Menina aishtaki DSTV, adai shilingi za kitanzania bilioni 1.2

Menina aishtaki DSTV, adai shilingi za kitanzania bilioni 1.2

Akipata mwanasheria mzuri anashinda kesi hii. Haya ma vipindi mengine ya umbea umbea ni ya kijinga sana
Hawezi shinda kesi ya kipuuzi kama hii hata siku 1,unajua mahakama itakupa kulingana na value yako,ktk maisha yake hata 50milion tuuu haijui inafananaje,akidai bilioni kama fidia inatakiwa atuletee na auditing report ya miaka 3 iliyopita inayoonesha alipata fedha kama hizo kwa kipindi hicho au zaidi ya hizo ili iwe justification ya claim zake na tuone alizilipia kodi.

Pili,yeye siyo daktari wala mwanasaikolojia amejuaje athari hizo zitaisha baada ya miaka 3?? Na kwa hiyo miaka 3 anayokadiria atakua kaathirika nani atathibitisha kuathiruka kwake kulitokana na kipindi cha umbeya kilichorushwa na dstv ili aweze kustahili malipo??

Mwisho akibanwa vizuri atatakiwa kusema na ile kideo yake na mwijaku ilimuathiri kwa miaka mingapi na alilipwa bilioni ngapi
 
Sheria ya urushaji wa matangazo kwenye tv,kwanza wanatakiwa wabalansi maelezo kwa kusikiliza pande zote mbili,kama waliishia tu kuwahoji majirani na yeye hakuojiwa basi anaweza fungua kesi na akashinda kesi kwani wamemdhalilisha kiutu.....Uwezekano wa kushinda upo ila apate mwanasheria mzuri mfano wakili kibatala
Ana pesa gani ya kumlipa Kibatala? Hivi unajua kuna mawakili ambao matumizi yake ya siku tu ya kusimama mahakamani anaweza akakutwanga million 4? Mafuta, Chakula sijui na wapambe wake! Huyo Menina hizo hela za kumkodi wakili wa aina hio anazo?
 
Kwani mimi nimesema washtakiwa waandishi /watangazaji wa chombo husika? La hasha. Hapa tunaongelea chombo husika au aliyenukuluwa ndio ashtakiwe?
Kwa muktadha huo, hiyo habari kama ilikuwa inawaailishwa kilichosemwa na mtu, mfano Mugufuli aseme chanjo haifai, na hilo gazeti liliripoti alichokisema Magufuli kama kilivyo, bila kuunga mkono wala kupinga. Halafu kampuni za chanjo zipate hasara, atashtakiwa Magufuli aliyetoa hio kauli na kunukuliwa na gazeti? Au watashtaki Gazeti? Hiyo ndio arguement, usichanganye madesa.
Mimi naona watashitakiwa wote. Mmoja kasema na mwongine kasambaza kilichosemwa. Wote ni wahusika. Asingesema msemaji yasingesambaa na asingesambaza msambazaji pengine atheri isingekua kubwa. Tunaangalia matokeo ya tendo lako kwenye kuathiri jambo na si vinginevyo
 
Menina atashinda hii case. Kama DStv wangekua makini kihivyo kama mnavyoamini wasingerusha hicho kipindi. Watachotwa tu this time, kama Ray kihosi alivyowachota 100millions
Ray aliwapiga 100m kumbe!? Huyo Menina labda amtumie Msando tu
 
Inawezekana wewe ndio haufikiri sawa sawa. Kilichomletea madhara ni DSTV kuruhusu umbea huo kutangazwa. Hao majirani umbea wao pengine hata tusingeujua
Na majirani walifatwa kuhojiwa, na inawezekana walitengenezwa sio majirani, DStv waliruhusu maudhui ya kumchagua menina yarushwe kwenye decorder zao ambazo Zina watizamaji wengi. Imemuathiri. Pia annawashtaki nna kina Mai na wenzie
 
Ameangalia wapi atapata huo Mpunga. Ameona hao Majirani zake hata akiwauza wao na Mali zao hamna kitu ataambulia
Unaweza Kuta wale sio majirani Bali ni watu walipangwa na kina maimatha. Sasa mahakaman utaona kama kina Mai wataweza kiwaleta kama mashaidi.
 
Ifike mahala sheria watu waielewe vizuri, sasa hapo dstv wamefanya nini? Wahusika si wapo?

Hakuna cha mwanasheria mzuri kashitaki mtu/ taasisi/ kampuni ambayo sio sahihi.

Sidhani wakili smbae ni msoni anaweza mshauri huu ujinga.

Nadhani anateja atakapopata pesa ila akumbuke nao wanaijua sheria so ajiandae
Atapigwa na ma bush lawyers tu ambao wanajua kesi haiendi popote ila watagawan a hela tu
 
Liabilities zina mipaka, Kwa mantiki hiyo hata Tanesco walio-supply umeme washtakiwe? Maana ndio waliosuoply umeme TV za nchi nzima watu wakaona, kwanini Tanesco hawakukata umeme? Liabilities zina mipaka. Kufikisha taarifa (hata umbea ni taarifa) kwa mtu mwenye leseni si kosa, na hajakiuka masharti ya leseni kurusha hiyo taarifa. Kama alipigiwa simu ili kubalance story na muhusika akagoma kutoa ushirikiano kwa sababu anazojua yeye, leseni inamruhusixkuirusha hiyo taarifa, na baadae inakuwa ni jukumu lake huyo mhusika kukanusha au kuikubali hiyo taarifa. Kama kilichorushwa then kimemchafua, kilichomchafua ni maneno ya majirani, na majirani wanafahamika, akawashtaki hao.
Vipi kama wale ni majirani wa kutengenezwa?? Kama ni majirani wataletwa mahakaman kama mashaidi naa upande wa DStv
 
Sh 100,000,000 ni pesa ndogo sana kununua nyumba America. Hiyo pesa ni sawa $49, 000- 52,000 pesa ambayo ni kiduchu saana. Hata bed seat hupati. Labda alinunua nchini Haiti.
Nyumba alinunua ya worth 800,000,000 za kibongo ambayo kwa haraka ni equivalent na kama $300,000+ hivi sasa useme hio pesa hainunui nyumba tena!
 
Unamtukana mwenzio Malaya as if wewe ni mtakatifu Sana. Hao kina fa unaosema Wana Elimu kwani wao ndo walikua mawakili wa kesi?? Waliajiri wakili. Hata Menina ataajiri wakili. Na Kwa kesi za hivi wakili Wala haitaji umlipe, kesi ipo wazi hii, mtalioana pindi kesi ikiisha.

Halafu hao unaosema wasomi kina fa na Ay una taarifa Tigo wamekata rufaa na wameshinda na kina fa wanatakiwa kurudisha fedha zote??

Usikariri maisha mkuu
Labda kama wameshinda njaa, rufaa inakatwa kabla ya malipo na kesi kufungwa! Uliona wapi kesi imefungwa halafu inakatiwa rufaa tena 😂 acha undezi wewe!
Huyo Menina hana hela ya kumpa wakili msomi na hio kesi haiendi popote sababu mlalamikiwaji halisi ni juma lokole na wapuuzi wenziwe! Sio Dstv
 
Nafkiri TRA wamemsikia Menina na natarajia wanajiandaa kwenda kuangalia kama kwa miaka mitatu iliyopita pia amelipia kodi inayoendana na 1.2 Bil alizopata.
 
Mkuu yaani unaamini hawa wa South kwa uwekezaji mkubwa waliofanya itakuwa rahisi sana kula pesa yao? Mwanasheria yupi huyo mzuri atakula kirahisi pesa ya DSTV?
Hii nchi imejaa wajinga, utakua katibu mwenezi wao
 
Suala sio udogo wa kampuni au ukubwa, suala ni kuwashitaki Dstv badala ya kuwashitaki majirani, shida inaanzia hapo
kwann vyombo vya habari hua vinafungiwa na serikali na sio waandishi walio andika hizo habari?? Jipige kifua sema "mm n mjinga"

Hiyo habari n mali yao, na ukiisambaza ww watakushak umewaibia kazi yao , wao ndio wazalishaji na wao ndio wasambazaji

Lkn pia wao ndio wahariri
 
Back
Top Bottom