TANZIA Meneja wa TANROADS Mkoa wa DSM, Mhandisi Ngusa Julius afariki dunia

TANZIA Meneja wa TANROADS Mkoa wa DSM, Mhandisi Ngusa Julius afariki dunia

Duu! Kwani huu ni msimu wa watu wakubwa serikalini kufariki🤦🤦
 
Ikipiga hodi kwako ikakuta kuna presha, kisukari,au kinga yako ipo kwenye mapambano na virusi vingine bas hapo kuuteka mwili wako hata siku mbili haziishi.

Ili uweze kuhimili vita hii vikute jeshi la kinga zako halijapambana muda mrefu.
Kwa hiyo unaweza kupona bila kwenda hospitali mkuu?
 
Kigogo kule twitter alisema Cooona inapendelea kufyeka watu wenye mafuta mafuta.
 
Utamaduni una nguvu kuliko kisomo.

RIP.

Poleni.
Kwenye maziko mbalimbali ya watu wanaokufa kwa Corona pia kuna misongamano ya kufa mtu halafu anaibuka punguani fulani anasema kuwa serekali haina wajibu wowote katika kuzuia kusambaa kwa Corona wajibu ni wa kila mtu kujikinga individually!
 
Samahani lakini.. huyu si ndio alisimamia kuvunjwa kwa nyumba kule Kimara? ambapo watu wengi walipoteza maisha kwa presha na mfadhaiko..Mungu amuweke panapostahiki yake kwa maisha aliyoishi duniani
 
Namfahamu huyu mpendwa na kwao ni hapa karibu na NENGELO OIL

Naona familia wamekusanyika wapo kwenye maandalizi ya msiba

Pumzika kwa amani mpendwa wetu
 
Na hapo si ajabu wengine wakaambukizwa.
Kabisa mkuu maana kwa ninavyoona hapa watu kutoka vijijini na mjini wanakuja

Na wale wataoleta/sindikiza mwili wa marehemu kutoka huko alikofia watachanganyikana na hawa...
 
Kabisa mkuu maana kwa ninavyoona hapa watu kutoka vijijini na mjini wanakuja

Na wale wataoleta/sindikiza mwili wa marehemu kutoka huko alikofia watachanganyikana na hawa...
Ngoma yetu ngumu.

Huvi hawa wanaojichanganya bila ulazima wanakuwa hawaelewi kuhusu maambukizi au wana suicide mission ndogondogo tu?
 
Kwahiyo hapo kuna mtu anapandishwa cheo kucover nafasi yake, sivyo?

R.I.P
 
Acha kujidanganya ,nafanya kazi kwenye hospitali kubwa sana hapa nchini watu wanakufa,mabinti wadogo wala siyo hivyo unavyodhani ww
Kwa uzembe mulionao ktk hospitali zetu hakuna atakayepona. Hospitali ambazo hakuna hata mitungi ya oksijeni! Mukiulizwa eti mahitaji ni makubwa, hamkujua? Kwa wanaotimiza wajibu, watoto na vijana hawaathiriki kiasi hicho.
 
Dar es salaam.
Kwa kweli hata oxygen cylinders kwenye hiyo hospitali hazitoshi tunalazimika mara nyingine kwenda kupokonya kule wadi ya watoto.
Mbaya sana.
Hakika hili ni janga na kiuhalisia tulitakiwa kuomba msaada ila sasa tumeshupaza shingo
 
Back
Top Bottom