Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Mwamba wa pande za Kusi, mwanadiplomasia nguli Bernard Membe ameunguruma baada ya kutoswa na CC ya CCM.

Ngoma bado mbichi kabisa hii.

Kwa undani zaidi, jipatie nakala yako ya "The Citizen" hapo kesho Jumamosi 29 February.

View attachment 1372047,
Kwa akili zake fupi anajiona ana nguvu na ushawishi wa kisiasa kuropoka anayoropoka?? Ajielewi!
 
Akagombee urais kupitia Chadema, akatimize hiyo ndoto yake. Makamanda tayari wameshajitayarisha kumpigia deki barabara.
IMG-20200228-WA0007.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maadui wa adui yako ni rafiki zako. Wale wote walioumizwa na CCM watampigia Kura ya Siri.

Ngoja movie iendelee
Maybe........ila atakwama maana hana mvuto sana kisiasa labda kwenye social media......2015 EL hata alivyoenda cdm mtaani alikuwa na watu wanaomkubali....ila huyu naona threads tu hapa JF na twitter.....ngoja tuone nn mwisho wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkia hauna ubavu wa kumtikisa Ng'ombe


Hata Nyerere analijua hilo, Azimio la Arusha tulianza kufungia vitumbua Nyerere akiwa hai na hakuna alichofanya zaid ya Makelele tu!

Kidumu chama cha Mapinduzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mafumbo ya kihayawani kama haya hufumbiwa wajinga.

Tabia za kinafiki hata siku moja haziwezi kupumbaza watu walio na uelewa wa kinachofumbwa.

Hapo ulipo unamaumivu endelevu tokea awamu ya Mwalimu hadi kwenye hii hata kama hakuna ushabihiano wa aina yoyote kati ya awamu hizi.

Maumivu hayapati ahueni kwa kuwa mnafiki.
 
Huo ndio ukweli hakuna kingine. Watafute watu wote walioonyesha nia kugombea urais 2015 kupitia ccm, uangalie Magufuli alichowafanya.

Anza na Prof.Muhongo, kamuondoa Uwaziri kwa vijembe, nenda kwa Mwigulu, Nenda kwa makamba, haya Mtafute Mwandosya, na Sasa Benard Membe. Wote kawaharibia mbele za umma, akitaka kujitengenezea njia. na kisha huko mbele atatengeneza mtu wake.

Sasa Sijui ndio Doto James, Au Makonda?!
 
Back
Top Bottom