Menina aishtaki DSTV, adai shilingi za kitanzania bilioni 1.2

Mbona Musiba alivyoshtakiwa hakushtaki wachapishaji wa gazeti? ilikuwa ni lazima? kesi ikianza hao kina Juma lokole ndiyo watenda kuwaleta hao majirani kama mashahidi na source ya habai yao ambayo haikuwa balanced
By the way ushawahi kuona presentation ya kipindi chao, siyo kwamba wana report wanshadadia na hukumu wanatoa hapohapo
 
Dstv hadi wanarusha walijidhisha kuwa kilichosemwa na majirani ni ukweli?
Au wanarusha kila kitu hata mambo ya uongo
Dstv karusha kilichosemwa kama kilivyosemwa, hakujudge kusema kama ni kweli au la, hawakuunga mkono wala kubisha, bali walitoa taarifa kwamba majirani wanasema moja, mbili, tatu. Kazi ya kukanusha au kukubali ni yake yeye Menina; na pia kama anaona hao majirani wamemchafua basi awashtaki hao.
 
Akipata mwanasheria mzuri anashinda kesi hii. Haya ma vipindi mengine ya umbea umbea ni ya kijinga sana
Akina Juma Lokole na kundi lake huo sio uanahabari ni uharibifu sawa na Mange Kimambi, sijui kwanini maudhui hayo yanaruhusiwaje kurushwa.
 
Huyu mwanamke mpuuzi sana kwa hiyo kwa miaka mitatu ana uhakika wa kuingiza bilioni 1.2? Au ile kazi ya kukatikia muhogo? Ndio inaweza mpatia hiyo pesa embu tuwe serious.
 
Hayo yatajulikana mahakamani, haki itapatikana huko tusijifanye wanasheria hivi wewe ukiwa accused kumuua mzazi mwenzako na kipindi kikarushwa kwenye media kikaonekana east africa nzima utaenda ku dela na waliohojiwa?
Kulikuwa na ugumu gani hao watangazi wa hiko kipondi kianchoitwa CHUMA CHA UMBEYA kwenda kupata upande wa pili wa menina? nimeweka link hapo ya you tube ya hiko kipindi kiangalie halfu ujiweke kwenye viatu vya menina
 
Akina Juma Lokole na kundi lake huo sio uanahabari ni uharibifu sawa na Mange Kimambi, sijui kwanini maudhui hayo yanaruhusiwaje kurushwa.
Imagine watu wanashangilia kwamba Menina hana haki kulalamika ,jama wanavyotangaza wanashibedua na kuchochea kabisa kwamba Meninia kamuua mzazi mwenzake
 
Unajua ni kwanini Ruge alikataa kipindi cha shilawadu(kilichozaa hiyo ICU inayoleta shida) kisirushe ile clip kuhusu Gwajima kuzaa na mwanamke kichaa hadi bashite akakasirika na kuvamia clouds?
Ruge aliwaambia hawa kina Kwisa na soudy brown ni lazima wa balance kipindi kupata upande wa pili unasemaje ila hii Meninia kawa accused na majirani, na watangazaji nao wameunga humohumo wanamlaumu kwa mauaji leo mtu anapigania haki yake anabezwa,duh
 
Jamaa angu punguza kula kande la mawese,hicho kipindi hata Leo huko DSTV kimeonyeshwa na wambea wenzako walikua wanakiangalia hapa sebuleni.
 
Kwani gazeti likichapisha taarifa za uongo.
Anafungiwa mwandishi wa habari hiyo au gazeti
Kwani mimi nimesema washtakiwa waandishi /watangazaji wa chombo husika? La hasha. Hapa tunaongelea chombo husika au aliyenukuluwa ndio ashtakiwe?
Kwa muktadha huo, hiyo habari kama ilikuwa inawaailishwa kilichosemwa na mtu, mfano Mugufuli aseme chanjo haifai, na hilo gazeti liliripoti alichokisema Magufuli kama kilivyo, bila kuunga mkono wala kupinga. Halafu kampuni za chanjo zipate hasara, atashtakiwa Magufuli aliyetoa hio kauli na kunukuliwa na gazeti? Au watashtaki Gazeti? Hiyo ndio arguement, usichanganye madesa.
 
Jamaa angu punguza kula kande la mawese,hicho kipindi hata Leo huko DSTV kimeonyeshwa na wambea wenzako walikua wanakiangalia hapa sebuleni.
una hakika Dstv unajua ni nini ndugu yangu? we endelea kuangalia movie za Juma khan za kutafsiri kwenye mabanda ya kuku huko nanjilinji
 
Musiba ndio ameshtakiwa kwa kauli alizotoa yeye na kuzichapisha, sio kwa kuchapisha alichosema mtu mwingine, sasa mshtakiwa atashtaki nini tena wakati yeye ndiye mshatakiwa, arguement yako inakosa logical basis
 
Musiba ndio ameshtakiwa kwa kauli alizotoa yeye na kuzichapisha, sio kwa kuchapisha alichosema mtu mwingine, sasa mshtakiwa atashtaki nini tena wakati yeye ndiye mshatakiwa, arguement yako inakosa logical basis
Basi kumbe Bashite alikuwa na haki kuwavamia hawa kina kwisa pale clouds maana Ruge alikataa kipindi kiruke hadi gwajima ahojiwe ili story iwe balanced sijui kama kwenye hili menina alipewa haki ya kimsingi kusikilizwa na kuhijiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…