Meneja Huduma za Utangazaji kutoka TCRA, Inj. Andrew Kisaka, amesema asilimia kubwa ya Waandishi wa Habari hawajui kusoma tarakimu hasa wakiandikiwa ili wasome, kwani wamezoea maneno isipokuwa tarakimu za laki kwani ndizo wanacheza nazo kila wakati, hivyo hivyo ameiomba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, kutumia maneno zaidi ,ili wananchi wasije pewa matokeo tofauti wakati wa uchaguzi.
Inj.Kisaka anaeleza haya katika mkutano wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi na waandishi wa Habari ,kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Chanzo: ITV