Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Ukwaju, Mnajitekenya mnacheka wenyewe, achana na habari ya kutisha tisha watu Kwa kigezo cha kuwa na bundukk, mtaondoka mtaziacha hizo bunduki, huwezi kutawala Kwa amani Kama unatawala Kwa kutumia bunduki, angalia msiba yuko wapi?

Ameishaaga ameenda kulaala ni baada ya kugusa wababe wenzao, mtaishi Kwa hofu hadi lini? Huwezi jua kesho itakuchaje, unaweza kujikuta hali inabadilika mnaahangaika huku na kule hata huyo magufuli anajua kuwa alipata urais Kwa Bahati? Nani alijua kuwa magufuli atakuwa rais?

Hata membe laweza kutokea akawa rais chunga midomo yenu, msifikiri kuwa bunduki inaweza kila kitu, mnaweza kujiona kuwa mnawaweza wa Tz akatokea gafla mbabe zaid yenu mkapigwa mweleka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungejikalia kimya ushakosa ulaji 2015 tulia ule makombo kama ukuiendelea na makombo utayasikilizia sege
 
Kuna process yoyote ya kichama imerukwa mumfukuza uanachama? Process zote zimefuatwa ametendewa Haki tofauti hata na Lowassa ambae process gazikufuatwa na ndio maana lilalamikia process.

Membe halalamikii process Kwani zimefuatwa kikamilifu wenye chama wamemfukuza kwa mujibu wa taratibu na tamaduni za Chama chao.
So ndiyo wamkatae kwa process za kichama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika umenena aisee, wasijefanya makosa haya tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie mtakuwa ni Ccm, makosa yapi mnayoyasema? Kwani hao akina lowasa hivi kurudi CCM kuna kitu chadema walipungukiwa?

Kinachojulikana Nikuwa lowasa alipoenda chadema, ndipo chadema ilipata wapiga kura wengi tangu vyama vianzishwe, na ndio maaana ikapata wabunge wengi na madiwani wengi, sasa sijajua hoja yenu kuwa wasije wakafanye kosa kumchukua membe, hivi nyie mko Sirius Au ni

Ccm mnajifanya chadema? Hivi kauli ya Mama suruhu kuwa Ccm tusifukuze tutapata taaabu Kama tuliyoipata 2015 mlimsikia vizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Membe akigombea kupitia CCM ndio atashinda kihalali? Ndio maana Membe anang'ang'ania CCM kwasababu hana ushawishi nnje ya Chama Dola.

Yeyote akigombea CCM atashinda kwa Lazima na Membe anajua hilo. Hata JPM asipopiga kampeni atashinda tu na hilo ninaweza kubet kwasababu niuhakika.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unamuogopesha au? Hivi unadhani kuwa kila mtu ni muoga? Unadhani kumtishia mtu ili aogope ndio suruhu? Kinachotakiwa ni kujiuliza kuwa Kwa nini huyo anaogopa kuingia ulingoni na wenzake? Kwa nini anaogopa hivyo? Mbona amekuwa muoga Sana? Tatizo ni nini? Kwa nini hajiamini? Je hiyo ndio suruhisho ya yeye kupita?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaogopwa kwa lipi? Ananguvu gani Membe yakuizidi CCM? Acha kupamba vitu visivyokuwepo. Kwamba ukikosea kwenye Chama uachwe ili uwe hauogopwi?

Basi sasa kafukuzwa Membe mwenye nguvu CCM haitafika mwezi ujao itakua imekufa maana anaeogopwa kafukuzwa hadi macheka aiseeee. Kwamba CCM inamtegemea yeyote zaidi ya vyombo vya dola?
Stuxnet,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF na Twitter Vimemponza.

Huyu mzee hakuna anayemzungumzia kwenye mijadala huko mitaani. Hakuna.

Mgombea wa mitandaoni na safari imeishia mitandaoni.
umeona mbali sana
 
Ngoja tuone atakavyopigania haki yake nje ya CCM.
 
Hili game tu,. Hassan mwalimu na mwalimu Hassan sawa tu. Wanataka kucheza mchezo kama ule WA Lowasa. Tofauti ni kwamba Lowasa alizuga anaondoka mwenyewe huyu anazuga amefukuzwa.
Kwakifupi hii ni movie tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo corona ikuangamize wewe na familia yako na wenzio wanaokuzunguka. Fanya kazi uinue uchumi wako na familia yako
 
stroke,
Ndugu mbona wakimbilia kujipa faraja. Hata Nelson Mandela alipohukumiwa kifungo cha maisha, wa aina zenu walishangilia sana MWISHO wake. Mpaka hata baadhi ya nduguze wa damu, wa karibu walimruka kimanga na kumshutumu kwa 'UJINGA' wake wa kujaribu kupambana na dola kubwa lenye maguvu.

Kinyume chake, Membe bado yu na nguvu na nafasi yake katika siasa bado ipo sana.Historia itamsafishia njia na kumwinua kwa ushujaa wake dhidi ya ukoloni wa WEUSI wenzetu.

Watz wengi hasa walioko HUKO kwenu wameishaathirika na uoga wa ubabe na vitisho hasa vya dola, wanaogopa kabisa kujiruhusu kufikiri, kutafakari na hata kuuangalia ukweli kwa mtazamo wa historia. Wengi HUKO.

wasomi na wasio wasomi siku hizi wanazidi kujivunia na kujisalimisha kwenye kwaya za mapambio kwa wakandamizaji wao ilimradi WAISHI. AMEN
 
ostrichegg,
Membe hawezi kwa namna yeyote kumkaribia Julius Malema, let alone Mandela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…