Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Namba moujer huwa ni mwepesi sana wa kusamehe ukiamua akusamehe..
Na ukijiona una kiburi utajua kiburi chake..
Akili kichwan mwako tu kudeal na nba moujer wetu
 
Kwenye ubobezi nakataa, mbobezi gani anadukuliwa mawasiliano ya simu kirahisi rahisi.
Huwajuwi watu wa Dunia ya kwanza walio wahi kudukuliwa wenye nguvu kubwa kuliko Jiwe !? Au huwa mnasomaga gazeti la Uhuru tu
 
Simtishi Membe bali ni kumjulisha kuwa baada ya zoezi la uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu kwa hakika satoshi magumu mno!


Kama wasemavyo wao kwamba MWENYE KULITAFUTA NA HULIPATA.


Ni hayo tu.
Ulikuwa wapi siku zote?? UNACHEKESHA SANA 🤩🤩
Screenshot_20200624-091356_Chrome.jpg
 
Jasusi mbobezi Membe: Kudukua ni kosa la jinai, ukipatikana na hatia na ushahidi ukiwepo unafungwa gerezani....Nimewauliza kwenye kikao, nani kanidukua

Wajumbe: Hatujui mkuu,
 
Mumenielewa? Nmeeleweka?. Sasa naomba Vijana wote kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mtulie, Msilete ghasia zozote, tulieni hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu Mapema. Naelewa jinsi Mioyo yemu inavyowaka Moto. Lakini muwe na imani kwa sababu leo nmepigiwa simu nyingi sana kutoka Dar Es Salaam na kutoka Mikoa mingine
Sjui Kwa nini Historia huwa inamatokeo ya kweli!

Woote waliowahi kuusaka uraisi Kwa nguvu waliambulia patupu, na huyu Jamaa haitatokea awe Raisi wa hii nchi ya wastarabu na Taifa la wacha Mungu
 
Nimpongeze kwa kuendelea kujipa moyo; bado muda upo.

Mh Membe akumbuke tu shida sio kuruhusiwa, shida hiyo fomu nyingine unaipata wapi?

Wakati wa Dodoma zile zigazaga mlifurahia sana; Mungu akaamua kuwaletea kipenzi chake Watanzania.

Sasa leo tuendelee kuwa wapole na kukubali matokeo kama alivyokubali Mh Lowassa kipindi kile; hakuendelea kukimbizana alikubali uhalisia.

Tuachieni Dk wetu Rais Magufuli twende naye mbele ya safari Mungu atatuongoza; haya mambo ya kila mtu kugomabania kama mnaweka kumbukumbu makumbusho, hatutaki tena.

All d best
 
Smoothly and silently [emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211]
 
Nikiona mtu anaandika kwa all caps huku akiwa hajui matumizi ya koma ama nukta, namuona ni mpuuzi kama mpuuzi mwingine.
Kuna style inamtambulisha mtu kiasi mpaka akija na ID nyingine unaweza mshtukia.

Mleta uzi hii ndiyo style yake miaka yote.

Sasa hapo hujaanza kudeal na misspelling.
 
Hivi Buku 7 pale mitaa ya lumumba mmeongezewa ujira wenu ama bado kama wafanyakazi wengine? ukiona mtu anaandika mwandiko huu, ni kikundi cha waliokuja mjini kutokana na mbio za mwenye na walipatikana kupitia mikesha ya mwenge
 
Alafu na ofisi ya kuchukulia form imepigwa kufuli la kilo tano na sekretari kapewa likizo ya miezi sita hukoo ughaibuni akatulie.
 


Membe anasema:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM, tukafikia mwafaka na Washauri, Tukafikia uwamuzi kwamba, sisi hatujamkosea mtu, sisi hatujawa waharifu, sisi hatuna uoga na tunaniamini, sisi tuna haki kabisa kabisa ya kugombea urais huu kwa sababu tunalindwa na Katiba sio Utamaduni. Tunalindwa na Katiba ya Nchi.

Lakini tukasema, kwakuwa Kamati Kuu tunaiheshimu, tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Tungependa basi, kamati Kuu itamke iseme kwamba, kile tulichokisema sisi Wakati ule ni Mapendekezo ni Bahati mbaya yalitoka nje. Ni mapendekezo ambayo yatafanyiwa Uamuzi na Halmashauri kuu ya taifa mwezi ujao wa Saba.

Na mpaka hapo Halmashauri kuu ya Taifa itakapo kaa, Mheshimiwa hana hatia. Wakitamka hivyo leo, au wakitamka hivyo Kesho, tutajaza kugombea urais Jumatatu asubuhi. Naomba nirudie, kwakuwa chombo kinachotoa adhabu ni Halmashauri kuu ya Taifa, na kwakuwa kamati ya Maadili tayari imeandaa taarifa yake na wameipitisha kwenye Kamati Kuu na kwa bahati Mbaya Kamati kuu ikatamka kwamba "Membe tumemfukiza" kinyume cha Utaratibu. Kamati kuu au Msemaji yeyote au Katibu Mkuu au Katibu Mwenezi, akieleza leo kwamba alichokisema Mheshimwa Membe ni sahihi, sisi tunayo repoti iliyotoka kwenye Kamati ya Maadili na Sisi Kamati kuu tumeshaweka mapendekezo yetu, tunayapeleka kwenye NEC.

NEC inakutana mwezi ujao lakini Shughuli za Urais zipo sasa, mpaka hapo NEC itakapo kaa na kuamua iwapo Mheshimiwa Membe afukizwe au la!, Sasa hivi Mheshimiwa Membe yupo huru Kujaza Fomu, Kugombea, Kupata Wadhamini, na kujipima na Rais. Wakitamka hivyo leo au Kesho, Jumatatu nitajaza Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano CCM Oyeee..!!

Lakini Kamati Kuu inaweza kukataa, ikasema hapana, sisi tulichoamua tumeamua, Mheshimiwa Membe tumemfukuza, sasa yeye akitaka aende Upande mwingine tukutane mwaka 2020. Kamati kuu ni kubwa, inaweza kabisanikakataa. Ikikataa, huwezi mimi kunituma niende Dodoma. Niende kule nikikataliwa kuchukua Fomu? Je, nikipewa ile Fomu nikaenda kwenye Mkoa au Kwenye Wilaya nisimkute anayekusika, anasema ameitwa Dodoma kwenye Ushauri au unauguliwa na Mkwe wake nimsubiri baada ya Siku Mbili? Haitawezekana.

Kwahiyo kugombea kwetu kwenye Chama cha Mapinduzi, ambapo kungewasha hisia kubwa na Msisimko Mkubwa wa Watu kwenda kupiga kura. Na watu wote wangesema Uchaguzi huu unanoga kama mnavyo sikia Uchaguzi wa Zanzibar unavyo Noga, you Mnogeshaji ni Mimi. Ukinikataa mimi nisiende kugombea, Uchaguzi huu hauonogi!.

Na niwaambie Siri.. Naiambia Tanzania na Dunia na nyie watu wangu wa Rondo. Na nimalizie tu kwa kusema hivi, Mimi sitakwenda Dodoma Mpaka Kamati Kuu, au Mjumbe yoyote wa Kamati Kuu atakapo nieleza Mheshimiwa Membe upo Huru fanya hivyo. Kwa sababu tusipofanya hivyo, tutaingia kwenye Mitego. Tutaingia kwenye nini?.. (Mitego)... Tena inaitwa Shilibata.. Utanasa.

Ni lazima tupewe ridhaa, kama hatutapata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri kwenye Uchaguzi huu. Hilo la Kwanza.

La pili;

Uchaguzi ni Mwezi wa ngapi? (Wananchi wanaitikia... Wa kumiii...)

Huu ni mwezi wa ngapi? ( Wananchi wanaitikia wa Sitaaa)

Chochote kinaweza kutokea hapa katikati.(Wananchi wanapiga Makofi na Kelele)

Mumenielewa? Nmeeleweka?. Sasa naomba Vijana wote kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mtulie, Msilete ghasia zozote, tulieni hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu Mapema. Naelewa jinsi Mioyo yemu inavyowaka Moto. Lakini muwe na imani kwa sababu leo nmepigiwa simu nyingi sana kutoka Dar Es Salaam na kutoka Mikoa mingine ya Kusini wote wakiwa na Mioyo hii.

Lakini naomba tutulie, tusilete fujo, tusilete gasia yoyote Vyote tumuachie Mwenyezi Mungu. Lengo letu sisi tuwe na Uchaguzi wenye amani lakini wengine sisi hatutoacha kueleza Ukweli kwa sababu ukweli ndio hazina ha Siasa.

Nitasema kweli? (Wananchi wanaitikia.. Daima)

Fitina kwangu? (Wananchi wanaitikia.. Mwiko)

Asanteni na salaam Aleikum.

Pia Soma:

Elections 2020 - Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Alionyesha misimamo yake dhidi ya jiwe. Pumzika kwa amani Membe
 
Back
Top Bottom