Uchaguzi 2020 Membe aenda Tume ya Uchaguzi kuhakiki fomu zake kabla ya kuziwasilisha rasmi kesho

Uchaguzi 2020 Membe aenda Tume ya Uchaguzi kuhakiki fomu zake kabla ya kuziwasilisha rasmi kesho

Hivi hizi form si zilitolewa na wao Nec sasa hizo feki zimetoka wapi?
 
Kuna mwanasheria mmoja wa CHADEMA huko sehemu za Iringa au Mbeya alijaza fomu za ubunge, halafu akajiapisha mwenyewe ambapo ni kinyume cha sheria, na hivyo fomu yake ikatupiliwa mbali. Kuwa mwanasheria siyo kuwa bingwa wa kila kila kitu; uzoefu una matter sana. Lissu sasa hivi amekuwa anaongea maneno yanayoonyesha kuwa uwezo wake wa sheria umepungua sana, kwani hajafanya kazi zake za kutetea kesi za mazingira na haki za binadamu kwa muda mrefu sana tangu aanze siasa. Ndiyo maana mara nyingi amekuwa anaropoka madai kama vile siyo mwanasheria tena. Kumbuka kuwa hata Richard Nixon alikuwa mwanasheria mzuri sana kabla ya kuingia kwenye siasa; baada ya muda mrefu kwenye siasa akawa crook.
Huyo aliyejiapisha mwenyewe alikuwa anafanya usanii na mzaha!Ulishawahi kuona wapi mtu akijiapisha?Ndio ukanjanja wengine!Nimesema kujaza form kunatosha kuhakikiwa ndani ya chama kwani yaliyoko kwenye form ni maelezo ya kawaida sana hata darasa la 7 anajaza kwa ufasaha tu!
Mwambieni basi na JPM aende kuhakiki form zake NEC kama amejaza kwa ufasaha!
 
..kesi ya karibuni ambayo ninaikumbuka ni TL kumtetea Peter Lijualikali.

..hata alipokuwa bungeni, TL alikuwa ni msaada mkubwa ktk kurekebisha makosa ya serikali ktk miswada waliyokuwa wakiwasilisha.

..ukitaka kujua umahiri wa TL ktk sheria waulize wanasheria waliofanya naye kazi wakati wa bunge maalum la katiba.
Aliwakilisha Chadema kwenye kesi dhidi Zitto akishirikiana na Kibatala; wakati ule Zitto aliwakilishwa na Albert Msando, ambaye alikuwa hajulikani sana wakati huo. Chadema ilibwagwa!
 
Huyo aliyejiapisha mwenyewe alikuwa anafanya usanii na mzaha!Ulishawahi kuona wapi mtu akijiapisha?Ndio ukanjanja wengine!Nimesema kujaza form kunatosha kuhakikiwa ndani ya chama kwani yaliyoko kwenye form ni maelezo ya kawaida sana hata darasa la 7 anajaza kwa ufasaha tu!
Mwambieni basi na JPM aende kuhakiki form zake NEC kama amejaza kwa ufasaha!
Busara inasema kuwa kama huna uhakika, uliza. JPM aliwahi kuzijaza hivyo yeye anaweza kuwa ana uhakika, Membe ametumia busara hiyo, na iwapo Lissu ana uhakika, basi hana haja ya kufanya uhakiki. Ila sasa ikitokea kuwa jamaa wa tume wakamwambia kwamba fomu yake ina makosa basi asilalamike. And this applies kwa Magufuli pia, kuwa iwapo fomu zimebadilika na yeye akawa amefuata format ya 2015, pia silalamike iwapo tume itaona kuna makosa kweye fomu zake.
 
Hilo ni suala jingine unalozungumzia na ni technical!Hili la kujaza form hadi darasa la saba anaweza kwa ufasaha kabisa sembuse mwanasheria ambaye yeye ni area of exoperities!Come on bhana!!!!Kama ni makosa ya kibinadamu,mbona hamjahoji kwanini JPM hajaenda kuhakiki?Kama ni uzoefu,basi hata Lissu ni mzoefu na fomu hizo kwani amekuwa mwanasheria wa CDM kwa miaka mingi na hizo form zimekuwa zikipita kwake wakati wagombea wengine wanagombea urais kupitia CDM!
Tatizo hutaki kuamini kuwa wapo bunch of fools and idiots kwenye fani mbalimbali. Fuatilia humumu JF kilichotokea jimbo la Kibamba kwa mgombea wa ACT Wazalendo kuna video clip leo.
 
Aliwakilisha Chadema kwenye kesi dhidi Zitto akishirikiana na Kibatala; wakati ule Zitto aliwakilishwa na Albert Msando, ambaye alikuwa hajulikani sana wakati huo. Chadema ilibwagwa!

..Albert Msando yuko CCM, alitia nia ubunge wa Arusha mjini hakupitishwa.

..Ni vigumu wakili kushinda kesi zake zote. Na kushindwa kesi haimaanishi kwamba 100% wakili ni mbaya.

..mchango wa TL ktk kutetea wananchi WANYONGE hapa nchini ni wa kupigiwa mfano. mawakili wachache sana wana rekodi kama yake.
 
Tatizo hutaki kuamini kuwa wapo bunch of fools and idiots kwenye fani mbalimbali. Fuatilia humumu JF kilichotokea jimbo la Kibamba kwa mgombea wa ACT Wazalendo kuna video clip leo.
Nasema CDM ni taasis kubwa,suala la kujaza form linahakikiwa huko huko CDM na copy za form zinawekwa kama ushahidi!
 
Busara inasema kuwa kama huna uhakika, uliza. JPM aliwahi kuzijaza hivyo yeye anaweza kuwa ana uhakika, Membe ametumia busara hiyo, na iwapo Lissu ana uhakika, basi hana haja ya kufanya uhakiki. Ila sasa ikitokea kuwa jamaa wa tume wakamwambia kwamba fomu yake ina makosa basi asilalamike. And this applies kwa Magufuli pia, kuwa iwapo fomu zimebadilika na yeye akawa amefuata format ya 2015, pia silalamike iwapo tume itaona kuna makosa kweye fomu zake.
Form zina maelekezo ya namna ya kujaza!Wala sio jambo gumu kama mnavyoaminisha watu!
Watu mnadeal na petty issues mpaka mnaboa!
 
Form zina maelekezo ya namna ya kujaza!Wala sio jambo gumu kama mnavyoaminisha watu!
Watu mnadeal na petty issues mpaka mnaboa!
Mganga hajigangi; hasa yule anayedhani kuwa ana tatizo dogo tu.
 
..Albert Msando yuko CCM, alitia nia ubunge wa Arusha mjini hakupitishwa.

..Ni vigumu wakili kushinda kesi zake zote. Na kushindwa kesi haimaanishi kwamba 100% wakili ni mbaya.

..mchango wa TL ktk kutetea wananchi WANYONGE hapa nchini ni wa kupigiwa mfano. mawakili wachache sana wana rekodi kama yake.
Albert Msando alikuwa Wakili wa Zitto; na nadhani alikuwa bado ni kinda sana kwenye bar wakati huo, ila kesi hiyo ndiyo iliyomtangaza.

Halafu sijasema kuwa Lissu hana rekodi nzuri ya sheria, nimesema alipokuwa akipigania mazingira na madhara yake kwa maisha ya watu alikuwa mzuri sana kabla hajaanza siasa. Nilichosema ni kuwa siasa imempoteza sana; kurekebeshisa miswada hapa na pale kwenye bunge ni jambo dogo sana kuliko kuchukua jambo zima la kisheria na kuliangalia kwa mapana na marefu. Hata mimi nikiweza kuingia bungeni naweza kurekebisha miswada mingi kwa vile huletwa na makosa madogo madogo mengi sana, ambapo makosa mengine huishia kuingia kwenye sheria zetu. Ndiyo maana sheria zetu nyingi bado zimeandikwa vibaya sana. Kwa ujuzi wangu wa kuungaunga ninaweza kurekebishwa miswada mingi, lakini siwezi kusimama mbele ya mahakama kumtetea mtu kisheria.

Tofautisha kurekebishwa miswada iliyoandikwa vibaya na kusimama kutetea sheria; zaidi ya kujua elimu ya sheria na kuwa kwenye bar, utetezi wa sheria unahitaji uzoefu mkubwa ambao Lissu keshaupoteza. Zamani sana Lamwai naye alikuwa mahiri sana wa sheria, baada ya kuingia kwenye siasa akaijukuta anaanza kuyumba kwenye sheria, ndipo akaamua kuacha siasa na kurudia taaluma yake ya sheria.
 
Mgombea Urais wa ACT Wazalendo Bernard Membe leo amekwenda kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi Jijini Dodoma kuhakiki fomu zake kama ziko sawasawa kabla ya kuziwasilisha rasmi hapo kesho 25/08/2020.

Membe aliongozana na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo mkuu wa ngome ya vijana Abdul Nondo.

Yohana najiuliza huu utaratibu upo siku zote? Na je mgombea urais wa CHADEMA, Tundu Lisu amehakiki fomu zake?

Maendeleo hayana vyama!
Membe anajichosha maana hata kura laki 1 hafikishi
 
Back
Top Bottom