Watu wengi wameharibikiwa kwa sababu ya ushauri mbovu toka kwa marafiki.
Marafiki wa Membe wanamshauri agembee Urais kwa maslahi Binafsi.
Utaratibu wa CCM ni kumruhusu Rais aliyeko madarakani kumaliza muhula wake wa kikatiba wa miaka 10 endapo hajavunja Katiba ya Inchi/Chama, wala kukiuka ilani, imani na kanuni za chama katika awamu ya miaka 5 ya kwanza.
Lengo kuu ni kulinda Amani ya Inchi bila kuleta ushindani usio na tija.
Membe bado ana nguvu na miaka mitano ijayo atakuwa anafaa zaidi kugombea Urais .
Njia rahisi na fupi zaidi ya Membe kuupata urais 2020 ni kuwa karibu na Mh. Makufuli na sio marafiki zake ambao wanataka kuiuza Inchi kwa Mlo wa Siku moja.
Neno la Mungu linasema "ole wao".
Lazima tukiri. Katika Mawaziri waliopita katika awamu ya tatu na nne, hakuna Waziri aliyetukuka katika katika utendaji kazi kama Mh. Makufuli.
Katika Marais waliopita ukiacha Hayati Mwalimu Nyerere, hakuna aliyepigania maslahi ya Inchi kama Makufuli.
Kama tunaipenda Inchi yetu na hatuendekezi mambo ya urafiki , maslahi binafsi na chuki binafsi tumwache Mh . Makufuli amalize kipindi chache cha kikatiba.
Hata kama tutakuwa tunampenda na tunamhitaji, ni usaliti na kuivuruga Inchi kwa kubadilisha katiba ili aendelee miaka zaidi ya 10.
Hayati Mwalimu Nyerere alisema " Kama unarafiki, kanywe nae chai na si kutaka kumpeleka Ikulu"