Membe ulisema ‘’NIGUSE NINUKE’’, Kwa sasa tunasubiri hiyo harufu uliyoahidi!

Membe ulisema ‘’NIGUSE NINUKE’’, Kwa sasa tunasubiri hiyo harufu uliyoahidi!

Harufu ikianza mtakuja hapa nakuanza kusema Membe sio Mzalendo mara msaliti auwawe na maneno meeeengi.

Tumuombe Mungu tu watu wawe na busara na hekima haya mambo yawe kimya tu maana mwisho wa siku wahanga ni sisi wananchi.
 
Kudukua maongezi ya wenzako ni ushamba,ujinga na kutojiamini!
Wakati wa Obama, Edward Snowden ambae alikuwa Jasusi wa NSA Marekani, alitoa tuhuma ambazo NSA haijakanusha mpaka sasa. Tuma zenyewe ni NSA kumdukua Chancellor wa Ujerumani Angela Markel.

Kwa muktadha huu, udukuzi ni jambo la muda mrefu kuliko tunavyodhania.

Wakuu wa taasisi kijasusi Marekani CIA John Brenan na Gen. James Clapper wa DNI wote walikuwa na ushahidi pasi mashaka kuwa Russia alidukua mfumo wa uchaguzi wa Democrats na mfumo wa uchaguzi 2016.

Ukitaka usidukuliwe, acha kabisa kutumia simu au computer. Ishi full analog, hapo utakuwa umejinasua na udukuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha Dogo bhana, nakumbuka jinsi Lema alivyompokonya Mwigamba Kompyuta na kuiba nyaraka huenda bado ulikuwa shule. Kimsingi Mleta hoja kaibua jambo zito ambalo linahitaji majibu na sio kejeli.
Mi nimesema kudukua maongezi ya watu ya chumbani ni ujinga,ushamba na kutojiamini!
 
Ng'wamapalala,
CCM ni ya ajabu, KWanini msitengeneze ushindani? Hii haina tofauti na watoto wagombanao mdogo zaidi akilia, mkubwa anashikwa mikono na miguu huku wakimuita mdogo aje alipize kisasi kwa kumpiga mkubwa aliyekabwa mikono na miguu.

Hili jambo si jema, CCM ingekuwa imekomaa, wangekuwa wanachukua cream ili iongoze, sio mnachagua mtu then mnaweka na mbeleko kisa under perfomance.
 
Freddie Matuja,
Kuna kitu hujaelewa,wenzetu wanadukua mawasiliano kwa sababu za kiusalama na hata siku moja huwezi kuwaona wanaweka hadharani!

Sasa huku bongo mtu anadukua na kuweka hadharani namna anavyosengenywa, ushamba wa hali ya juu!
 
Tusubili tuone but believe me siasa ni mchezo mchafu lolote linaweza kutokea kwa mtu yoyote na kwa muda wowote..
Mkuu;
Ninakubaliana kwa kiwango kikubwa na angalizo lako ila tukumbuke kuwa Membe alituahidi kuwa akiguswa ananuka!

Kwa sasa ni zamu ya Membe kunuka baada ya upande wa pili kuamua siyo kumgusa tu bali pia kumtupa nje ya CCM!
 
Back
Top Bottom