Uchaguzi 2020 Membe anaweza shinda uchaguzi ujao. CHADEMA kazi kwenu

Mkuu nawe umepoteza muda bure,chadema sasa hivi ajikite kwenye kutafuta japo wabunge watano katika mbunge lijalo,kuwashauri kuhusu mgombea urais ukitumaini kuwa watashinda urais ni ndoto za mchana

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Chadema haihitaji ushauri kama huu, hususam unaotolewa na mtu anae sound kama wa "lumumba".
Hii kazi itafanywa kwa taratibu za Chadema.
Mara mia awekwe hata Halima Mdee,Ester Bulaya, au hata diwani wa chadema kutoka kata isiyojulikana kuliko kumpokea huyo mtu.
HAIWEZEKANI TENA ....Huyu alikuwa akipinga hoja za chadema na upinzani kiujumla zilizokuwa na mwelekeo wa kukuza demokrasia....
**kuanzia hoja za kuwepo mgombea binafsi,tume huru ya uchaguzi/marekebeshisho/mabadiliko ya kikatiba.
Acha atundike daluga....tuuu.Labda aende ACT
 
Membe kumuamini kama mpinzani wa kweli inahitaji akili ndefu, yatakuja tokea ya mzee lowasa na sumaye hawa sio wakuamini hata wa 15% pengine atumike kuongeza wabunge wa upinzani,
Kachelo mbobezi.. hawezi kuisaliti kazi yake
 
Bila TUME huru ni kutwanga maji kwenye kinu
 
Anaweza shinda atashindaje bila kutangazwa? Kwa nn hamtaki kufikiri? Lowasa alishindwa membe ndio ataweza? Ktk watendaji wa tume membe kamteua nani?
 
Nafkr Lowasa na sumaye wangekuwa bado wapo chadema na membe akajoin the race hapo kdog wangeenda 50/50 na CCM , lakn kwa sasa hv ni ngumu , hakuna tumaini lolote zaid ya miujiza
 
Bila TUME huru ni kutwanga maji kwenye kinu

Nguvu ya uma ya kweli kweli haizuiwi na tume huru au isiyo huru. Kama umma ukimuelewa na ukimkubali mgombea, tume haiwezi kuzuia, hata kama sio 'huru'.
 
Mkuu umeelezea vizuri sana..na maelezo yako ni KWELI tupu..
Asante sana.
 

Hii ni aina ya ushauri inayoonyesha kama Tanzania ni taifa lililokufa. Yaani watu wake ama ni mazezeta au hawana umuhimu kabisa. Hawahusiki kabisa na mustakabali wa nchi yao. Ni Taifa linalomilikiwa na kufaidiwa na “CCM” na, pengine, “CHADEMA”. Wananchi wanaishi kwa huruma ya vikundi maslahi hivyo! Ni upumbavu mkubwa sana tuliorithi tangu kuasisiwa kwa taifa hili.

Yaani uchaguzi ni mapambano kati ya “CCM” na “CHADEMA”. Mikakati au njama za ushindi kwao ndio kitu muhimu. Ile dhana kwamba uchaguzi ni hatua muhimu ya wananchi kupata uongozi wa maana ni “illusion” - ndoto ya mchana. Cha maana ni kuzidiana kete kwa CCM/dola na upinzani! KUNA HAJA GANI YA UCHAGUZI WA AINA HII?

Kama hilo ndilo taifa aliloasisi Nyerere basi alifanya kitu cha ovyo sana. ALIUNDA NA KUTUACHIA CHAMA DOLA ambacho kinahakikisha dhana ya demokrasia ya vyama vingi haiwezekani nchini. Ni kupoteza muda, nguvu, jasho na damu za Watanzania kuwaaminisha kushiriki katika chaguzi hizi za viini macho! Hazina manufaa yoyote kwao.

SASA, unapotaka kuwaaminisha watu kuwa chama cha upinzani kinaweza kushinda uchaguzi kwa kumsimamisha MEMBE kama mgombea wake wa urais ni kuendeleza ULAGHAI uleule wa tangu enzi za awamu ya kwanza hadi leo. Dola ipo kuhakikisha CCM inashinda by hooks and crooks, PERIOD.
 
Membe ana jipya kwakuwa mfumo wa uchaguzi waratibu ni vyombo vya dola hata akiwa ameshinda hawawezi kumpa ushindi!
Tatizo lenu la kipuuzi kuacha h. Hapa inaonesha ulitaka kusema Membe hana jipya.... Lakini inasomeka membe ana jipya... Hivi shule mlienda kuvuta bangi?
 
Membe aende akagombee Kupitia ACT-WAZALENDO ili angalau wapate kura za Kusini,Magharibi,Visiwani na Wabunge kadhaa.
Lakini CHADEMA wakitaka kupunguza idadi na imani wampe Membe wajizike rasmi.
 
Hata hao wapinzani unaweza kuta ndo hao hao CCM kwenye vazi lingine tu!

Usiamini amini sana watu!
 
Membe kumuamini kama mpinzani wa kweli inahitaji akili ndefu, yatakuja tokea ya mzee lowasa na sumaye hawa sio wakuamini hata wa 15% pengine atumike kuongeza wabunge wa upinzani,
Kachelo mbobezi.. hawezi kuisaliti kazi yake
Membe aachwe apambane na CCM yao kwa njia zao...
Asikaribishwe upinzani kama mgombea, hakuwahi kuwa neutral katika suala la kukuza usawa wa kidemokrasia, akienda upinzani kuna watu kibao hatutashiriki uchaguzi believe.
Na mpaka sasa "speculation" zinaonyesha wabongo kibao ambao sio watu siasa,yani wapiga kura tu, hawana mpango wa kupiga kura.
Tutarudi kule waliojiandikisha milioni 15, walioshiriki zoezi la upigaji kura milioni 9.
Mshindi wa urais asilimia 75-85 yani rais anapatikana kwa kuchaguliwa na watu wasiozidi milioni 7.
Katika nchi yenye raia takribani milioni 56!!!
Hii inaonyesha kiasi gani watu "wamechoka"
 
Naunga mkono hoja watu wanapotosha kweli eti CHADEMA hawajajifunza eti kwa Lowassa ,kiukweli Lowassa aliibeba sana CHADEMA ,Bila Lowassa CDM/UKAWA isingekuwa na Wabunge na kura nyingi huo ndio ukweli hata CCM wenyewe wanaujua sema wanajaribu kupotosha tu.

Membe ni mtu sahihi wa Kupambana na ANKO MAGU maana anakijua kindakindaki CCM ,hata CCM wenyewe wanamuogopa Membe na ndio maana wanajaribu kupotosha na kuwakatisha tamaa upinzani kwamba hawakujifunza kwa LOWASSA.

Mziki wa 2015 ANKO anautambua na ndio maana anafanya figisu vyama visiungane na wakataka waweke sheria kibao kuzuia wagombea wasihamie vyama vingine kabla ya mwaka siku ya uchaguzi.

Twende na Membe - KAZI NA BATA.
 
Sasa imagine wanaotuandikia hizo habari za Membe, mara tuko uchumi wa kati ni watu kabisa wana nafasi katika vyombo vya serikali, kweli tutafika hiyo per capita ya 3000 usd by 2025?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…