Uchaguzi 2020 Membe anaweza shinda uchaguzi ujao. CHADEMA kazi kwenu


## Uko vizuri kwa propaganda za kuingiza watu kichakani na kuwachinja bila wao kujua kuwa wanaenda machinjioni. Safari hii unaonekana na kujulikana unapeleka watu kichakani. Haendi mtu huko. Kaeni na Membe wenu...

## Ushauri wako juu ya uchaguzi wa SZM mwaka jana hauwezi kuwa msingi. Ulibeti na ukabahatika. This time mkeka wako umeshachanika maana game ya kwanza tu, matokeo ni kinyume chako...!

## uchaguzi utaamuliwa kikanda. Jiwe anakubalika Kanda ya Ziwa Victoria (Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara na Kagera)...

Kwa hoja hii, sijui unaandika ukiwa wapi. Inawezekana uko DSM ama Dodoma. Mimi naposti ujumbe huu kwako nikiwa Kanda hii. Niko Shinyanga. Siyo kweli. Jiwe hana kura za moja kwa moja huku. Hakubaliki unless ashawishi watu kwa hoja na bahati mbaya kwake ni kuwa hawezi, hana ushawishi. Hakuna "automatic votes" kwa kigezo cha "usukuma wake" au eti ukanda wake...!!

Ipo mikoa kama Mara na Kagera. Huko hawaishi wasukuma. Kagera ni wahaya na wanyambwa; Mara ni Wakurya na wajita, wazanaki na mengine madogo dogo. Kihistoria mkoa wa Mara kwa ujumla hawaipendi CCM...

Kwa hiyo, wataweza kumchagua JIWE na CCM kwa kile kwa miaka mi5 uwepo wake na miaka zaidi ya 60 ya maisha ya CCM. Lazima atoe ushawishi kwa watu ili wamuelewe. Lazima CCM ijieleze kwa ufasaha ili ichaguliwe tena. Hakuna kura za mezani....!!

## Kuhusu Tundu Lissu kukubalika ndani ya chama yake. Yes, may be you are right...

Labda hujui na hutambui kuwa CHADEMA kina wanachama zaidi ya milioni 10 achilia mbali mashabiki na wapenzi. Sasa kama anakubalika ndani ya chama kwa kura zaidi 10M hajashinda huyo???

##. Sikia ndugu. CCM na MAGUFULI hawakubaliki na hawapendeki Tanzania. Magufuli is a dead horse. CCM is old fashioned house. CCM in its reality, is no longer exists...

Yote uliyoyaeleza hapo juu kwenye bandiko lako hayana impact kwake wala CCM yake. Ni propaganda za ulaghai tu kwa kudhani mnaandaa watu kisaikolojia kukubali ushindi wa uporaji....

This time haporwi na haibiwi mtu. Ni kwa katiba hii, NEC hii, mazingira haya haya. Lazima kitaeleweka tu. Ni ama zenu ama zetu....

We can agree on one thing;

Kwamba, Magufuli na CCM Urais kama kawaida yao watalazimisha ushindi siyo kwa BALLOT BOX bali kwa kutumia nguvu za kimfumo wa dola (fedha za umma, polisi, jeshi na TISS)...

Akilazimisha kutwaa ushindi mwaka huu 2020 hata atakapokuwa ameshindwa (na ofcoz ndivyo ilivyo) hapo ndipo mtakapoona yanayotokea nchi zingine hususaani Malawi juzi kati yakitokea Tanzania tena katika UNIQU STYLE....

Ataiona NGUVU YA UMMA (PEOPLE'S POWER) in its reality...

MAJIRA na NYAKATI ya haya kutokea ni SASA siyo KESHO tena....!!!
 
Mkuu unajipa matumaini hewa tu, Watanzania hatuko civilised hivyo eti tufanye waliyofanya Malawi.. Hakuna hiyo kitu boss.

Leo si tulikubaliana kuwe na 77 Nyeupe, vipi raia wameitikiaje hiyo?? Boss amini kwa raia sisi CCM itatawala mpaka itakapoamua kusema basi, la sivyo labda hiki kizazi kife na kutokomea chote..

From the top to the bottom Watanzania ni watu waoga kiasili. Tunaogopa hata kuingia kwenye soko la pamoja la EA eti kwa hofu ya kupoteza ajira na ardhi kwa Wakenya na wengine. We are inferiors by nature, PLS ACHANA NA MAWAZO ETI CCM WAKIJISHINDISHA WATU WATAINGIA BARABARANI. ONDOA HILO WAZO UNAJIDANGANYA
 
Huyo Membe ccm impeleke kwingine CDM tuko TL ......hizi mbinu zenu ni za kizamani sana
 
Tatizo la wapinzani wanafikiri wanaweza kulala na kuamka kuitoa ccm madarakani kwa chama kikongwe kama ccm kunahitaji mkakati wa muda mrefu kuwatoa madarakani lakini kila uchaguzi ukifika wanasubiria mtu toka ccm awatoe madarakani
 
Membe its a strategic plan kuja upinzani chadema tuwe makini tumejenga chama kwa mda mrefu mlimleta lowasa tukaawaamini tuna mtaji wa uaminifu wa wafuasi wetu tutumie watu wetu wanatosha hatuhitaji ccm aje atusaidie. Tutafanikiwa tu lissu anatosha...... Acha akpambane na ccm wenzake..
 

Mkuu Nami kakwambia watz wanahitaji maneno. JPM ndio DEAL lenyewe. Urais pigeni maneno Ila Ndo hivyo.
 
Kwa maono yangu, Lowasa alikuwa na mvuto zaidi na maandalizi makubwa kuliko Membe. Kwa mantiki hiyo sioni maajabu ya kumpa ushindi
 

So kwa Utendaji. Membe na Lissu wanamshinda JPM. Hivi nyie Ni wacongo au watz.
 
Watu wengine bhanaπŸ˜‚, yaani unawaza chadema kushinda uchaguzi kweli!??, hivi upo kwenye akili za wapiga kura!?, Mtaishia kuleta thread kama hizi lakini lakini chadema kuchukua dola ni ndoto. Trust me mkuu.
 

Mlikubaliana na nani hili la 77?

Angalieni, huu usije ukawa ndiyo ukweli kwenu/kwao....KUJIPA MATUMAINI HEWA...

Naamini katika falsafa ya;

".....hakuna cha asili ya binadamu kisichokuwa na mwanzo wake na vivyo hivyo mwisho wake....."

Historia iko wazi sana juu ya hili. Hakuna ubabe uliodumu kwa miongo mingi...

Na ubabe na uhahari huanguka katika majira na nyakati ambapo wahusika hudhani ndiyo wako imara zaidi kuliko nyakati zingine zote...

Haya ndiyo matumaini hewa. Hayatambui nguvu inayotawala uumbaji huu...
 
Unaota mchana kweupe.

Nisome hapo juu. Unaweza kuwa ndiyo wewe unayeoota mchana huu!!
 
Sasa Lengo la Membe ni kuiangusha CCM ili afanye kitu gani kipya, ebu acheni kituzingua. Kwanza chama cha Siasa tunachokitaka ni chama kinachoitwa JPM Philosophy. Hatuna Muda na waomba neti kwa kutoa Tanzanite, Diamond, Platinum
 
Kweli membe ni threat mpaka wewe unalia lia ivyo kada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…