Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Watanzania sijui tunakoelekea naanza kuwa na wasiwasi. Tuweni na umoja ili nchi isije sambaratika, nchi za kiafrica bado siyo wamoja sana kama tunavyodhania. Natamani jambo hili viongozi wetu wapo wakae wayamalize, Membe atatuletea shida unaona mwelekeo wake kudai tume huru siku za nyuma mbona hakusema? Halafu na wewe usizungumzie mambo ya AK47 usijianishe kutumia nguvu si sawa na wala siyo njia sahihi nchi inaweza ingia kwenye machafuko makubwa na visasi. Hatutaki nchi yetu ifike huko, itaikadi za chama zisigawe nchi. Nasema Membe aitwe aelezwe aache atatuleuea shida. Unaona reaction ya watu kama.wewe wanakimbia kusema silaha hiyo hapana ndugu yangu italeta shida tutaharibu kila kitu na hakuna atakaeshinde.
Dawa ya yote haya ni CCM waweke democrasia kwny mchakato wa uchaguzi..kila mwanachama mwenye Nia achukue form mbona Sita kwenye uspika alikubali ninyi kwnn hamtaki mnaogopa nini?
 
Jiwe hapati usingizi ujue

SUBIRI KIDOGO
Nikikumbuka ile 2015 Magu dizaini kama alichanganyikiwa hivi kipindi kile cha kampeni EDO alijua kumuhenyesha asee. Ijapokuwa edo hakuwa mwana mageuzi wa ukweli....leo naona ny'aa inagonga pichu[emoji23][emoji23][emoji23] Ila huyu atamfanya achanganyikiwe zaidi
 
Aise...
Hivi bado kuna wanaowaza kushindana na magu? Yaani kwa hapa tz upinzini kuchukua nchi bado sana labda damu imwagike au umoja wa mataifa uingilie kati ma tume iliopo ibadilishwe
 
Huyu barafuyamoto ni mtu ambae siku zote mimi na yeye huwa tunakinzani kimawazo na kimisimamo hapa JF yeye aikionekana kuwa ni mtu anaeunga mkono CCM na mimi nikiwa ni mtu naeunga mkono upinzani.

Hata hivyo,kwa mshangao mkubwa leo hii mimi na yeye tumewaza kitu kile kile kwa asilimia 100 jambo ambalo linenifanya nijiulize kama hii imetokea tu kwa bahati au vinginevyo ila nimekuja ku-conlude kuwa haya yatakuwa maono na hiki huenda ndio kinaweza kuja kutokea hapo baadae kabla ya Oktoba mwaka huu.

Ni hivi:Baada ya kuisikiliza clip ya Membe,ndani ya muda mfupi tu nikapata wazo kuwa Membe atahamia ACT-Wazalendo na atateuliwa kuwa mgombea na watachofanya CHADEMA ni kutosimamisha mgombe(watacheza mchezo wa kisiasa) alafu waje wamuunge mkono Membe na lengo ni wao kukwepa kurudia kosa kama lile la kumsimamisha Lowassa(hawatataka kuonekana wanachakuwa tena wagombea kutoka CCM hasa kwa ngazi ya uraisi).

Hivyo ndivyo nilivyowaza, ila kwa mshangao mkubwa, nimekuta na huyu member barafuyamoto nae kawaza kama mimi kwa asilimia 100 ingawa mimi nilienda mbali zaidi kwa kuwaza/kuamini watachofanya CHADEMA ni kumsimamisha Lissu alafu baadae Lissu atajitoa kwa kuhofia usalama wake na hatarudi nchini na mchezo huo wa kisiasa utakuwa umekamilika na CHADEMA wataamunga mkono Membe.

Najua yako yanayosemwa kuhusu Lissu kufanyiwa mizengwe kwenye uteuzi ila hizi zote zinaweza kuwa ni siasa tu zenye malengo fulani.

Tusubiri.

Maoni yangu:
Mimi kama mwananchi wa kawaida,nawashauri wapinzani wasirudie kosa la kumsimamisha mgombe yoyote aliekataliwa,kufukuzwa au kujiondoa CCM katika uchaguzi huu, hasa kwa nafasi ya uraisi, kwani wananchi teyari wana majereha katika mioyo yao hivyo kurudia kosa kama hili kupitia chama chochote cha upinzani ni kutonesha vidonda hivi na zaidi ni kukaribisha hatari ya vyama vya upinzani kudharauliwa, kupuuzwa na hata kukataliwa na wapiga kura na madhara mengine ni hali hii kuwakatisha tamaa wananchi wengi na kuwafanya wasijitokeze kwenye kupiga kura.

Hata Nyalandu nawashauri msimpitishe kuwa mgombea kwasababu hizi hizi nilizozitaja.
Mkuu una mahaba niue na Lissu! Huoni kwamba mwenyekiti wa chama katia nia na hivyo ni vyema akapewa nafasi?
 


Membe anasema:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.

Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!

Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.

Pia Soma:

Elections 2020 - Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

Kwani lazima agombee kupitia CCM vyama vipo vingi aende Chadema,ACT ,CUF .Membe kitu gani bana.Tukutane kwa debe .
 
Jamaa anapenda kuongea huyu actions zero, chagua moja sio kulia lia ,chagua ccm au pinzani mara moja, shushu mbobezi unalalamika muda wote vipi wewe? vyama vingi vipo hata Tz na muda una yoyoma fanya haraka kampeni zianze.
 
Kwa act, kwa kumchukua membe wao watapata kitu zaidi ya kupoteza! Kwa sasa hawana kitu. Nothing to lose sio kama chadema wakimchukua membe moja kwa moja kama mgombea wao.
Nami nionavyo ni kama mleta uzi, kuwa lissu ndiye atakuwa mgombea wa chadema ila hatorudi nchini, na kujitoa automatically! Chadema wataisapoti act.
Haina ubishi, membe hawezi gombea kupitia sisiemu ila kauli yake ya chochote chaweza tokea kati ya juni na octoba na alipoongea hapa nilimuangalia mara mbili sura yake iliangalia dawati na kuiinua na kuwa na usitiaz zaidi, niliamini anaenda gombea urais, kwa tiketi ya act...

Sioni ushawishi wowote wa ukweli wa kisiasa alionao Membe, sana sana ninachoona ni yeye kutokukubali kuwa kondoo kwa Magufuli kama walivyo wengine. Pia nguvu ya ushawishi ya kweli ya chama cha ACT iko pemba/Zanzibar, sehemu ambayo ni ndogo sana. Lakini kwa huku bara chama cha upinzani chenye ushawishi mkubwa ni CDM. Hata Lowassa hakuwa na ushawishi wowote wa kisiasa hiyo 2015, bali alikuta cdm ikiwa imepata hamasa kubwa. Vinginevyo angejiunga chama kingine angepata chini ya za Anna Mghwira.

Hata hivyo sitaki kuamini eti tatizo la upinzani ni mgombea, kwangu tatizo hasa la wapinzani kupata kura, ni tume isiyo huru ya uchaguzi. Iwapo wapinzani hawatasimamia hili kwa nguvu zote, itakuwa ni upotevu wa rasilimali muda na fedha. Ni bora kususia siku ya kupiga kura na kuhamasumisha wananchi kutokutokea siku ya kupiga kura, ili kushinikiza uwepo wa tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom