Meremeta Report: Released to the Public (Revised & Free!)

Meremeta Report: Released to the Public (Revised & Free!)

The Official report approved by NedBank Board of 29th January 2009 reveals alot on what we are discussing. It is worrying! The Country under threat, serious threat! I quote;

' That the three officials named as Directors of Deep Green Finance Ltd (Mark Ross Eston - New Zealand, Antony Taljaard and Rudolph Van Schalkwyk - South Africa) have no any connection to NedBank or our Business partners. The quick search has proved that these are International racketeers dealing with dubious transactions including arms trafficking as well as smugling of resources in various African Countries'

Deep Green agent in Tanzania is IMMMA Advocates. Partners of this company includes our Internal Affairs Minister.............!!!!!!!

I am digging more as NedBank are yet to denie its dealings on MEREMETA whose partners is named on the letter from IKULU to Deutsche Bank AG London (ie NEDCOR TRADE SERVICES LTD - 100% owned by NEDBANK according to its Annual Report of 2008 as approved by the Board on February 2009.

Ninaamini tunayoenda kuyajua ni ya hatari. Lakini ili tusafishe nchi ni lazima tuyajue............

Zitto, Sandton, Johannesburg, Republic of South Africa
 
Last edited:
Well, swali linakuja hata tukijua ndio itakuwa nini? Mbona EPA tunajua na viongozi wetu wameambiwa lakini jibu walilotoa ni kuwa wanajua wahalfu lakini wanawaogopa. Kama hawa wa Meremeta sio ndio itakuwa wanaongopa hata kusema?
 
Oops!!!! Thanks Hon.Zitto, i advice you mobilize your colleagues (MPs) and compile all important findings about these dirty deals (esp. Meremeta) and submit a private motion (agenda) in the next house sitting.
 
Hili ndio lengo haswa. MwanaKijiji ameni inspire sana kwa kweli. Kwamba yeye raia wa kawaida ameweza kutengeneza taarifa hii ambayo sisi wabunge kwa rasilimali tulizonazo tulishindwa kufanya. Nimeamua kumuunga mkono kwa vitendo na kwa kweli inalipa kweli maana taarifa mpya tulizopata ni shehena!

Fedha zetu zote zipo Mauritius..............................
Nedcor Trade Services Ltd - Mauritius

:: General Information :: Products/Services :: Related Organisations :: Contact Information

:: Update :: Upgrade
General Information

Organisation Type/Location: Company in Mauritius Registration No.: 20425/4243 Find Related: [ News Items | Pages | Companies or Organisations ]
:: Update :: Upgrade
Products/Services

There are currently no products or services associated with this directory entry.

:: Update :: Upgrade
Related Organisations

is owned by: Nedbank Group Limited - Sandton, Johannesburg, South Africa
is owned by: Women Investment Portfolio Holdings Ltd - Sandton, Johannesburg, South Africa

Hawa ndio wana siri zote za nani kapata nini? MwanaKijiji andaa Review ya pili...! Tutafikia ukweli tukiwa HAI, Inshaallah
 
Well, swali linakuja hata tukijua ndio itakuwa nini? Mbona EPA tunajua na viongozi wetu wameambiwa lakini jibu walilotoa ni kuwa wanajua wahalfu lakini wanawaogopa. Kama hawa wa Meremeta sio ndio itakuwa wanaongopa hata kusema?

EPA ni wizi wa kawaida wa Benki. MEREMETA ni wizi wa heshima ya Taifa letu. MEREMETA inaweza kuangusha serikali. MEREMETA inahusu Tanzania mbele ya jamii ya Kimataifa. MEREMETA undoes our history in the struggle for liberation in Africa. EPA is them, MEREMETA is US
 
Zitto.. unajua kuna info nyingi zinatiririka hadi inaoogopesha kwa kweli. Nashukuru kwa sababu taarifa ulizonazo zimeongeza sana kuelewa jinsi genge la wahalifu wa kimataifa wameweza kujipenyeza nchini mwetu kwa staili ya aina yake (uwekezaji).

Hilo la Mauritius mwanzoni sikutaka kulifuatilia sana lakini tumedokeza kidogo kwenye ripoti relevance ya anuani ya Tangold kule Mauritius. Anuani ile ile inatumiwa na makampuni lukuki ya offshores ambayo si yote yana sifa nzuri kwenye nchi zao.
 
EPA ni wizi wa kawaida wa Benki. MEREMETA ni wizi wa heshima ya Taifa letu. MEREMETA inaweza kuangusha serikali. MEREMETA inahusu Tanzania mbele ya jamii ya Kimataifa. MEREMETA undoes our history in the struggle for liberation in Africa. EPA is them, MEREMETA is US

Zitto this is the main reason kwanini ripoti tuliamua kuiandika kwa lugha yetu kwanza kwa sababu nina uhakika kama tungeitoa kwenye Kiingereza ingekuwa zaidi ni kwao. Ndio maana toka mwanzo tumekuwa tukiidokeza kwa vipande vipande ili kuwapa nafasi serikali to make a move to clear the name of our country.

Lakini kubwa ninaloamini ni kuwa hili ni suala la serikali ya CCM (CCM gvt) na siyo suala la nchi nzima. Jamii ya kimataifa haitaihukumu Tanzania nzima au wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya madudu ya serikali iliyoko madarakani. Hata Hitler na mambo yake yote alihukumiwa yeye na kundi lake la waliomuunga Mkono na siyo Ujerumani kama ujerumani au wananchi wa Ujerumani kama wananchi wa Ujerumani. It is the same principle imetumiwa hata kwa Wamarekani.

Mambo yaliyofanywa na kina Oliver North katika Iranian Contra au na kina Tim na Tony kwenye Arms to Africa Affairs yalihusu serikali ya Reagan na Tony Blair na siyo Wamarekani au Waingereza as such. Madudu yanayofanywa na watawala walioko madarakani ni wao pekee wanabebeshwa na sisi Wananchi tusijisikie hatia kwa sababu hiyo.

CCM na serikali yake imelea uozo huu, imeulinda, imeufunika na wakati mwingine kuupamba kwa maua huku wakirushia manukato; lakini ukweli umebakia kuwa ni uozo na sasa maua yameondolwa na mifuniko imezibuliwa. Tunaouna uchafu kwa rangi yake ya asili na harufu yake. Ni kwa sababu hiyo hatupaswi kuona vibaya kusema huu ni uozo wa CCM! Huu ni uozo wa serikali iliyoko madarakani.

Katika kufanya hivyo na ninaamin this is where youu have the strongest point, tusiidemonize nchi yetu, taifa letu au Watanzania wote. Hatuwezi kusema Tanzania iko hivi au vile au Watanzania wako hivi au vile; Ni haki kusema Utawala wa CCM... Utawala wa Mkapa..
 
Mh. Zitto,

Asante sana kwa taarifa hii angalau inatupa matumaini sisi wananchi kwamba kuna wawakilishi wetu huko mjengoni nao wako msituni wakitafuta nondo kwa ajili ya kutetea na kulinda maslahi ya nchi na wananchi wake, na pia kulinda sifa ya u-Tanzania wetu.

Je, baada ya huu ukweli kuanikwa swala hilo linaweza kurejeshwa Bungeni ili serikali iweze kutoa majibu sahihi? Nimeona kuna mmoja wetu amependekeza kuandaa Hoja Binafsi, nina mashaka hoja hiyo inaweza kuzimwa kiaina kwa kuzingatia mfumo wa Bunge letu kwamba lazima kwanza Spika ajiridhishe na hoja na ndipo anaruhusu hoja iwasilishwe mjengoni. Je, ikitokea hali hiyo, ufanyike mkakati gani ili kashfa hii iweze kufikia mwisho na wahusika washughulikiwe? Hili si swali la Mh. Zitto peke yake bali wana jamvi pia wanaweza kuweka mapendekezo yao, lengo ni kuongeza pressure ili serikali i-come out clean badala ya kufunika bovu na kutudanganya kwamba linahusu usalama wa Taifa.

Hivi kabla mtu hajateuliwa kuwa Waziri huwa hakuna Vetting? Mh. Masha awe Waziri wa Wizara nyeti kabisa na huku kampuni yake ilishiriki kwenye hizi dubious deals ambazo zinahatarisha usalama wa nchi yetu?

Swala la MEREMETA si swala la CCM wala wapinzani ni swala la Taifa zima kama watanzania. Iko siku haya yaliyofanywa na Meremeta yatakuja kufanyika Mombasa ama Uganda, tutakuja kulia na kusaga meno na hakuna atakayekuja kusikiliza kilio chetu. Kulikalia kimya swala hili ni sawa na kukubali kwamba sasa Tanzania ni uchochoro wa kupitisha silaha haramu. Silaha zinakuwa haramu pale ambapo mnunuzi hataki ajulikane ana malengo gani na hizo ndiyo zimesababisha sana mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Hizo hizo ndiyo zimezagaa Kagera na Kigoma, kiasi kwamba kuna baadhi ya mistu huwezi kupita bila escort ya polisi na hiyo si misitu ya mpakani la hasha bali ni ya ndani ya mipaka yetu.

Imefika wakati watanzania tunatakiwa kusema NO kwa sauti kubwa, usalama wetu uko hatarini. Leo silaha zinaenda Rwanda, Burundi na DRC ambao ni jirani zetu, kesho zitapita huko na zitakuja kutumaliza sisi, na nyingine zimeishaanza kutumaliza. Escort ya polisi unakuta landrover inefungwa Machine Gun na mnyororo wa risasi as if tuko vitani na haya ni matokeo ya hizi deals za Meremeta.
 
Kwa uchungu mkubwa inabidi nikiri na niseme wazi kuwa Lowassa was right aliposema kuwa suala la Meremeta ni la Usalama wa Taifa. Hata Pinda naye alipotoa kauli hiyo, alikuwa sawa kuwa ni sualala Usalama wa Taifa.

Lakini tunapozungumzia Usalama wa Taifa, je tunalipokea vipi na kufikiri linamaanisha nini?

Mwanzoni nilihoji, kwa nini Jeshi lipewe fedha uvunguni? Je kulikuwa na Covert Operation? Lakini kadri siku zinavyoendelea na nikendelea kuunganisha nukta zangu mithili ya Buibui kujenga utando wake, ndipo taswira halisi ya kilichotokea na maana ya maneno ya Mawaziri Wakuu wawili kuwa hili ni suala la Usalama wa Taifa.

Ni uamuzi wako kutafakari kwa kina nitakachokisema hapa chini na kama umesoma ile makala yangu ya "Tumeuza Uhuru wetu" https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/35092-tumeuza-uhuru-wetu-na-hazina-yetu-tumeifuja.html utaelewa ninachokizungumza hapa.

Suala la Meremeta si suala la wizi wa kujitajirisha kama EPA au kutumia fedha kwa uchaguzi kama Kagoda.

Suala la Meremeta kwangu ni Uhuru wetu kuwekwa rehani!

Swali ni hili, je viongozi wetu walifanya nini mpaka wakashikwa kende na kulazimishwa kufuja rasilimali zetu na kuwaruhusu Mamluki wafanye kazi Tanzania tena kwa mkataba na serikali yetu?

Kwa nini viongozi wote husika anzia Rais, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama waTaifa na wenginewe hawakutumikia viapo vyao vya utii kwa katiba na kuilinda Tanzania kutoka kwa maadui wa ndani na wa nje? Walifanya nini wakaasi viapo vyao na kuidhalilisha Katiba yetu?

Ni Woga gani ambao alikuwa nao Mkapa, Mboma, Apson na wengine mpaka wakakubali kumruhusu Viktor Bout, EO na wahuni wengine kujifanyia wanalotaka kwa baraka za viongozi wetu?

Ni maslahi gani waliyokuwa wakiyalinda na hata kuhakikisha kuwa mkono wetu unatumika kwa mhuri wa Ikulu kuruhusu vurugu za Kongo na Rwanda?

Je tulipokuwa tunasamehewa mikopo na Paris Club huku Waingereza na Tony Blair wakitusifu, ilikuwa ni takrima waliyopewa viongozi wetu ili kutupumbaza sisi wananchi tusijue kilichotendeka na kinachoendelea?

Ni kwa nini tumeuuza uhuru wetu na kukubali hazina yetu ichukuliwe kirahisi na tunadanganywa kuwa ni suala la Usalama wa Taifa?

Je ni suala la Usalama wa Taifa kwa kuwa tukikataa kutii matakwa ya EO, Blair na wengine, watahakikisha kilichotokea Rwanda na Congo kinatokea Tanzania?

Je ni suala la Usalama wa Taifa kwa kuwa tukijua ukweli kuwa udhaifu, uroho na tamaa za Uongozi wa Awamu ya Tatu (serikali kuu na vyombo vya Ulinzi na Usalama), basi ile aibu na hasira ya vitendo vya waliotoa rehani Uhuru na Hazina yetu zitazaa hasira na rabsha ndani ya nchi na hivyo kuvunja ile Amani, Mshimkamano na Utulivu?

Cha mwisho ninachoojiuliza, haya yote yamefanyika kwa manufaa ya nani?

Je ndio tumerudi kutawaliwa upya kwa hiari tukiwa na bendera yetu, lakini Hati ya Uhuru tuliyopewa usiku ule wa Disemba 9 1961 pale uwanja wa Taifa tumetishiwa kunyang'anywa kwa nguvu na hivyo tukaisalimisha kwa hiari ili kuficha aibu?

Ningekuwa mimi, ama ningejiuzulu kazi ili nisiliingize Taifa langu kwenye giza na mkasa kama huu na kama hiyo blackmail ingekuwa ni kuzidi kitakachoeleweka, Mwenyezi Mungu angebidi anisamehe pale ambapo kujiuzulu ingekuwa ni tabu na aibu na hivyo kujipiga risasi ya kichwa!

Walichokifanya Watanzania wote waliohusika na Meremeta, iwe ni Rais, Wakuu wa Usalama, Mawaziri, Makatibu wakuu au nyadhifa zozote ni UHAINI!
 
Hongereni wote mnaohangaika usiku na mchana kumkomboa Mtanzania.

Mh. Zitto pole na kazi za kila siku. najua unamajukumu mengi.
Leo nina swali dogo kuhusu wizi huu unaoendeshwa na serikali yetu kupitia njia na watu mbalimbali kiini kikiwa ni ikulu.

Je Bunge lina nafasi gani katika kupambana na uhalifu na wizi wa mali za wananchi hasa pale serikali inapokataa kutekeleza maamuzi ya Bunge, rejea Richmond saga.

Je bunge linaweza kutoa maamuzi ya kufikishwa wahalifu mahakamani bila ya serilikali kuhusishwa.

Na ni kwanini Bunge katika maamuzi yake lisitunge sheria au kuzisimamia sheria zinazotaka kila anayechunguzwa kutoka kwenye kazi husika ili achunguzwe bila longo longo nyingi.
Mfano, ilikuwaje bunge mkakubali uchunguzi wa Richmond uendelee kwa upande wa serikali bila kushinikiza wale wote wanaochunguzwa kutoka kwenye nafasi husika? hata kabla ya wabunge kusomewa taarifa ile ya Richmond bungeni ni wazi wahusika wasingeweza kujinyonga wenyewe?

Pili kama hatuna mfumo ulio imara wa uchunguzi hasa kwa wale wanaotuhumiwa kuchunguzwa na vyombo huru, ni vipi tutafikia na kuweza uchunguzi wa Meremeta ambao ni wizi uliohusisha serikali na vitengo nyeti kama usalama wa taifa, jeshi, na ikulu?

Na je sheria za bunge zinasemaje kwa wabunge waliohusishwa na makosa ya jinai pamaoja na rushwa kuendelea kuwepo bungeni, je maadili ya bunge ni nini? Je ni vipi kuwa na wabunge watuhumiwa wengi kuliko wahalifu mitaani kwa asilimia? Je bunge linajenga picha gani machoni kwa jamii na watoto
 
Well, swali linakuja hata tukijua ndio itakuwa nini? Mbona EPA tunajua na viongozi wetu wameambiwa lakini jibu walilotoa ni kuwa wanajua wahalfu lakini wanawaogopa. Kama hawa wa Meremeta sio ndio itakuwa wanaongopa hata kusema?

Mara 100 ni bora kujua kuliko kuambiwa kwamba ni suala la usalama wa taifa wakati tumegawa uhuru wetu kibwege halafu watu mnashabikia ujinga wa kufutiwa madeni hamjua hata chanzo. EPA watu wamejilia yameshapita na sidhani kama inahatarisha taifa kama hili la meremeta kwakweli kwa mlolongo huu MKJJ, ZITTO NA REV nafikiri leo wamenifungua macho. Ila mm ninabakia na usemi wangu "MWISHO WA UBAYA AIBU"
 
jamani hebu niooneeni huruma maana hichi kichwa kinataka attention ya shemeji yenu na anaona namuignore kwa kusoma haya madubwana!

laa haula wa laa kuwata illa billahi laadhim

khatari mambo haya
 
Well, swali linakuja hata tukijua ndio itakuwa nini? Mbona EPA tunajua na viongozi wetu wameambiwa lakini jibu walilotoa ni kuwa wanajua wahalfu lakini wanawaogopa. Kama hawa wa Meremeta sio ndio itakuwa wanaongopa hata kusema?
Mapambazuko yanaanza na jua kuchomoza kwa mbali sana. Kwa waliokuwepo, au kusoma historia ya uhuru wetu au wa nchi yeyeto ile mambo yalianza pole pole kabla ya vita yenyewe.

Kwanza uhuru haukupatikana 1961 kama inavyosomeka ila kilele chake kilikuwa 1961. Kitu cha kwanza kilianza ni watu kujua kwamba wao ndio wenye nchi na waingereza ni wezi, na wageni ndani ya nchi yao, na hilo halikushuka kama jua ila baadhi ya watu ndio walianza kupata mwangaza na kuanza kuwaelimisha wengine taratibu na kuhusisha umasikini, kazi ngumu, kubaguliwa na nchi yao ndipo baadhi waliaanza kuwachukia wazungu wale na wageni wengine na kuanza kupigania haki yao ambayo ni uhuru. sasa uhuru ukafikia kilele 1961 mwingireza akaachia.

Ila uhuru ule haukuwa kamili kwani tuliachwa tukiwa sisi ni masikini na wajanja wale wakoloni tayari walikuwa wamejenga matabaka na marafiki. (Hawa marafiki wa mkoloni)waliitwa vibaraka ambao waliachwa nyuma watumalize kwa staili nyingine, moja wapo ya kutufanya wazalishaji wa malighafi na kuuza kwa bei poa bila kutengeneza products, na wale wakuchombeza kuwarudisha wakoloni kwa mikataba feki.

Tulipo ni lazima wananchi wengi wamjue adui yao, ni lazima tujue kila aina ya uovu na madhara yake kwetu na ndugu zetu, huwezi kuunganisha nguvu bila kutoa elimu inayoeleweka , ni wajibu wa wasomi, wenye kuelewa wenye nyaraka na wanaona yanayofanyika wayaweke hadharani ili wale mama vitumbua nao wajue si lazima kuuza vitumbua ili watoto wao wasome, si lazima kutengeza kokoto kwa nyundo ili watoto wale, wasome na kutibiwa. Ni lazima wajue tungeweza kuwa na viwanda, mashamba, na madini kwa ajili yao na watoto wao huku wakipata huduma safi na bora za jamii kama maji, dawa, barabara na miundombinu mbalimbali.

Haya yote ni lazima wayajue ili tuweze kumtoa Meremeta ikulu, lazima wayajue ili tuweze kumtoa mwanamwali deepgreen ikulu, Richmond na vyeti fafa. Ni lazima wananchi wajue wanatakiwa kuandamana mpaka dodoma au ikulu kutaka walioshindwa nchi watoke wawaachie wenye nia na moyo.
 
Hongereni wote mnaohangaika usiku na mchana kumkomboa Mtanzania.

Mh. Zitto pole na kazi za kila siku. najua unamajukumu mengi.
Leo nina swali dogo kuhusu wizi huu unaoendeshwa na serikali yetu kupitia njia na watu mbalimbali kiini kikiwa ni ikulu.

Je Bunge lina nafasi gani katika kupambana na uhalifu na wizi wa mali za wananchi hasa pale serikali inapokataa kutekeleza maamuzi ya Bunge, rejea Richmond saga.

Je bunge linaweza kutoa maamuzi ya kufikishwa wahalifu mahakamani bila ya serilikali kuhusishwa.

Na ni kwanini Bunge katika maamuzi yake lisitunge sheria au kuzisimamia sheria zinazotaka kila anayechunguzwa kutoka kwenye kazi husika ili achunguzwe bila longo longo nyingi.
Mfano, ilikuwaje bunge mkakubali uchunguzi wa Richmond uendelee kwa upande wa serikali bila kushinikiza wale wote wanaochunguzwa kutoka kwenye nafasi husika? hata kabla ya wabunge kusomewa taarifa ile ya Richmond bungeni ni wazi wahusika wasingeweza kujinyonga wenyewe?

Pili kama hatuna mfumo ulio imara wa uchunguzi hasa kwa wale wanaotuhumiwa kuchunguzwa na vyombo huru, ni vipi tutafikia na kuweza uchunguzi wa Meremeta ambao ni wizi uliohusisha serikali na vitengo nyeti kama usalama wa taifa, jeshi, na ikulu?

Na je sheria za bunge zinasemaje kwa wabunge waliohusishwa na makosa ya jinai pamaoja na rushwa kuendelea kuwepo bungeni, je maadili ya bunge ni nini? Je ni vipi kuwa na wabunge watuhumiwa wengi kuliko wahalifu mitaani kwa asilimia? Je bunge linajenga picha gani machoni kwa jamii na watoto
Na hasa ikichukuliwa kuwa hata watumishi wa umma wanapokuwa na kesi au tuhuma usimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi? Sasa hawa walio na tuhuma na kesi mahakamani kwa nini wanaendelea kuruhusiwa kukaa bungeni?
 
Niliipitia halfway infact kazi imefanyika big up Mkjj, ingawa hawa viongozi wetu wana macho lakini hawaoni na wana masikio lakini hawasikii. Heritage Oil ndo hiyoo inaendelea kufanya utafiti wa mafuta tutapona kweli ndani ya kinywa cha mercenary soldiers!!?
 
Mungu Akubariki Babu yangu sana na tena Nitakuongezea Panga, Shoka, Na nyundo ili uzidi kuchimba zaidi, Asante na Mungu akufiche zaidi na akupe moyo wa ujasiri zaidi babu yangu
 
Nimeamua kutoa photocopy ya hii ripoti katika condensed form (i.e. not on an a4 size paper kuibind) na kuigawa bure kwa malengo.

Kitabu cha LINKED by Albert Barabasi kimenisaidia kwamba nagawa kwa watu wanaojulikana kama NODES kwenye society.

Asante Mwkjj and the rest. Hakuna mtanzania yeyote anayethamini utanzania na utu wake anaweza akasoma hii ripoti, akaielewa na kupuuzia.
 
..i am speechless.

..Mwanakijiji na wenzako kazi nzuri.

..sasa kuna uwezekano yapo madubwana mengine mengi tu ya mfano wa kashfa ya Meremeta.
 
Poleni wote na Lazima tujipe Pole sisi Watanzania kwa kuona kuwa Tanzania linakuwa shamba la bibi kwa kipindi kwa sasa. Kuna haja ya kufanya mabadiliko ya haraka sana
 
Back
Top Bottom