiwa, elewa namna ya nyuzi zilizopo, sasa hapa mtu atabisha nini, na kila kitu kipo wazi? Huu uzi umelenga kuelemisha watu. Unabaki hapa kuwa "reference". Tukibishana huko, nakuleta hapa ujionee au nakuvutia post nakubandikia ulipo.Uzi umesusiwa
Kilimo kiko Mashambani. Hizi mbwembwe za kwenye keyboards hazisaidii wakulima.
Darsa gani mkuu, maana hali halisi za wakulima tunazijua, siasa za wanasiasa kuwanufaisha wakulima hazijaanza leo.Sijakuelewa. Nani anae tafuta pesa? na nani anaetafuta uteuzi? Labda tuanzie hapo halafu tukupe darsa hayo utayapata wapi na vipi.
BBT ni mpango wa kipekee kuwahi kutokea Tanzania ( pengine hata duniani) ulianzoshwa na amama Samia kwa kiwango kikubwa kupitia rasilmali mama ya Tanzania ambayo ni ardhi, kwa sasa kngo kikubwa unasimamiwa na Mheshimiwa Bashe, Waziri wa Kilimo: Jiponee na jisikilizie:BBT ni NINI?