Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

hivi aliyemwambia Membe kuwa wananchi wanamuhitaji yeye ni nani?binafsi naona Membe hana ushawishi wowote compared na Magufuli alivyo sasa au hata Mbowe.
 
Hamna mwenye uwezo Wa kumpinga Bwana Mkubwa ndani ya CCM..
Kinachoangaliwa hapo ni je Katiba ya CCM ilifiatwa wakati wa kimfukuza uanachama Membe?

Kama haikufuatwa ni kwanini haikufiatwa na baada ya hapo ndipo mtakapojilua kuwa chama kina was mwenyewe.
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
Vigezo anavyo,,lakini tamaduni yetu haitaki
 
Yeye alishasema hajapewa barua yeyote ya kufukuzwa Uanachama. So yeye bado ajiona yu mwana CCM mwenye sifa za kugombea nafasi hiyo pendwa
Lakini hajaforce,anasema akikubaliwa kuchukua form atachukua,asipokubaliwa haendi dodoma,
Mbona kaeleza kila kitu wazi?
 
Ok
Kumbe tunabaguana tena
Ofisi gani intampa hizo fomu, Kama anatumwa na K. Kikwete na wanamtandao aende chama chochote maana jumatatu fomu hapewi ofisi yoyote ya CCM, na ajiandae kweli kweli anaemtuma kachelewa angempa urais 2015, watu wa pwani walijiaminisha ccm washaimiliki sasa ndio basi na ccm hamtaikamata tena. Aanzishe vita bwege huyu tutamfuata huko aliko na AK47 tumevumilia sasa basi, ruhusa inachelewa sana, moto auwashe hio wiki ijayo. Hio corona ya Bibi zake.
 
Tuliza mshono huo sisi ndiyo wana ccm na tupo tayari kumuunga mkono

Kwani shida iko wapi, kama mnaumia sana nendeni mumpe fomu ya chadema agombee.
Mbona nyie mliwafuta uanachama akina sirinde kupitia kikamati cha mbowe na wao hawajataka kung'ang'ania huko?
Yeye CCM ameachamo nini, kama kingunge aliondoka yeye ni nani sasa?
 
Bado yupo yupo sana hapo hadi October tumkabidhi inchi ndani ya ccm.
Kwani shida iko wapi, kama mnaumia sana nendeni mumpe fomu ya chadema agombee.
Mbona nyie mliwafuta uanachama akina sirinde kupitia kikamati cha mbowe na wao hawajataka kung'ang'ania huko?
Yeye CCM ameachamo nini, kama kingunge aliondoka yeye ni nani sasa?
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
Hoja ya msingi iko palepale.
Katiba yenu CCM inamruhusu Membe kama wengine kuchukua form ili kuomba kuwa mgombea urais, kwani ni mwanachama hai.
Hivyo basi akipenda anaweza kuitumia haki yake. Anafaa au hafai kwa macho yako haimwondolei haki hiyo.
 
Ofisi gani intampa hizo fomu, Kama anatumwa na K. Kikwete na wanamtandao aende chama chochote maana jumatatu fomu hapewi ofisi yoyote ya CCM, na ajiandae kweli kweli anaemtuma kachelewa angempa urais 2015, watu wa pwani walijiaminisha ccm washaimiliki sasa ndio basi na ccm hamtaikamata tena. Aanzishe vita bwege huyu tutamfuata huko aliko na AK47 tumevumilia sasa basi, ruhusa inachelewa sana, moto auwashe hio wiki ijayo. Hio corona ya Bibi zake.
Ccm wapo tayari kufanya lolote hata kumwaga damu ya mtu au kutoa uhai kabisa, ili kutetea maslahi yao. Na hapa ndo idara ya usalama inapopoteza weledi wake
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
CDM mtuache asije akasababisha watu wetu wazidi kuuwawa.
 
Membe anasema:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM, tukafikia mwafaka na Washauri, Tukafikia uwamuzi kwamba, sisi hatujamkosea mtu, sisi hatujawa waharifu, sisi hatuna uoga na tunaniamini, sisi tuna haki kabisa kabisa ya kugombea urais huu kwa sababu tunalindwa na Katiba sio Utamaduni. Tunalindwa na Katiba ya Nchi.

Lakini tukasema, kwakuwa Kamati Kuu tunaiheshimu, tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Tungependa basi, kamati Kuu itamke iseme kwamba, kile tulichokisema sisi Wakati ule ni Mapendekezo ni Bahati mbaya yalitoka nje. Ni mapendekezo ambayo yatafanyiwa Uamuzi na Halmashauri kuu ya taifa mwezi ujao wa Saba.

Na mpaka hapo Halmashauri kuu ya Taifa itakapo kaa, Mheshimiwa hana hatia. Wakitamka hivyo leo, au wakitamka hivyo Kesho, tutajaza kugombea urais Jumatatu asubuhi. Naomba nirudie, kwakuwa chombo kinachotoa adhabu ni Halmashauri kuu ya Taifa, na kwakuwa kamati ya Maadili tayari imeandaa taarifa yake na wameipitisha kwenye Kamati Kuu na kwa bahati Mbaya Kamati kuu ikatamka kwamba "Membe tumemfukiza" kinyume cha Utaratibu. Kamati kuu au Msemaji yeyote au Katibu Mkuu au Katibu Mwenezi, akieleza leo kwamba alichokisema Mheshimwa Membe ni sahihi, sisi tunayo repoti iliyotoka kwenye Kamati ya Maadili na Sisi Kamati kuu tumeshaweka mapendekezo yetu, tunayapeleka kwenye NEC.

NEC inakutana mwezi ujao lakini Shughuli za Urais zipo sasa, mpaka hapo NEC itakapo kaa na kuamua iwapo Mheshimiwa Membe afukizwe au la!, Sasa hivi Mheshimiwa Membe yupo huru Kujaza Fomu, Kugombea, Kupata Wadhamini, na kujipima na Rais. Wakitamka hivyo leo au Kesho, Jumatatu nitajaza Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano CCM Oyeee..!!

Lakini Kamati Kuu inaweza kukataa, ikasema hapana, sisi tulichoamua tumeamua, Mheshimiwa Membe tumemfukuza, sasa yeye akitaka aende Upande mwingine tukutane mwaka 2020. Kamati kuu ni kubwa, inaweza kabisanikakataa. Ikikataa, huwezi mimi kunituma niende Dodoma. Niende kule nikikataliwa kuchukua Fomu? Je, nikipewa ile Fomu nikaenda kwenye Mkoa au Kwenye Wilaya nisimkute anayekusika, anasema ameitwa Dodoma kwenye Ushauri au unauguliwa na Mkwe wake nimsubiri baada ya Siku Mbili? Haitawezekana.

Kwahiyo kugombea kwetu kwenye Chama cha Mapinduzi, ambapo kungewasha hisia kubwa na Msisimko Mkubwa wa Watu kwenda kupiga kura. Na watu wote wangesema Uchaguzi huu unanoga kama mnavyo sikia Uchaguzi wa Zanzibar unavyo Noga, you Mnogeshaji ni Mimi. Ukinikataa mimi nisiende kugombea, Uchaguzi huu hauonogi!.

Na niwaambie Siri.. Naiambia Tanzania na Dunia na nyie watu wangu wa Rondo. Na nimalizie tu kwa kusema hivi, Mimi sitakwenda Dodoma Mpaka Kamati Kuu, au Mjumbe yoyote wa Kamati Kuu atakapo nieleza Mheshimiwa Membe upo Huru fanya hivyo. Kwa sababu tusipofanya hivyo, tutaingia kwenye Mitego. Tutaingia kwenye nini?.. (Mitego)... Tena inaitwa Shilibata.. Utanasa.

Ni lazima tupewe ridhaa, kama hatutapata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri kwenye Uchaguzi huu. Hilo la Kwanza.

La pili;

Uchaguzi ni Mwezi wa ngapi? (Wananchi wanaitikia... Wa kumiii...)

Huu ni mwezi wa ngapi? ( Wananchi wanaitikia wa Sitaaa)

Chochote kinaweza kutokea hapa katikati.(Wananchi wanapiga Makofi na Kelele)

Mumenielewa? Nmeeleweka?. Sasa naomba Vijana wote kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mtulie, Msilete ghasia zozote, tulieni hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu Mapema. Naelewa jinsi Mioyo yemu inavyowaka Moto. Lakini muwe na imani kwa sababu leo nmepigiwa simu nyingi sana kutoka Dar Es Salaam na kutoka Mikoa mingine ya Kusini wote wakiwa na Mioyo hii.

Lakini naomba tutulie, tusilete fujo, tusilete gasia yoyote Vyote tumuachie Mwenyezi Mungu. Lengo letu sisi tuwe na Uchaguzi wenye amani lakini wengine sisi hatutoacha kueleza Ukweli kwa sababu ukweli ndio hazina ha Siasa.

Nitasema kweli? (Wananchi wanaitikia.. Daima)

Fitina kwangu? (Wananchi wanaitikia.. Mwiko)

Asanteni na salaam Aleikum.

Pia Soma:

Elections 2020 - Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Total stupidity! Kwani ulizaliwa kuwa rais? Huyu na yule jamaa wa Bunda hakuna tofauti. Kila leo wanwaza siasa. Nadhani walifaidi sana ndani ya siasa, mbona sisi tunalima?
 
Kinachoangaliwa hapo ni je Katiba ya CCM ilifiatwa wakati wa kimfukuza uanachama Membe?

Kama haikufuatwa ni kwanini haikufiatwa na baada ya hapo ndipo mtakapojilua kuwa chama kina was mwenyewe.
Kama Katiba Mama ya Nchi ameisigina na hamna aliyethubutu kumkemea sidhani kama Kikatiba uchwara cha CCM kinaweza kumtisha vyovyote..
 
Back
Top Bottom