pjjande ngao
Member
- Nov 20, 2019
- 23
- 4
lazima anuke na atueleze zile appartment za vijana wake kule dom na dar...... na usajili anaofanya vyuo vikuu .........Labda Maembe ila kama ni Membe hapana ccm wote wezi hakuna mwenye moral authority aanze kwanza yule aliyehonga nyumba ya umma kwa hawara.
# niguse ninukeHuyu Membe anajiona ana nguvu sana ndani ya ccm wakati aliingia tano bora akagaragazwa vibaya hadi na January Makamba tu..
Kama anajiamini aje chadema achukue fomu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Haya mavyama hatari, ukimkosoa mwenyekiti tayari unaitwa kwenye vikao..
Bahati nzuri alikwiba na kula pamoja na cabinet yote akiwemo Mzee Meko... the reason Membe anadunda freely tangu Oct 2015. Mzee Meko sio clean kama mnavyodanganywa...Ajiandae kurudisha mabilion ya Watanzania aliyokwiba kutoka libya
Atapata tabu sana Membe atulie sasa,Huyu Membe anajiona ana nguvu sana ndani ya ccm wakati aliingia tano bora akagaragazwa vibaya hadi na January Makamba tu..
Kama anajiamini aje chadema achukue fomu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mikwara yake si mizuri sana kama Urais autafte taratibuHuyu jamaa ana mikwara sana
Hataweza kabisa ndio ameshaharibuMembe kwisha Habari yake
Ajiandae kurudisha mabilion ya Watanzania aliyokwiba kutoka libya
Ameharibu kila jamboHataweza kabisa ndio ameshaharibu
Akihamia kwingine atakuwa kama Lowassa leo hii ameshajichokea karudi kuomba msamaha alipotokaAmeharibu kila jambo
Upo sahihi kabisa,wana uwezo wakumchukulia kila kitu anajiharibia sanaWatu wanaongea kana kwamba system ikitaka kukuondoa inashindwa.
Unaondolewa dakika moja tu, ukiona system haikuondoi inakutumia na huenda hata wewe unatumika na unajua au hujui ila Watu wa nnje wanaweza wasijue.
Na inawezekana unaonekana huna madhara Umemalizwa unawekwa kama mfano watu watakua wakikuangalia wanajua nguvu waliyonayo Watu wa system wanakaa kimya wasije kuwa kama wewe.
Mtu aliyekua tishio CCM ni Lowasa tu Na kama alishindwa kuiua CCM basi CCM haiwezi kumpigia Magoti yeyote nchi hii.
Membe anaweza kupewa adhabu ya kutoshiriki masuala ya siasa ya CCM kwa mwaka mmoja, hapo atakua hana chakufanya au akaambiwa rudisha kadi yetu atakua pia hanachakufanya.
Sent using Jamii Forums mobile app
membe ni akili kubwa niguse ninukeNasikia Kolimba aliitwa pia. Baada ya hapo kilichomtokea wote tunakijua. Membe inatakiwa ufuate maadili ya Chama chako.
Jiandae kuwindwa kama swaladuuuh hata mimi natarajia kuchukua form2020 kupitia Ccm ....
Si akheri yao wanaitwa kwenye vikao?Haya mavyama hatari, ukimkosoa mwenyekiti tayari unaitwa kwenye vikao..
Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
WAZIRI wa zamani wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa nchini Tanzania, Benard Membe amesema, anasubiri kwa hamu, barua ya wito ya kumtaka kufika kwenye Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Anasema, “kutokana na wingi wa meseji, nashindwa kumjibu kila mtu aliyeniandikia ujumbe kuhusu tangazo la kuitwa kwangu. Niseme tu kwamba, nasubiri kwa hamu barua ya wito.”
Katika taarifa yake ya kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, tarehe 13 Desemba 2019 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, CCM kimeeeleza kuwa viongozi wake watatu wandamizi, “watahojiwa” na kamati yake ya maadili na usalama.
Polepole amewataja viongozi wanaopaswa kuhojiwa na kamati hiyo, kuwa ni Membe, Kanal Abdulrahaman Kinana na Luteni Yusuf Makamba.
Kinana na Makamba, waliwahi kwa nyakati tofauti, kushikilia wadhifa wa ukatibu mkuu ndani ya chama hicho, huku Membe akiwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.
Alisema, viongozi hao wandamizi, wataitwa mbele ya kamati hiyo, kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.
Membe, Kinana na Makamba, wamenukuliwa wakiutuhumu uongozi wa juu wa chama chao, kumkumbatia
Katika kinachoitwa, “kuvuja kwa mazungumzo yao waliyofanya kwa njia ya simu,” Membe, Makamba, Kinana, Nape Nnauye na January Makamba, kwa nyakati mbalimbali, walisikika wakimtuhumu Rais John Magufuli, kumkumbatia Cyprian Musiba, anayetukuna na kusingizia watu kadhaa mambo mbalimbali.
Kinana na Makamba, waliamua kufikisha malalamiko yao kwa Pius Msekwa, katibu wa kamati ya wazee ya chama hicho.
Katika barua yao kwa Msekwa, Makamba na Kinana wanasema, “vitendo vya Musiba, anayeonekana ametumwa na anayetumia mwamvuli wa CCM na Ikulu, kushambulia kila mtu, vinakidhalilisha chama chetu.”
Akiandika kwa kujiamini, kujibu madai hayo ya Polepole yanayomtaka kufika kwenye kamati ya maadili, Membe anasema, “…nasubiri kwa hamu sana barua ya wito. Nitakwenda; hoja zitatolewa na hoja zitapanguliwa.”
Jina la Membe – mwanadipromasia mashuhuri nchini aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka takribani nane ya utawala wa Jakaya Kikwete – limepata umaarufu mkubwa katika siku za karibuni, kufuatia kuhusishwa na mbio za urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 kupitia CC.
Hata hivyo, Membe mwenyewe hajaweka wazi jambo hilo, ingawa watu waliokaribu naye wanasema, “ni lazima atajitosa kwenye kinyanganyiro hicho.”