Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Ni faida zaidi kwa act kuliko chadema, chadema hawawezi mpokea moja kwa moja kwa sababu hawataki tudia kisa la 2015. Act hawana cha kupoteza maana mpaka sasa hawana kitu zaidi ya zitto.
chadema wakimchukua ni goli la kujifunga kwao. Wataisapoti act na mgombea wao ila hawatchukua wao kwa tiketi yao agombee.
 
Nimeamini hivi vyama Ni magenge ya watu, kumbe membe kaonewa naye, kamati kuu haina mamlaka ya kumfukuza MTU uwanachama.sasa kina silinde wanakokimbilia ndo kupo vivo duh
 
Kwa act, kwa kumchukua membe wao watapata kitu zaidi ya kupoteza! Kwa sasa hawana kitu. Nothing to lose sio kama chadema wakimchukua membe moja kwa moja kama mgombea wao.

Nami nionavyo ni kama mleta uzi, kuwa lissu ndiye atakuwa mgombea wa chadema ila hatorudi nchini, na kujitoa automatically! Chadema wataisapoti act.

Haina ubishi, membe hawezi gombea kupitia sisiemu ila kauli yake ya chochote chaweza tokea kati ya juni na octoba na alipoongea hapa nilimuangalia mara mbili sura yake iliangalia dawati na kuiinua na kuwa na usitiaz zaidi, niliamini anaenda gombea urais, kwa tiketi ya act...
 
Nimekusoma halafu kama sijakuelewa vizuri, au kama ni hayo maono yenu nadhani hayajakamilika, mmeota ndoto lakini ikaishia njiani, au huko mbele hiyo ndoto imewadanganya/haitekelezeki.

Kama ACT itasimamisha mgombea Urais Zanzibar, something which is very much likely, itawezekana kweli hao ACT wasimamishe tena mgombea Bara wakiwa kwenye coalition na Chadema? kwamba Chadema hawana mtu yeyote wakugombea tofauti na Lissu!, watakuwa hawajiamini, na kwa chama kinachojinasibu kuwa kikuu cha upinzani ku-fall kwa hii simple trap kwangu itanishangaza.

Hivi Membe himself anakubalika kwa kiasi gani kama mwanasiasa nchi hii? anaweza kweli kupewa hiyo nafasi akaitendea haki kwa kiwango kinachohitajika? kwangu Membe ni jina tu lile linatembea, but sioni chochote cha ziada kwake, JK alimbeba wakati ule but now, no more.. he is done.
 
Mkuu mbona msajili kasema muda wa kujiunga ushaisha!!!!!!
 
Amesema lkn kuwa hakuna ajuae Mungu kapanga nn juu yake na Magu pia. Oct. mbali tutegemee lolote hapa katikati.
Hawa mambwiga wa Lumumba kila siku nawaambia hawaelewi wanajifanya wao ni miungu watu,wanatukana mamba kabla hawajavuka mto.
 
Wewe umeanza kuchanganikiwa na barafu za moto wako, we unadhani sisi chadema tunaweza kutegemea chama cha hovyo kama Act kukiunga mkono...nakuomba uhamie ccm huko ndo kuna zero brain .
Dah...
Things are Falling apart aisee..
 
Membe asizuiwe kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM, ili Magufuli ajipime kupitia kwake namna anavyokubalika ndani ya chama chake na pia kuonesha demokrasia kama kweli ipo huko.
 
MSIMAMO WA MEMBE KUHUSU KUGOMBEA URAIS

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe amesema kuwa atagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 endapo tu Chama cha Mapinduzi kitabatilisha adhabu aliyopewa.

Amesema adhabu ya kufukuzwa uanachama ilitolewa kimakosa kwa sababu uamuzi ulitakiwa kufanywa na Halmashauri Kuu lakini badala yake ulifanywa na Kamati Kuu. "Kwa kuwa chombo kinachotoa adhabu ni Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), na kwa kuwa Kamati ya Maadili tayari imeandaa taarifa yake na wameipitisha kwenye Kamati Kuu na kwa bahati mbaya kamati kuu ikatamka kwamba Membe tumemfukuza. Mpaka hapo Halmashauri Kuu [ya CCM] iatakaposema mheshimiwa Membe hana hatia, wakitamka hivyo leo [jana] au wakitamka hivyo kesho [leo] tutajaza kugombea Urais jumatatu asubuhi," amesema Membe.

Chanzo: swahilitimes

Kazi ipo mwaka huu hakyanani!
 

Mkuu salary slip hakuna mipango yoyote bali ni kupoteza kujiamini tu. Hapo ccm walipo wanaomba usiku na mchana wapinzani wa kweli wasisusie uchaguzi. Maana wanajua hilo litawaweka kwenye mazingira magumu, kwani wapiga kura watakuwa wachache mno, pia taswira yao itachafuka kimataifa, halafu watakosa uhalali wa wananchi. Lakini wanajua wapinzani wakishiriki, watahalalisha hicho walichopanga kufanya kwa maslahi ya chama chao. Wapinzani wadai tume huru ya uchaguzi, hakuna kisingizio cha muda, kwani madai halali hayana muda, hasa kwa watu wenye nia ovu.

NB: Salary slip ww ni nguli hapa jukwaani, inakuwaje unaandika bila kuweka koma, wala nukta! Unakwama wapi sheikh wangu?
 


Pia wanaweza kufikiria kuungana tena kufanya UKAWA nyingine
 
Mkuu hawa jamaa ni wazi kuwa wameishiwa hoja nguvu na karata yao ya mwisho iko kwenye UPORAJI na siyo kwingine.
 
Membe asizuiwe kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM, ili Magufuli ajipime kupitia kwake namna anavyokubalika ndani ya chama chake na pia kuonesha demokrasia kama kweli ipo huko.
He has never been a threat! Hata akifanya hivyo poa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…