Sijui kama nipo sahihi kama nikitafsiri directly kama 'Akili ya kutengeneza', ni akili iliyounganishwa katika mashine ili kuweza kumsaidia binadamu baadhi ya shughuli, akili hii inaweza kufanya reasoning, problem solving, kujifunza nk.
Artificial Intelligence (AI)
Hili ni moja kati ya masuala ambayo huwa yananifanya niwaze sana kuhusu future hasa ukizingatia kiu ya muda mrefu ya wanasayansi kudevelop "superintelligence" na wengi wanaamini kwamba maendeleo ya AI yanaweza kutufikisha kwenye 'superintelligence'. Mfano mzuri ni programu ya Fritz ambayo umeitolea mfano hapa kwenye uzi.
Itakuwaje kama maendeleo ya AI yakitufikisha huko, kuwa na superintelligemce (system au program yenye akili zaidi kuzidi binadamu mwenye akili kuzidi wote)? Inaweza kuwa ni gunduzi muhimu zaidi kuwahi kutokea kwenye historia lakini pia inaweza kuwa ni gunduzi hatari zaidi kuwahi kutokea kama itatumila vibaya.
Hapa chini nimejaribu kutoa mfano mdogo wa namna ambavyo AI inakuwa kwa kasi mno. Nimekuwa nafuatilia hiki kitu kwa miezi kadhaa sasa.
Sophia: Humanoid Robot
Binafsi nadhani hii ni moja kati ya sekta ambayo inakua kwa kasi mno na muda mwingine ukitazama hatua za kisekta zibazopigwa unaweza kuogopa.
Uwezo wa robots ku-utilize Artificial Intelligence umekuwa mkubwa kiasi kwamba ndani ya miaka 10 au ishirini ijayo kwa hakika tunaweza kuwa na robits ambazo ziko developed kwa kiwango ambacho kinaweza kufanana kabisa na akili ya mwanadamu au pungufu kiduchu tu.
Mfano mzuri ni Robot anayejulikana kwa jina la "Sophia" ambaye ametengenezwa na kampuni ya Hanson Robotics.
Sophia ni aina ya Robots ambao ni 'Humanoid', kwa maana ya kuwa na mfanano mkubwa na muenekano wa binadamu.
Katika kumuunda Sophia, kampuni ya Hanson Robotics wametumia aina maalumu ya sponji ambayo wanaiita Frubber (flesh rubber) ambayo inafanana kabisa na muonekano wa ngozi ya binadamu. Na si kufanana muonekano tu bali pia, hisia na elasticity ni sawa kabisa na ngozi ya binadamu.
Aina hii maalumu ya material wanayotumia imewawezesha kumfanya Sophia kuweza kuwa na 'facial expressions' kama vile kutabasamu, kukunja uso kwa hasira, kushangaa na kadhalika.
Sophia ameundwa katika namna kadhaa adhimu za kiteknolojia…
Kwa mfano, katika macho yake amewekewa Kamera maalumu ambazo zinafanya kazi pamoja na algorithms ambazo zinamuwezesha kuona, kukumbuka kile ambacho amewahi kukiona, kufuatilia uso wa mtu ambaye anaongea naye na kufanya eye contact.
Sophia pia ameundwa na teknolojia yenye kufanana kwa kiasi fulani na 'Alphabet Google Chrome Voice Recognition Technology' lakini iliyo developed zaidi.
Teknolojia hii pamoja na uwezo wa AI ambao uko installed ndani ya Sophia unamfanya awe na uwezo wa kutambua kile ambacho mtu anazungumza na kisha kujibu kwa ufasaha kabisa kile ambacho anaulizwa au kinachohusu mazungumzo hayo.
Huu ni moja ya mifano michache sana kudhihirisha namna gani ambavyo AI inakua kwa kasi na katika kiwango cha kutisha.
Miaka kadhaa ijayo Robots kama Sophia wanaweza kufanya kazi ambazo leo hii zinafanya na binadamu kama vile kazi zihusuzo Huduma kwa wateja (customer services), therapy na hata katika sekta ya elimu.
Kuna makampuni mengi ambayo yanashindana kwa kasi ya ajabu kuleta aina ya robots au teknolojia ambazo zinarandana kabisa na uwezo wa kufikiri wa binadamu.
Kwa mfano licha ya umahiri wa Robot Sophia bado kampuni ya Hanson Robotics wanakuna vichwa kwenye labs zao ili kumfanya Sophia kuwa 'intelligent' zaidi kwa maana ya kumfanya awe mwepesi, kuongeza kasi yake ya kuform logic na kuwa na accuracy ya hali ya juu ya maswali anayoulizwa na kutoa majibu lakini pia kumuongezea facial expressions na body languages.
Nchi ya Saudi Arabia imeridhishwa na umahiri huu wa Hanson Robotics na wameamua kumpatia Sophia Uraia wa nchi ya Saudi Arabia.
Lakimi pia umoja wa Mataifa wamempatia Sophia tuzo maalumu (kwa mara ya kwanza) ya UNDP Inovation Champion.
Kesho inakuja kwa haraka mno na muda mwingine inaogofya… na kadiri ambavyo tutajiandaa ndivyo ambavyo tunajijengea ufanisi wa kukabiliana nayo na kunufaika nayo.
(Unaweza tazama hapa chini mahojiano mubashara ya Sophia na mwandishi Andrew Ross Sorkins wa CNBC ya Marekani)
The Bold
To Infinity and Beyond