Kwa uchungu mkubwa inabidi nikiri na niseme wazi kuwa Lowassa was right aliposema kuwa suala la Meremeta ni la Usalama wa Taifa. Hata Pinda naye alipotoa kauli hiyo, alikuwa sawa kuwa ni sualala Usalama wa Taifa.
Lakini tunapozungumzia Usalama wa Taifa, je tunalipokea vipi na kufikiri linamaanisha nini?
Mwanzoni nilihoji, kwa nini Jeshi lipewe fedha uvunguni? Je kulikuwa na Covert Operation? Lakini kadri siku zinavyoendelea na nikendelea kuunganisha nukta zangu mithili ya Buibui kujenga utando wake, ndipo taswira halisi ya kilichotokea na maana ya maneno ya Mawaziri Wakuu wawili kuwa hili ni suala la Usalama wa Taifa.
Ni uamuzi wako kutafakari kwa kina nitakachokisema hapa chini na kama umesoma ile makala yangu ya "Tumeuza Uhuru wetu"
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/35092-tumeuza-uhuru-wetu-na-hazina-yetu-tumeifuja.html utaelewa ninachokizungumza hapa.
Suala la Meremeta si suala la wizi wa kujitajirisha kama EPA au kutumia fedha kwa uchaguzi kama Kagoda.
Suala la Meremeta kwangu ni Uhuru wetu kuwekwa rehani!
Swali ni hili, je viongozi wetu walifanya nini mpaka wakashikwa kende na kulazimishwa kufuja rasilimali zetu na kuwaruhusu Mamluki wafanye kazi Tanzania tena kwa mkataba na serikali yetu?
Kwa nini viongozi wote husika anzia Rais, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama waTaifa na wenginewe hawakutumikia viapo vyao vya utii kwa katiba na kuilinda Tanzania kutoka kwa maadui wa ndani na wa nje? Walifanya nini wakaasi viapo vyao na kuidhalilisha Katiba yetu?
Ni Woga gani ambao alikuwa nao Mkapa, Mboma, Apson na wengine mpaka wakakubali kumruhusu Viktor Bout, EO na wahuni wengine kujifanyia wanalotaka kwa baraka za viongozi wetu?
Ni maslahi gani waliyokuwa wakiyalinda na hata kuhakikisha kuwa mkono wetu unatumika kwa mhuri wa Ikulu kuruhusu vurugu za Kongo na Rwanda?
Je tulipokuwa tunasamehewa mikopo na Paris Club huku Waingereza na Tony Blair wakitusifu, ilikuwa ni takrima waliyopewa viongozi wetu ili kutupumbaza sisi wananchi tusijue kilichotendeka na kinachoendelea?
Ni kwa nini tumeuuza uhuru wetu na kukubali hazina yetu ichukuliwe kirahisi na tunadanganywa kuwa ni suala la Usalama wa Taifa?
Je ni suala la Usalama wa Taifa kwa kuwa tukikataa kutii matakwa ya EO, Blair na wengine, watahakikisha kilichotokea Rwanda na Congo kinatokea Tanzania?
Je ni suala la Usalama wa Taifa kwa kuwa tukijua ukweli kuwa udhaifu, uroho na tamaa za Uongozi wa Awamu ya Tatu (serikali kuu na vyombo vya Ulinzi na Usalama), basi ile aibu na hasira ya vitendo vya waliotoa rehani Uhuru na Hazina yetu zitazaa hasira na rabsha ndani ya nchi na hivyo kuvunja ile Amani, Mshimkamano na Utulivu?
Cha mwisho ninachoojiuliza, haya yote yamefanyika kwa manufaa ya nani?
Je ndio tumerudi kutawaliwa upya kwa hiari tukiwa na bendera yetu, lakini Hati ya Uhuru tuliyopewa usiku ule wa Disemba 9 1961 pale uwanja wa Taifa tumetishiwa kunyang'anywa kwa nguvu na hivyo tukaisalimisha kwa hiari ili kuficha aibu?
Ningekuwa mimi, ama ningejiuzulu kazi ili nisiliingize Taifa langu kwenye giza na mkasa kama huu na kama hiyo blackmail ingekuwa ni kuzidi kitakachoeleweka, Mwenyezi Mungu angebidi anisamehe pale ambapo kujiuzulu ingekuwa ni tabu na aibu na hivyo kujipiga risasi ya kichwa!
Walichokifanya Watanzania wote waliohusika na Meremeta, iwe ni Rais, Wakuu wa Usalama, Mawaziri, Makatibu wakuu au nyadhifa zozote ni
UHAINI!