Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Hivi Membe anachohangaikia ni nini hasa,si achane na siasa aendelee na shuhuli zake.Hamuoni Pinda alivyotulia? It's safer and comfortable that way na ataheshimika zaidi kwenye jamii kuliko kuendeleza malumbano na Serikali na Chama, ambayo hayatakuwa na matokeo mazuri kwake binafsi na familia yake.

Membe ni lazima sasa atambue kwamba kwa jinsi alivyokivuruga Chama na Serikali, hawezi tena kuwa sehemu ya siasa za Tanzania. He has simply messed himself so much.

By the way,did Membe really believe CCM would allow him to run in the next presidential elections under the present circumstances?Very naive indeed.
 
Niguse ninukeee!. Niko hapa katikati ya jiji naangaza pua yangu sijasikia harufu bado.

AMEKATWAAA..Ulisikika huu msemo mnamo july 2015.

Membe apumzike tu aache kutembelea maneno ya wafuasi wake uchwara.
 
Zitto alikuwa anatumika kuisambaratisha Chadema na ndiyo maana lile kundi lake lote na wenyewe wamemsaliti wapo CCM.

Yani Zitto aliwekwa mtu kati akiamini ana wafuasi kumbe na wenyewe ni mamluki part B. Huyu Membe anataka kuokoa hali ya nchi na wapo watu serious nyuma yake.
Huyu Membe alitaka kuharibu CCM wamemuindoa je kuna kosa?[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kichaa anayeweza kulazimisha kugombea wakati CCM ndiyo inayokupitisha! CCM ikikataa atagombeaje?
Sio ukichaa, ni uhuru na haki ya mwanachama yeyote kugombea. Pengine hukumsoma hapo, kaeleza wazi wamwache agombee ila katika mchakato walikate jina lake, kwa kuwa uwezo huo wanao.
Ila uoga wa kuona mwenyekiti ana upinzani wa ndani, ambayo ni aibu, imewafanya wamtimue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyekiti na genge lake ndio ccm? Amesema fika kuwa angechukua fomu ili agombee lakini mwenyekiti na rais wa sasa hana sifa za kushindana. Tabia hiyo iko wazi hata kwenye uchaguzi wa nchi nzima, ambapo mwenyekiti wa ccm anatumia madaraka yake ya urais kuchezea box la kura.
Ukiamua kukabidhi akili zako wenzako wakushikie na kukukaririsha kitu cha kufikiri na kusema una tabu tubu. Hizo fomu za uchaguzi za kuomba kuteuliwa na CCM ni nani anazitoa? Ni nani anazipokea wakati wa kurudisha?
 
Nayeye kama ana nia yakugombrea Urais siaende chama chochote? Kwani mpaka CCM?
Lengo ni kugombea na kushinda,na anaamini hivyo kupitia ccm kuwa ushindi kwake upo. Hana ndoto za kushiriki Kama wafanyavyo wakina LIPUMBA.
 
BM kama kirusi cha corona tu, dunia nzima ina watu bilioni 7+, walio athirika na ugonjwa huo jumla kwa nchi zote 195 hawafiki laki 5 ila kila ukifungulia radio, tv. Social networks issue ni Corona tu!

BM hawezi fukuzwa CCM kwa sababu ya kutaka kugombea urais kupitia tiketi ya CCM kwa hoja milioni

1. Nani anayempitisha mgombea wa CCM?

2. Katiba ya CCM inazungumziaje Mwanachama anayetaka kugombea nafasi ya urais kabla ya rais aliyepo madarakani kutumiza miaka 10?

3. Nguvu aliyokua nayo Endward Ngoyai Lowassa 2015 inakaribiana na hata chembe ya nguvu aliyonayo BM ndani ya chama?

4. Je, nguvu na nafasi ya Edward Ngoyai Lowassa katika Serikali inakaribiana hata kwa mbali na aluchowahi kuwa nacho BM

5.CCM wanaijua siasa kuliko chama chochote nchini! Unadhani hawajafanya tathmini ya hasara na madhara yake kabla ya kumtimua chamani?

BM anatafuta pa kutokea na ndio maana specifically akaamua kumpaka Mwenyekiti na Katibu nnya, kupata mileage na kujenga hiruma kwa wapinzani wa JPM kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya Chadema chombo hicho. Kazi na bata. Chadema nendeni na Membe 2020!
Hata Membe mwenyewe Hana mpango wa kwenda huko hata kama amefukuzwa ndani ya chama chake,mtabanana hukohuko mminyane mpaka kieleweke.
 
Zitto alikuwa anatumika kuisambaratisha Chadema na ndiyo maana lile kundi lake lote na wenyewe wamemsaliti wapo CCM.

Yani Zitto aliwekwa mtu kati akiamini ana wafuasi kumbe na wenyewe ni mamluki part B. Huyu Membe anataka kuokoa hali ya nchi na wapo watu serious nyuma yake.
Mkuu haujafanya utafiti wa kutosha.

Membe aokoe nchi gani na aina gani ya wokovu anaotegemea kuufanya zaidi ya tumbo lake binafsi?

Na hao wengi unaosema wapo nyuma yake ni 'image' zisizo na kiwiliwili, hawapo na kwa hili kabakia peke yake.

Kumbe hauwaelewi wanamtandao maslahi wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cherenganya,
Hayo maswali unamuuliza Nani kwa mfano. Ungekuwa mjuzi wa mambo ungekuja na majibu ya hayo maswali kwakuwa ndio maswali yetu watanzania na kwa hakika majibu tunayo. Unachokifanya no kutaka kutuaminisha upuuzi na kuuficha ukweli.
 
Kumbe unaipenda na kuijali sana CCM eeh?

Naona umeumia sana Membe kufukuzwa 🤣
Kwani kuitaja katiba ya Chama ni kuipenda? Mkuu Mbona unakosa uelewa kiasi hiki!!! Wengi tunafuatilia mjadala huu hivyo kuwa makini Upstairs.
 
Back
Top Bottom