Uchaguzi 2020 Membe: Naufahamu uwezo wa Lissu, nitahakikisha anapata kazi kwenye serikali yangu

Uchaguzi 2020 Membe: Naufahamu uwezo wa Lissu, nitahakikisha anapata kazi kwenye serikali yangu

Usiku wa leo nimeota kuwa hapa kwetu yatatokea Kama yale yaliyotokea DRC, yaani was halisi wanapambana na hatimaye kushinda uchaguzi, mazungumzo yanafanyika na hatimaye anatangazwa mpinzani dhaifu na anakabidhiwa nchi 😩😩😩☹️☹️☹️
Ht 2015 uliota hvy hvy lkn hayakutokea
 
Go membe go, vuruga kabisa na tarehe 28 Oktoba kama kawa tumpe Magufuli kura ya urais.
 
Nadhani hayuko sawa, walio karibu nae wamsaidie
 
Membe baada ya uchaguzi anarudi CCM.

Lissu ndio mpinzani wa kwelii.
Nimepata hizi tetesi kuwa, huenda Jumanne ijayo akarejea CCM kwa sharti la kurejeshewa uanachama wake. Yuko kwenye majadiliano, ndio maana ya kufunga goli dakika 89

Upande mwingine huenda akaendelea kuwepo ACT lakini kwa kazi ya kuleta mgogoro kama ule ulioletwa na Lipumba kule CUF kiasi cha kina Maalim Seif kuhama.
 
Atleast Membe ametimiza ndoto yake ya maisha ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ.

Na yupo sahihi. Ni uhayawani kumuunga mkono katikati ya safari mtu mnayegombea nae nafasi moja. Why did he run in the first place?

Anachofanya sasa ni kujaribu kuretain some sort of respect anayodhani bado anayo ila moyoni mwake anajua kabisa hana lake na madame Queen Sendiga ana chances kubwa za kushinda Urais kuliko Membe
 
Dawa ya hawa watu kama Membe ni kuwapotezea tu kwa sasa. Hakuna sababu ya kuwajadili sana. Tuwaache waendelee kubwabwaja upuuzi wao, wakichoka watakaa kimya.
 
Membe yuko live anafanya mahojiano na redio Tehran mida hii na ameulizwa kuwa kuendelea kwake na harakati za kampeni haoni kama zinamuhujumu Lissu na upinzani kwa ujumla?

Membe amejibu kwa kuwa yeye anaongoza kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali anaona ingekuwa busara kwa upinzani kama wangeweka nguvu pamoja na kumsupport yeye, pia amedai anaufahamu vizuri uwezo wa Lissu kisheria na hivyo kumhakikishia kazi katika serikali yake mpya kadri ya katiba itakavyoruhusu.

Wakuu yapi maoni yenu?
HUYU ACT WAMFUKUZE, NI PANDIKIZI
 
Mimi nashangaa watu mnaomtoa akili Membe ila wa kutolewa akili ni Zitto na Maalim seifu,kwa sababu Membe anajulikana toka huko ccm jinsi alivyokuwa na uroho wa kugombea urais kiasi kwamba akajifanya anataka kutingisha hadi chama kwa mikwara mingi ila akaishia kutimuliwa na hakuna alichofanya. Sasa hawa waliyomchukua mtu kama huyo hawakuona hayo matatizo yake?

Membe kaja upinzani ili apate nafasi ya kugombea urais tu baada ya kutimuliwa huko ccm,sasa anaanzaje kumuachia mtu mwengine?si asingegombea toka mwanzo?

Hapa wanasiasa ndio wanatuona sie hatuna akili.
 
Usiku wa leo nimeota kuwa hapa kwetu yatatokea Kama yale yaliyotokea DRC, yaani was halisi wanapambana na hatimaye kushinda uchaguzi, mazungumzo yanafanyika na hatimaye anatangazwa mpinzani dhaifu na anakabidhiwa nchi 😩😩😩☹️☹️☹️
I've written earlier about this watu wanaona ndoto 😁.
 
Back
Top Bottom