Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Lissu hayupo tayari kushindwa kwa namna yoyote,yupo kishari zaidi na kulipa kisasi.kwa hiyo,hata apewe kura zake ahesabu mkononi,hata kibali,nia yake ni machafuko tu
mkuu we ni muongo sana , et hata apewe kura zake kuesabu atakataa, fanyeni hivyo muone kama atakataa na kumbuka ugombea wake wa kwanza wa ubunge mbona alishindwa hata yeye anakili , acheni izo mkuu tume ikimkata wajiamdae kwenda icc maana litakalo tokea kwa sasa wao ndo wanawajibika kwa asilimia 100 na hakuna namna wanaweza chomoka
 
Walitaka Lissu atafute wadhamini kimya kimya ili apate chance ya kumuua vizuri bila ya adha ya kutuma watu wakafungue cctv camera

"Membe lilikuwa pandikizi lilikokuwa limelengwa Chadema ila Kutendaa kosa sio kosa kurudia kosa ndio kosa"
 
Tume ya uchaguzi kwa maelekezo ya Magufuli na ccm ndio wanatumika kuaandaa machafuko. Inakuwaje nchi yenye wananchi karibia 60m wapiga kura wawe 29m+? Ina maana nusu ya watanzania wako miaka 18 na kuendelea? Kama idadi ya wapiga kura ni ya uongo, matokeo watatamgazaje ya ukweli? Kama sio kuandaa mazingira ya machafuko ni nini?
We mfano ulitaka uambiwe wangapi ndugu tindo?
 
Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe amesema wao wamepata wadhamini katika mikoa kumi

Amesema ACT-Wazalenda waliamua kutafuta wadhamini kimyakimya ili kuepuka kuteleza

Majina wa wateule wa kugombea Urais yanatarajia kutolewa na Tume ya Uchaguzi, NEC Agosti 25, na kampeni zitaanza Agosti 26

Chanzo: ITV
Huyu saikolojia yake inamtuma kwamba waambie NEC kuwa Tundu Lissu alianza kampeni mapema so akatwe.Hii ndio mantiki ya hoja yake.uchonganishi.
 
Sina tatizo na uelewa sheria wa Mh.Tundu Lissu kuzielewa hizo kanuni za uchaguzi.Hata wakiamu kumkata si kwa sababu alivunja kanuni Bali kwa sababu ndio nia yao ovu.
 
Sina idadi maalum, bali nataka idadi ya kweli, ili niwe na uhakika wa kitakachotangazwa.
Ndio maana nikakuuliza ili uridhike na hiyo idadi kuwa kwako hiyo ni kweli inatakiwa wataje wangapi??
 
Ndio maana nikakuuliza ili uridhike na hiyo idadi kuwa kwako hiyo ni kweli inatakiwa wataje wangapi??

Kama tunakaribia 60m, inawezekana vipi nusu wawe 18+? Halafu idadi ni ya kupika kisha mtake tukubali matokeo? Wanaotangaza matokeo kama wameweza kutengeneza idadi ya kupika, watashindwa nini kutangaza matokeo ya kupika?
 
Hivi ukweli au uongo wa matokeo huwa unaamuliwa na uwingi au uchache wa watu?
 
So, bwana Membe kaamua kukomaa. Atleast atatimiza ndoto za jina lake kuonekana kwenye karatasi za kura za Urais.

He is totally toothless and finished. CCM walikuwa sahihi kutimua watu wabinafsi kama huyu
 
Hivi ukweli au uongo wa matokeo huwa unaamuliwa na uwingi au uchache wa watu?

Matokeo huwa yanaamuliwa na wapiga kura halali. Sasa kama tume ya uchaguzi inapika idadi ya wapiga kura, matokeo yatakuwaje sahihi?
 
Wasalaam wana jamvi!

Mgombea wa ACT Wazalendo jana alikwenda mahakama kuuu kula kiapo kwa judge ... alipoulizwa na waandishi kuhusu njia yake ya kutafuta wadhamini aliweka wazi kabisa yeye alikuwa mtulivu kusoma kanuni na sheria hivyo ndio maana alitumia njia ya kutafuta wadhamini kimya kimya ili asivunje kanuni alizo zisoma na kuzielewa!

Alisema wazi kabisa hakutaka kuingia kwenye mtego wa kuanza kampeni kabla ya muda maana muda ya kujinadi bado haujafika mpaka hapo watakapo vuka kiunzi cha kuteuliwa na tume!

Ni wazi kuna mtu hapa alikuwa ana kumbushwa na kutumiwa salamu!

Wape salaaam....

Mswahilikavaasuti
Imekuwa vyema Chadema wamemstukia huyo Membe kuwa katumwa!

Hivi unawezaje kuyatamka maneno hayo, wakati ukijuwa kabisa kuwa mgombea wa CCM amekuwa akifanya kampeni peke yake kwa kipindi cha miaka 5 mfululizo, huku akiwazuia wapinzani wasifanye mikutano yoyote nchini!

Ikitokea NEC wamem-disqualify mgombea wa Chadema kwa kigezo hicho, basi hawana budi kutopitisha jina la mgombea wa CCM, kwa kuwa na yeye atakuwa amevunja kanuni hizo.

Kusiwe na "double standard" katika maamuzi ya Umma
 
Matokeo huwa yanaamuliwa na wapiga kura halali. Sasa kama tume ya uchaguzi inapika idadi ya wapiga kura, matokeo yatakuwaje sahihi?
Atleast ungelalamika kuwa idadi ya wapiga ni kubwa kuliko uhalisia ungeeleweka. Ila kusema idadi halisi ni ndogo na wewe unataka iwe kubwa hapo unatia shaka.
 
Huyu saikolojia yake inamtuma kwamba waambie NEC kuwa Tundu Lissu alianza kampeni mapema so akatwe.Hii ndio mantiki ya hoja yake.uchonganishi.
Ndio lao yeye na zito. Usidhani zile kelele za Zito zinamtakia mema lissu na CHADEMA
 
Lissu ni mkongwe wa sheria ni wazi hajakurupuka,anajua alifanyalo,wajichanganye kumuengua uchaguzi UTASIMAMA.
Mkuu Lissu kajichanganya, watamfix kwa kuanza kampeni kabla ya wakati. Alikuwa na haraka ya nini kuanza kupanda majukwaani na kuanza kuuza sera za CHADEMA. Kama akichomoa basi itakuwa tu ni huruma ya Tume, vinginevyo anachomolewa saa moja asubuhi.
 
Atleast ungelalamika kuwa idadi ya wapiga ni kubwa kuliko uhalisia ungeeleweka. Ila kusema idadi halisi ni ndogo na wewe unataka iwe kubwa hapo unatia shaka.

Boss kumbe muda wote hujaona kuwa ninachosema kuwa idadi ya wapiga kura ni kubwa kuliko inavyopaswa!? Ngoja nirudie tena. Watanzania tunakaribia 60m. Nusu ya hiyo 60 ni hiyo 29m+. Kama 29m+ ndio imejiandikisha kweli ni kuwa kila watanzania wawili, mmoja kajiandikisha kupiga kura? Hiyo ni sawa na kusema watanzania wote wenye miaka 18+ wamejiandikisha kupiga kura, japo ambalo sio kweli kabisa. Na inawezekana vipi watu wenye miaka 18 na kuendelea, idadi yao iwe sawa na walio na umri chini ya miaka 18?

Hapo huenda umeona concern yangu, kuwa idadi hiyo ya 29m+ sio ya kweli kabisa, na lengo la kuweka idadi kubwa hivyo ni ili kupika matokeo. Na kwa vyovyote matokeo hayo ya kupika ni kwa ajili ya kuibeba ccm, sasa kama sio kuandaa machafuko ni nini?
 
Back
Top Bottom