Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

yamemkuta kama ilivyo jina lake musiba,tulimkanya sana hapa enzi ya mwenda zake akatuona tumekosa uzalendo wacha sasa avune upuuzi wake
 
Unajiabisha wewe kwa kushindwa kumchangia mwenzenu ambaye alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu wauawe.

Hongera sana Membe kwa kuwa na msimamo thabiti wa kutetea utu wa mwanadamu kwa kuwajibisha wale wote wanaoutweza.

Tungekuwa na watu japo 100 kama Membe nchi hii ingekuwa na mabadiliko fulani hata kwenye maadili.
 
Kwa nini haku appeal mpaka case ifike mahama za EAC, yaani yeye angeenda na mwendo wa ku apeal tu!
Sidhani kama hii case ilifika kwenye Mahakama ya Rufaa!
Well I’m just curious [emoji3166]
Alikuwa anakaidi wito wa mahakama kwa makusudi akijua mahakama isingekuwa na cha kumfanya bahati mbaya Uzi ukakatika/JPM akaondoka na kesi ikiwa imeshaamyliwa kuundelea upande mmoja.
 
Membe ni failure anayetapatapa.

Aliwahadaa ACT wazalendo kwamba ataingia dakika ya 89 na kufunga goli alafu akaishia kufanya kampeni za urais kwenye kijiji cha Rondo
Mkuu

Kufunga goli dakika ya 89. Ni kauli ya kijasusi sana kuliko unavodhani!

Unafikiri kufukuzwa kwake ccm ni Bahati mbaya!!!?

Alipaswa abaki ILI mwendazake amshulikie akiwa NDANI kuliko nje!

Kachero akiwa nje ana uhuru wa kutosha wa kufunga goli na kweli alifunga KWA kwenda Dubai na kurudi nchini dakika za mwisho!

Na ACT kutakua chama kikubwa sana tena chenye ushawishi mkubwa baada ya chadema kufa!!!

Zito anaenda kuwa mwenyekiti wa chama mkuu wa upinzani nchini!!!

Ujio wa Membe ACT haukua wa Bahati mbaya!!
 
Yeye adinde tu, Tunachomwombea ni uzima na uhai.

Kwani siku zinaganda??.

Magufulinists ni lazima tutarudi tu Katika Uongozi, ni lazima !!.
Magufulinists ni watu gani? Ni hao waliokuwa wanahamasisha watu kuuawa kama alivyokuwa anafanya Musiba, au ni wake waliokuwa wanaua, wanateka, kupoteza watu, na kuwabambikia watu kesi?

Kama ni hao, usahau kabisa. Uovu mkubwa hutokea once and forever. Baada ya pale watu huwa wamepata funzo, na hujenga tabia ya kutoruhusu kabisa uovu mkubwa usitokee tena.

Ni miaka mingapi imepita, umewahi kusikia Ujerumani ina kiongozi kama Hitler?

Ni miaka mingapi imepita umewahi kusikia Italy ina kiongozi kama Benito Mussolin?

Ni miaka mingapi imepita umewahi kusikia Chile wana kiongozi kama Augusto Pinochet.

Ni miaka mingapi imepita umewahi kusikia South Afrika ina kiongozi kama P. W. Botha?

Mataifa yote ambayo huwa yamepitia utawala wa kidikteta uliofanya uovu mwingi, baada ya pale huwa yanabadili mifumo ambayo hujenga chuki kubwa dhidi ya udikteta, na ndiyo maana huwa madikteta hawarudi tena na kupata nafasi ya aina yoyote.
 
Namwelewa sana Membe. Musiba ni jeuri kweli kweli. Binafsi sijawahi kumsikia Musiba akiomba msamaha hadharani wala kujuta hadharani kwa yale mambo yote ya hovyo aliyoyafanya badala yake anasubiri maaskofu wamuombee msamaha hadharani. Membe ni binadamu tena muungwana sana na naamini iwapo Musiba angeenda kwenye vyombo vyote vikubwa vya habari akakiri yote yaliyotokea na kumuomba msamaha Membe na wengineo aliowakosea na kuwaomba watanzania wote msamaha lazima Membe angefuta kesi na wala tusingefika huku kwenye hukumu.

Lakini yote kwa yote serikali iliombwa muda mrefu iunde tume ya maridhiano ya kitaifa ili kuondoa hasira zinazowaka ndani kwa ndani kwa watu waliumizwa na utawala uliopita lakini serikali haijalifanyia kazi suala hili. Kwa hiyo tutegemee tu huko mbele ya safari kuona kesi kama hizi za Musiba nyingi tu.

Kwa upande mwingine lazima watu wa hovyo hovyo lazima wajifunze katika kupitia hali ngumu na ikiwezekana nao wapitishwe katika njia zile zile au zinazofanana na walizopitisha wenzao ili wangine waliobaki wajifunze. Hili la Musiba na Sabaya liwafunze wale wote wanaofanya mambo ya hovyo kwa aidha kutumwa au kujipendekeza wajue kuwa itakapofika kusimama mahakaamani watasimama wao wenyewe kama watu wabinafsi na si vingenevyo.
 
Nchi imeoza hii!! TISS inachapa magazeti ya kuchafua raia wa nchi. Yaani taasisi inayotakiwa kuhakikisha nchi iko salama na ina utulivu ndio inashiriki kwenye kampeni za kuwavuruga wananchi?
Mkuu

Kitengo cha propaganda. Hicho mkuu!!

Kina kazi maalum !!

NADHANI. TISS watatafuta namna ya kumsaidia!kuna picha itachezwa tu halafu itamuokoa musiba kwenye hio ishu!!!

Kama alitumika bas ni KWA manufaa ya umma yasiyooonekana tena yenye faida KWA Membe!! Yeye mwenyewe tena kwa kazi yake ya kikachero!!!
 
kiongozi asiyesamehe hafai kuongoza watu membe huyu huyu je angekuwa raisi ingekuwaje ! kipimo cha akili ni karma

Kumsamaehe mtu mwovu anayehamasisha watu kuuawa ni ushetani mkubwa. Ni sawa leo umwambia Samia awatoe wafungwa wote wa makosa ya mauaji, halafu ndiyo useme.ni kiongozi mzuri.

Wauaji na wanaohamasisha mauaji ni mashetani wanaotakiwa kupigwa vita na kuadhibiwa vikali kwa nia ya kuwalinda binadamu wengine.

Ni kwa vile tu jeshi leta la Polisi nalo ni dhaifu sana. Musiba alistahili kukamatwa na kufunguliwa makosa ya jinai kwa kuhamasisha watu kuuawa.
 
Acha hizo, Musiba si WA kuonewa huruma!! Mwanaharakati uchwara
 
Ameshakataa huyo maaskofu, labda Zumaridi akienda atabadili maamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…