Mere prediction about the future: Yajayo yanafurahisha, upo tayari?

Mkuu Ontario kaandika mambo ambayo baadhi yake nimewahi kuyasikia...hasa kwenye AI. Dunia inabadilika kwa kasi sana. Na inapobadilika ina athiri professions za watu lakini pia iatengeneza fursa mpya kwa watakao adapt mabadiliko hayo.

Pia ninashangazwa na kiwango cha chuki ambacho baadhi ya wachangiaji wanakionesha kwa Ontario. Nawaza kama kweli hawa watu wanafanya haya wakiwa na akili timamu...au ni chuki tu zisizo na msingi...?

Big up Ontario kwa kushare yale uyajuayo kuhusu kuhusu future ya teknolojia. The wise will understand, fools will despise.
 
Sijaleta chuki yoyote, na sina chuki na yoyote.

Mpe mwanao basi.


Tumezunguka wee. Mwenge, moroko, kinondoni, buguruni, tabata, n. K
Mwisho tunaishia kituo cha forex

Acha kudanganya watu
Hii inadhihirisha ni jinsi gani watanzania tuna wivu, chuki, kinyongo kuanzia kiongozi wa juu mpaka mtanzania wa chini.

Kijana kaleta uzi, badala mjadili mada mmeanza kumtupia maneno machafu!!

Sizani kama wenzetu wangeanza kumtusi kabla ya kufanya walau karisechi!!

Kama mnaona mada zimewazidi IQ ni bora mkae pembeni.

Huu wivu, chuki, visasi na vinyongo ndio vinaendelea kutuweka tulipo, watanzania tubadilike!!
 
KAKA
Amka hayo maelezo yote ni mbwembwe tu..
Kuna kitu huyu jamaa anataka kukisema atunishe mfuko. Lengo la post yake ni hii..

Blockchain ya kwanza duniani iliundwa na mtu mmoja asiyejulikana ama kundi la watu wasiojulikana anayetambulika kwa jina la Satoshi Nakamoto mwaka 2008, teknolojia hiyo ikaanza kutumika mwaka 2009 kwa product ijulikanayo kama Bitcoin.Juzi tumeona Bitcoin 1 ikiwa na thamani ya $20,000. Muda huu natype huu uzi tayari kuna zaidi ya cryptocurrencies 1300, kama nilivyosema awali, teknolojia ni kama radi, kamwe huwezi kuizui kwa mkono, hata kama hatuyataki haya mapinduzi bado yatatufikia tu.


Ninachoamini miaka kadhaa pesa itakuwa full digitalized na decentralised, hakutakuwa tena na hizi noti na sarafu bali tutakuwa na cryptocurrencies nyingi, tayari dunia ipo huko, lkn watu hawajaanza kuadapt mabadiliko, hapa ndio hua nasema only the fit will survive. Mzee baba Bill gates tumeona akitia mzigo kwenye crypto iitwayo Ethereum sawa na makampuni kama Itel, JP Morgan, Watu kama kina JohnMcafee na Mark Cuban wote wanatia mizigo yao huku. Kama mtu aliyesmart mwaka 2012 angenunua bitcoins 102 kwa $100 tu,leo hii mtu huyo huyo angekuwa na $1,667,000 kutoka $100. Hapa ndio inakuja ile, I wish, I could, I would, I should.


Mimi binafsi hivi vitu nimechelewa kuvijua, na wala sijilaumu na sasa nimetumia muda mwingi sana kuvifahamu kwa undani. Kama Jan 2017 mtu angewekeza $1000 kwa kila 1 ya top 7 cryptocurrency yani Bitcoin, Ethereum, Ripple, Litecoin, Monero, Dash na Neo leo hii mtu huyo angekua anavuna $1,156,000 kiutani utani tu. Mimi Sept mwak jana nilitumia $800 kununua ripple 8012, leo hii kila coin 1 ya ripple inathamani ya $3 na si ajabu by December mwaka huu coin 1 ya ripple ina thamani ya $100. Siku si nyingi sana nimeinvest $103 kwenye coin inaitwa mintchip nimenunua coins 100,050 ndani ya masaa machache nimeweza kutripple capital na hapa plans zangu niendelee kuhold hadi December ambapo labda coin 1 itakuwa na thamani ya $1 kwa hivyo investment yangu ya $100 itakuwa imeleta zaidi ya $100,000 kiutani utani.

Tumeona hii inawezekana baada ya ripple kutoka $0.0063 hadi $4 kuanzia Jan 2017-Jan 2018.Huku ndipo dunia ilipofikia. Muda huu unasoma hii thread fahamu kuwa Larsen Founder wa Coin ya Ripple ndio tajiri namba 5 duniani, kawaacha kina Mark Zuckerback wa FB na hata mafounder wa Google Larry Page and Sergey Brin. Mpk mwaka unaisha jamaa atakua anamtuma Bill Gates sokoni akamnunulie ugoro.
 
Simple sana mzee baba kufyatua nyumba kwa dakaka 2. Ngoja niingie fb nilikoiona ile clip then ntashare hapa japo inaweza kunichukua muda maana ni tangu mwaka juzi nimeiona ile clip kwa page ya American tech..

Alafu hili LA mtu kutengenezwa maabala, mbona hatushangai kuku kutengenezwa maabala?
 
Hizi chuki,ubinafsi,wivu ndio zinatutofautisha sisi na wenzetu, huu uzi ungeanzishwa kwa wenzetu usingekuta comments za kijinga!!

Ila ndio hivyo tulivyo... Tatafanyaje sasa!!
 
Binafsi nashukuru nimepata elimu ya kunifungua na kuifahamu dunia kwa ujumla wake. Sisomi sana vitabu, articles ndio huwa nasoma kwa wingi. Pia kufanya kazi kwenye teknolojia kama mhandisi wa software kumeniweka karibu zaidi na mrengo wa dunia inakoelekea na kuelewa kwa mapana zaidi namna teknolojia inavyoibadilisha sunia na kuwa sehemu ndogo ya waleta mabadiliko hayo.

Japo kuna changamoto nyingi sana in practice kwa maono ya mtu kama Elon Musk kutimia, watu wanapambana usiku na mchana kutatua changamoto hizi.

Wanamwona chizi sasahivi, lakini wakati anaanza Tesla walimwona chizi vile vile.

Yule mazafaka ana kitu kinaitwa 'master plan' ya jinsi ya kuibadilisha dunia. Hatua kwa hatua, plan yake inaenda. Anajaribu kuifanya dunia iwe mahala pazuri zaidi pa kuishi, na siku dunia itakapokuwa si mahala panapofaa tena kwasababu ya 'great environmental disaster' basi species ya binadamu iwe inaishi Mars na kuendeleza uzao.

Cryptocurrency na blockchain zinasimangwa na finance investors kwasababu hazina any tangible value zaidi ya matarajio ya watu kuwa thamani itapanda. Lakini zipo platforms kama Ethereum ambazo ni zaidi ya cryptocurrency yake, Ether. December mwaka jana Ether ilikuwa 300$ leo nk 1141$. Kila siku naiona value yake ikipanda mbele ya macho yangu at coinmarketcap.com

Mwenda bure si mkaa bure. Hata kama sitawekeza pesa yangu huko, hata kama sitafaidika kifedha, naamini knowledge ninayoiokoteza ipo siku itaprove beneficial. I have the upper hand due to the power of knowledge.
 
USISUMBUE AKILI YAKO NA MANENO YA KUAMBIWA KITU FLANI KINALIPA

MFANO

Ukipata nafasi ya kufika kule Mbozi, Mbeya ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na kilimo cha kahawa, kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga, Njombe na kufuatilia stori na kutazama na milionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Iringa kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira kama ulikuwa mwajiriwa.

Ukitoka pale ukaenda mpaka Mang'ula na Ifakara Morogoro, ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye mpunga, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku, zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi kariakoo, Dsm kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule China, Uingereza na Dubai. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!

Usiende kwanza Zanzibar, bali chukua hata bus au Fastjet uende chapchap kule Arusha. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. Ukisimuliwa ABC za madini na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!

Unapoendelea kutafakari, rudi mtandaoni. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa Network Marketing utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, usiombe ukutane na fursa ya digital currency, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua. Na huku ndiko Ontario anapowapeleka mark my words

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale tunaokinadi kilimo kama dhahabu inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:


1.Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya network
marketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwenye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika network marketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja
Fursa zipo nyingi kuwa makini katika maamuzi.
 
Powerful thread! Thanks alot. Huwa natabasamu tu ninapoona mtu hatambui mchango wako katika fursa adhimu zote ulizotuletea. Huwa najilaumu kidogo kuchelewa kukufuatilia. Huwezi amini leo hii sina mpango kabisa wa kuajiliwa tangu nilipoanza kuadapt fursa ulizotufungua. Usikate tamaa matunda ya fursa na juhudi zako nimeanza kuyaona na kuyaishi. Mungu atakubaliki zaidi ukiendelea na moyo huohuo.
 
Heko, si mchezo. Je, Mungu atasubiri wafike huko? Ujio wa kristo na mpinga kristo utakuwa haujatokea?
 
Mr. Mangi Kuna mtu aliyeongea maswala ya kulipa au kutokulipa kwenye huu uzi??

Kwanza umeisoma mada ukaielewa au umepost tu??
 
mkuu ONTARIO naomba ufafnuzi hapo kwenye technology ya 3D printing,hasa uliposema kuwa huko china kuna ghorofa la ngazi 5 limejengwa kwa siku 17 na kuhusu hilo gari la ku-print linafanya kazi au ni gari la pambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…