Mercedes benz yamjibu Tesla vibaya sana

Kweli Tesla wanatawala. Lakini tayari keshapara wapinzani. Tesla angekuwa mjanja angetoa magari yenye bei nafuu. Sasa hivi kia na Toyota wako mbiini kutoa magari ya umeme yenye bei nafuu ambayo hadi walala hoi akina Idugunde wataweza kumudu kununua.
hata hayo magari yanayotumia diesel na petrol pia yapo ya bei rahisi lakini. bado lambo porsche ferari cadilac Rr zinasumbua sokoni
 
Ngoja niwahi kabla hazijaisha....
najua dola laki moja + dola laki moja kodi
 
Jamaa ana maproject mengi sana.....
zikija toyota za umeme huku......
sheli zijiandae kufungwa
 

Wachina pamoja na hayo walitangulia kyikubali Tesla, sasa hivi ni trending car Ulaya pia
 
Iyo mkuu inakaribia million 300 hapo bado TRA yani hadi uitoe bandarini pamoja na tozo kibao uchwara million 700 huko.

Labda ukiamia Zambia unaweza ukaendesha na million 400
Bora niinunue then nikaitolee Kenya, nakua naiendesha nikiwa kule nikirudi nchini natumia vitz
 
Tesla ni iphone ya magari ko wewe tegemea kuona wakiendelea kusumbua sanaaaa kwa miaka mingi ijayo
 
Hii mashine ni balaa nimeangalia summary review yake juzi sio poa...then AMG(Pro Max) yake inakuja sasa unadhani itakuaje? Kitu Ant covid iyo yan Bacteria na Virus humo hawakai...[emoji91]
 
Yani unaambiwa ndo ilikuwa the most anticipated car of the year 2021. Mimi panaponiacha hoi ni mlango kufungua kwa kubonyeza funguo.
BMW za sasa unawasha gari na funguo pia ukiwa nje.
 
Haya magari inabidi ununue mapya...hakianza kuchoka yatakusumbua sana na hii tech yetu hii ndo shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…