“Tatizo ni urais. Wala wasipindishepindishe. Mara oh maadili, eti sijui fanya nini. Shida kubwa ni urais,” - Bernard Membe.
#Note 😂😂🤣🤣Membe bwana, ndiyo hujakosea hata sisi tunajua tatizo ni kuutaka Urais mpaka unakiuka maadili ya chama, maana urafi wa urais ndiyo unamfanya mtu abadilike tabia kama wewe, aanze hujuma za chini chini kama wewe, aanze kusema hajakumbukwa kama wewe, aanze kusema Rais wa nchi amechanganyikiwa kama wewe, aanze kudhani yeye ndiye alitakiwa kuwa Rais na siyo mtu mwingine yeyote kama wewe, ndiyo huenda tamaa ya urais ndiyo imekubadili tabia na kukuponza, hata 2015 ulionywa na siyo mara ya kwanza kukiuka maadili.
Ndiyo, ugonjwa wa watu wanaoutafuta urais kwa gharama huwa ni ugonjwa wa ajabu sana, labda nikuulize Membe, kwani 2015 ulipohojiwa na kamati hiyo hiyo ya maadili wakati huo Kinana akiwa katibu mkuu na Mangula huyo huyo akiwa makamu mwenyekiti na ukapatikana na hatia kwa tuhuma zilizokuwa zinakukabili TATIZO LILIKUWA NI NINI kama siyo URAIS ??
Watanzania na wanaCCM wangekuwa hawakusikiliza ile rekodi ya sauti iliyovuja ungeweza kuwahadaa kwa jinsi unavyojitetea leo, lakini sasa hivi kila mtu anajua mbivu na mbichi. Hakuna anayekuzuia kugombea urais bali chama kinalinda maadili na kanuni za chama kwa maslahi ya nidhamu ya chama, kwahiyo ulitakiwa kuwa na ndoto ya urais bila kukiuka miiko na maadili ya chama.